Leo sabasaba, tunakumbuka kuzaliwa kwa TANU, tarehe 7/7/1954

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,003
20,662
Leo ni siku iliyozaliwa TANU, tushereheke birthday ya chama pendwa na kongwe iliyozaa CCM.

CCM ni kama maji, usipoyanywa utayaoga. Leo hata Chadema hawajaenda maofisini wakisherekea kuzaliwa kwa chama hiki kilichoendesha Siasa za ukombozi Afrika. Nani alikuwa haijui code ya 7-7? Ndio hiyo, lift the veil, you find the green party!

====

Asili ya Saba Saba ilikuwa kuundwa kwa chama cha Tanganyika African National Union (TANU) kwenye tarehe 7 Julai ya mwaka 1954. Chama hiki kiliongozwa na Julius Nyerere kikawa chama tawala wakati wa uhuru wa Tanganyika kilichoendelea kuongoza siasa ya nchi baada ya kushika viti vyote vya bunge.

Mwaka 1963 Nyerere pamoja na uongozi wa chama waliamua kupeleka nchi kwenye mfumo wa chama kimoja kisheria. Hivyo mwaka 1964 siku ya kuzaliwa kwa chama yaani "Saba Saba Day" iliorodheshwa katika sheria ya sikukuu za umma (Public Holidays Ordinance Act)

Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 07/07/1954 ndipo chama cha TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION(TAA) kiliungana na chama cha AFRICAN ASSOCIATION (AA) Kuunda chama kimoja kijulikanacha kama TANGANYIKA AFRICAN NATIONAL UNION (TANU).

Mara tu baada ya UHURU wa Tanganyika, serikali ilihimiza suala zima la kilimo ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza uchumi na kuleta ustawi mzuri kwa wananchi wa Tanzania. Jambo hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani wananchi walipata elimu ya kutosha kuhusiana na kilimo, pia iliamuliwa kuwa kila kiongozi wa chama lazima awe na shamba la mfano ili wananchi waweze kujifunza kutoka kwao. Hapo ndipo ilipoanzishwa sera ya SIASA NI KILIMO.
Hivyo, kila mwaka kukawa na maonesho ya sabasaba lengo likiwa ni kuonesha kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa TANU pia kukumbuka malengo ya msingi ya chama cha TANU ambapo ni pamoja na kuendeleza kilimo ambacho ni UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU

Nafasi hiyo ilitumika pia na wakufunzi pamoja na wanafunzi wa vyuo vya kilimo hususani chuo cha SUA (SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE)kuonesha ugunduzi wa mbegu mpya za kisasa, dawa bora za kuua wadudu au mbinu mpya ya kuongeza mazao ya kilimo. Kwa wakati huo serikali ilijali sana kazi za wakulima hata kutenga siku maalumu kwa ajili yao, ndio maana siku hizi karibu kila mkoa kuna eneo linaitwa sabasaba ambayo ni maeneo ya kibiasha.
Kitu cha kushangaza ikafika kipindi wakulima hao ambao ni siku yao ya kuonesha mazao ya kazi za mikono yao wakawa wanatozwa pesa za kuingilia na kulipia eneo ambalo watakuwa wanafanya biashara zao, kitu ambacho ni tofauti kabisa na malengo ya siku hiyo ya sabasaba.
Kadiri miaka ilivyozidi kwenda, ndipo wakulima wakawa wanashindwa kuja kuonesha bidhaa zao kutokana na gharama kubwa zilizokuwa zikitozwa. Nafasi ya wakulima ikachukuliwa na wafanyabiashara ambao walikuwa wanaweza kulipia gharama zote ambazo walikuwa wakitozwa, na mpaka sasa adhma ya sabasaba kuwa ni siku ya WAKULIMA imegeuzwa na kua siku ya WAFANYABIASHARA tena wa viwandani.

Kutokana na unyonge wa wakulima wetu ikabidi wapewe siku nyingone ambayo ni siku ya nane nane ili waweze kuadhimisha siku ya kilimo rasmi badala ya siku ya sabasaba kama ilivyo hapo awali na mpaka sasa wakukima huadhimisha siku yao ya nanenane na wafanyabiashara huadhimisha siku ya sabasaba, kitu ambacho ni tofauti na malengo yaliyowekwa na TANU.
 
Asante kwa historia adhimu.
Sikuwahi kulifahamu hili kwa undani huu.
Nachokumbuka miaka ya nyuma ningali mdogo, kuna shairi tulikuwa tukiimba shuleni. Sehemu ya maneno niyakumbukayo ni kama ifuatavyo;-

"Karibu na tuwashukuru, Nyerere na Karume,
Tulianza Julai saba, wakoloni kuwakaba,
Sikukuu ya saba saba."
 
..Ccm inakwenda kuzaa chama kipya kitakachoitwa Dp World.
katika miaka 30 ya karibuni ya Ccm imepitia vimbunga viwili vikubwa zaid na ikatoka salama

1993 upepo wa Njelu Kasaka na G55 na upepo wa ulipo tupo wa 2015

vingine ni vinyamkera tu
 
Back
Top Bottom