Leo nisipokufa basi sifi tena

Leo nisipokufa basi sifi tena

GRAMAA

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,327
Reaction score
4,250
Ndani ya muda huu rafiki yangu ameniletea taarifa kwamba mke wangu mama Neema ananisaliti ndani ya gesti moja mjini Mwanza.Rafiki yangu ameniambia kamuana akiingia gesti na jamaa mmoja ambaye ni jirani yetu anayefanya kazi TANESCO.

Nimejalibu kumpigia simu mke wangu mama Neema anasema yupo Mabatini kwa dada yake anaumwa.Rafiki yangu ananilazimisha twende kwenye hiyo gesti tukafumanie.Kwakweli nimechanganyikiwa sana mapigo ya moyo yamebadilika.

Wadau busara ni nini hapa niende gesti au nisiende? Maana hata sielewi kabisa.
 
Bora ununue bia baridi......kaa kwenye TV......mtizame Magufuli na Majaliwa wakishiriki usafi.......msubiri mama Neema arudi nyumbani mlale.......kwanza kushakua usiku saa hizi..........
 
Ha ha haa ni Pm nikusindikize najua itakua mitaa ya Kirumba tuu
 
Achana na maneno ya watu mkuu. Maneno yanavunja unyumba. Akirudi mpige busu na big hug kisha maisha yaendelee bila kusahau kuulizia hali ya mgonjwa
 
Dah pole sana mkuu, ila cha zaidi action ya kufanya lolote iko mikononi mwako ,but ukikuta kwel Ana chepuka wee usiongee chochote rudi hom , tafuta bongo movie "Oprah my wife "
 
Pole mkuu ndoa inahitaji jicho la nne maana la tatu lishatumbuliwa halitaona...pole sana
 
Ita watu wawili uende nao ili usije ukafanya maamuzi mabaya. Ila andaa kabisa taraka yake akirudi aikute
 
Usije ukaenda halafu goni lako likaishia kukupa "Hapa Kazi Tu" Kuchapiwa ni siri ya ndani. Vumilia!
 
Acha presha baba, wanawake ni wengi..... Usijeenda na ukaua mtu maisha yako yatayumba.... Muwaze mtoto zaidi!
 
Andaa talaka nenda, fika kabidhi hiyo talaka afu sepa
 
Kamanda kauka, uende guest kufanya nini? Jamaa anaweza akakuzulu bure katika kujihami. Wewe kesho asbhi sana anzia kwa huyo ndugu yake. halafu mmsubiri anapokuja. Akifika tu unamsalimia na kuondoka zako kurudi kwako. Yeye ndoo atachagua kuja kwako au kuhamia kwa TAnesco
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom