Leo siku muhimu kwa mzee wetu Alhaj Mohamed Said; Happy birthday Mzee wetu!

Heri ya kuzaliwa Mzee Mohamed Said, Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu.

Binafsi nakushuru kwa mchango wako katika kufanya marejeo sahihi ya historia yetu. Wakati mwingine sikubaliani nawe hasa unapoingiza mambo ya kidini ila nakukubali wewe na Dr. Ghassany kwa kuwa walau mnaeleza historia na vielelezo visivyotia shaka.
 
Heri ya kuzaliwa mzee Mohammad said napenda simulizi zako! kuanzia za uhuru wa tanganyika hadi maisha yako na rafiki zako enzi hizo!! Hakika uliishi! Uliutumia vyema muda wako!!for each stage of your life there is a tale to tell!! Mungu akupe maisha! Amen
 
Heri ya kuzaliwa Mzee wetu. Allah akulinde na shari za viumbe wanaoonekana na wasioonekana.
 
Tatizo lake anaamini Tanzania ni Kariakoo na Msimbazi.Kwa hiyo anakupigia hadithi ndeefu za mitaa ya Msimbazi mpaka unachoka mwishowe anamlaumu mwalimu kwa kutowapendelea wazee wake.

Namshauri wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa ajitahidi kuandika historia ya Dar es salaam.Afike na maeneo ya Kinondoni na Buguruni.



Akimaliza ya Kinondoni na Buguruni utahoji kwanini Historia ya Majohe na Malamba mawili haijaandikwa?

Kinondoni na Buguruni Enzi hizo ilikuwa Pori tu
 
Heri ya kuzaliwa mzee Mohammad said napenda simulizi zako! kuanzia za uhuru wa tanganyika hadi maisha yako na rafiki zako enzi hizo!! Hakika uliishi! Uliutumia vyema muda wako!!for each stage of your life there is a tale to tell!! Mungu akupe maisha! Amen
Capt...
Ahsante sana.
Amin kwa dua yako.

Namshukuru sana Mungu kuwa mimi nilipata bahati kati ya wenzangu
kupata malezi ambayo kiasi fulani yalikuwa tofauti na yale wengi wetu
tulipitia.

Nimewaona watu mashuhuri na kujuananao nikiwa mtoto mdogo sana.

Wakati ule sikufahamu wala sikijua kama hawa ndiyo watu walioandika
historia ya Afrika ya Mashaariki.

Nimemjua Peter Colmore, Jim Bailey Wazungu waliotajirika katika ukoloni
kwa kufanya kazi na Waafrika wakiwachukua, ''as equals.''

Nimefahamiana na Dome Okochi Budohi kiongozi katika TAA na mmoja wa
wanachama wa mwanzo wa TANU akiwa na kadi no. 6.

Baba yangu alinifunza kuishi maisha wenzangu wengi hawakuyapata utotoni.
Nivae vipi, rangi gani ya shati kwa suruali gani na kiatu rangi gani.

Tofauti ya ''blazer,'' na coat.
Wapi uvae, ''blazer,'' na wapi uvae suti.

Akinichukua kuangalia ''movies classics,'' akinieleza historia ya mji wa Dar es
Salaam na wenyeji wake.

Nani baba yake nani.
Jamaa gani alioa, ''Beauty Queen,'' wa enzi zao na ni dada yake nani.

Mzee alikuwa mtu wa taaradhi sana.

Namna ya kusoma menu na kuagiza chakula na mwisho kumaliza na dessert
ipi nk. nk.

Kusikiza muziki na kuupenda...

Akisikiza jazz ya Lois Armastrong, Victor Sylvester and His Orchestra,
Bing Crosby, muziki wa Cuba wa Sextet Habanero... kwa hakika mambo
mengi.

Sijui kati yake yeye na Abdul Sykes ni nani alikuwa na, ''collection,'' kubwa ya
muziki.

Huwa sie watoto tukikutana huwa tunakumbushana mambo ya wazee hawa.
Huwa tunacheka sana.

Hawa wazee wetu waliathirika sana na, ''colonial lifestyle.''
Chai ya saa kumi na biskuti au keki ilikuwa kila siku.

Huenda hawa wazee wetu walituachia chembechembe za hizi, ''taste,'' zao za
kikoloni.

7w9bMxTugXeWCwW7cija9BFQHc0aFWUpqnjU2LnAtVByUohjC0u83M3FM-jow8spm7zFGKlhAMGTgQH9Hn2kJRTp7eCks6S_zPqJfSmrB_F80mkKK5r5vnLvxeW4qCVwzxKjJIGz-IKhNrafZgNJwivDLcOE19rJ_xHhMC5mQzuvF2HjGl-1fVdNjBDwjq3i7b_hYg3apPPHDuvT3eSOsESOQfB9Ww42Su8FD59TC1qLO79Ul60ln7Q4-_1ZiJHP15Y5aobPE16xujdcjYiGR0OU-1Xu05mu3_wsUJB5mjPUIZZBHD9SgzFAKtGfvUHQbYbmxU-FoKfAUZjvlLyhifzHI177W5vGWir8TwwV4rcd5nAqKjTTOBMDL3heqRQx7g_Cmi8NIkqwblxib0kHaTyOkm5VzQdChbQrj5tZ-IX_f71cA8jCv5PJ3__a8FC_vzDGmjZjN7sKpJyfG9bVcTotCeOfyxTfaC1fZxKxGTAizEVVY9h1bgEY3eoXcfbcGHwrLd5huNtFcnGLdOXEB7gEm403xPqjww_cSrh8ofe34YxiIZeRimD-9ymV5ehVqO7mNkPjfr0ZuPaBo_otr1jjyS0MJ8t-DDqoUrIGzExX8aVd=w923-h692-no

Peter Colmore na Mwandishi Muthaiga, Nairobi 1995
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom