Leo siku muhimu kwa mzee wetu Alhaj Mohamed Said; Happy birthday Mzee wetu!

Mashallah,Allah amzidishie maisha mema,ampe mwisho mema,amuongezee mapenzi ya waja wake,amuongezee mapenzi ya Allah,na amuongezee busara na hekima na namukmba Allah amuingize peponi kwa rehma zake yy na familia yake yote.
Aamiin.
 
Pohamba,
Hizi ''bashing,'' unazozielekeza kwangu na kejeli si ngeni katika maisha
yangu.

Inawezekana ukawa unaumia labda kwa kuwa wewe huna historia ya
kueleza.

Mimi nina historia ya kueleza na inavutia nikianza na babu yangu mkuu
aliyeingia Tanganyika kutokea Belgian Congo katika miaka ya mwisho
ya 1880 kama askari katika jeshi la Wajerumani.

Nayajua mengi katika maisha yake.

Halikadhalika ya mwanae ambae ni kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika
na alizaliwa katika Boma ya Shirati Musoma.

Najua maisha ya babu yangu na mchango wake katika kupigania uhuru wa
Tanganyika baada ya kutoka Zanzibar alipopelekwa na baba yake kusoma
dini.

pGFMqHiD_JcEdikjw11_LJCp8Sjy1Whe28khv7mUvCeWxs9Z7Os-gDhcVpeNmMutOCxlcaa7Gq5vPhm-3lHYAuvCW6jWLhP8H_kPiQVmQOKjys_1KJr8HxNzUzul10qtuWY6_bsJNqwM3PIFrE83atS0iTjuo_3PYnslPw66DVkKeJHS3iqdq6Akk-D25_nFavAw2spWvdgjHCER2LkSU32KFGctvYXQ-PhO4_zWjnlTVa1QH33ibhmiKqmpzH8bkdFqmoqWnhLkUZ_rSXMcyCf6FrXr_0uW1SIZFNhDmXrDIz1osWzRRcSqsvxqDH4VPr7VdmuKrU1KO4hfqdUlUoookD8haEWNC-35dRPO91OXsrriJoHPuwmKjlHEZ_ISq5DlfJ6qf9qQz1iUTE8HwODTn5q_L2XTBaXMtOls9eF6O5oL6HbKUXSnnRjl3KZhkdBvm3_sB_-zQi0II3GQiPQ2vE4ivL_lkuDyliTsJmMFi5n4G7qyIOpebSban1H5tAztyDuMciFO9hlDBKJuoVE7YUYD8sXvVvtcI4Ja74Nyxrq8lie2d_laLJkDmsUmA0ED0mBKDCcGf-rnNe6-ejne6ehsXwqPTTgkxdjCRkTM2fw7IVsknw=w459-h692-no

Bibi Popo hii picha nimempiga mimi Tabora 1965

Najua maisha ya bibi yangu mkuu Bibi Popo aliyechukuliwa
utumwani 1880s Kongo akaletwa Tanganyika akiwa msichana mdogo.

Ninajua mengi sana na si ya Dar es Salaam tu.

Kuanzia kwenye asili yetu Manyema hadi Musoma hadi Tabora na Dar es
Salaam yote nimesomeshwa na wazee wangu.

Ikiwa historia ninayoandika inakukera hulazimishwi kusoma unaweza bila
shida ukaruka tu ukasoma vile vinavyokupendeza.

Haipendezi kuja hapa JF kutukana watu bila ya sababu.
Huu si uungwana.
santeeeeee,kama akchukia akale malimau apunguze maumivu
 
Mashallah,Allah amzidishie maisha mema,ampe mwisho mema,amuongezee mapenzi ya waja wake,amuongezee mapenzi ya Allah,na amuongezee busara na hekima na namukmba Allah amuingize peponi kwa rehma zake yy na familia yake yote.
Aamiin.
Albuluushiy,
Allahuma Amin ndugu yangu.
 
Mtanganyika...
Siku hizi nimekuwa "celebrity of sorts," näpokea wageni kila siku
kutoka kila pembe ya dunia na mwisho wa mazungumzo ni kupiga
picha.

Wanapenda kunisikiliza.
Alhamdulilah.
 
Huyu mzee ni johari na bohari la historia ya nchi. Kafungua bohari hilo na kukuta mengi tulikua hatuyajui au yamefunikwa.
Pongezi mzee na Mungu akupe afya na maisha marefu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom