Leo siku muhimu kwa mzee wetu Alhaj Mohamed Said; Happy birthday Mzee wetu!

Heri ya kuzaliwa mzee wetu Allah akuzidishie kila lenye kheri na jema, endelea kutuletea historia muhimu ya nchi yetu. Happy Birthday mzee Mohamed Said.
 

Begiu
Akimaliza ya Kinondoni na Buguruni utahoji kwanini Historia ya Majohe na Malamba mawili haijaandikwa?

Kinondoni na Buguruni Enzi hizo ilikuwa Pori tu
Pohamba,
Hizi ''bashing,'' unazozielekeza kwangu na kejeli si ngeni katika maisha
yangu.

Inawezekana ukawa unaumia labda kwa kuwa wewe huna historia ya
kueleza.

Mimi nina historia ya kueleza na inavutia nikianza na babu yangu mkuu
aliyeingia Tanganyika kutokea Belgian Congo katika miaka ya mwisho
ya 1880 kama askari katika jeshi la Wajerumani.

Nayajua mengi katika maisha yake.

Halikadhalika ya mwanae ambae ni kizazi cha kwanza kuzaliwa Tanganyika
na alizaliwa katika Boma ya Shirati Musoma.

Najua maisha ya babu yangu na mchango wake katika kupigania uhuru wa
Tanganyika baada ya kutoka Zanzibar alipopelekwa na baba yake kusoma
dini.

pGFMqHiD_JcEdikjw11_LJCp8Sjy1Whe28khv7mUvCeWxs9Z7Os-gDhcVpeNmMutOCxlcaa7Gq5vPhm-3lHYAuvCW6jWLhP8H_kPiQVmQOKjys_1KJr8HxNzUzul10qtuWY6_bsJNqwM3PIFrE83atS0iTjuo_3PYnslPw66DVkKeJHS3iqdq6Akk-D25_nFavAw2spWvdgjHCER2LkSU32KFGctvYXQ-PhO4_zWjnlTVa1QH33ibhmiKqmpzH8bkdFqmoqWnhLkUZ_rSXMcyCf6FrXr_0uW1SIZFNhDmXrDIz1osWzRRcSqsvxqDH4VPr7VdmuKrU1KO4hfqdUlUoookD8haEWNC-35dRPO91OXsrriJoHPuwmKjlHEZ_ISq5DlfJ6qf9qQz1iUTE8HwODTn5q_L2XTBaXMtOls9eF6O5oL6HbKUXSnnRjl3KZhkdBvm3_sB_-zQi0II3GQiPQ2vE4ivL_lkuDyliTsJmMFi5n4G7qyIOpebSban1H5tAztyDuMciFO9hlDBKJuoVE7YUYD8sXvVvtcI4Ja74Nyxrq8lie2d_laLJkDmsUmA0ED0mBKDCcGf-rnNe6-ejne6ehsXwqPTTgkxdjCRkTM2fw7IVsknw=w459-h692-no

Bibi Popo hii picha nimempiga mimi Tabora 1965

Najua maisha ya bibi yangu mkuu Bibi Popo aliyechukuliwa
utumwani 1880s Kongo akaletwa Tanganyika akiwa msichana mdogo.

Ninajua mengi sana na si ya Dar es Salaam tu.

Kuanzia kwenye asili yetu Manyema hadi Musoma hadi Tabora na Dar es
Salaam yote nimesomeshwa na wazee wangu.

Ikiwa historia ninayoandika inakukera hulazimishwi kusoma unaweza bila
shida ukaruka tu ukasoma vile vinavyokupendeza.

Haipendezi kuja hapa JF kutukana watu bila ya sababu.
Huu si uungwana.
 
Mzee Mohamed au yeyote ambaye anafahamu alipo au contacts zaUstaadhi Mohamed Kasim Lulengelule naomba ani inbox. Natanguliza shukran.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom