Leo nimetimiza miak 3 ya ndoa

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Wapendwa wana wa JF, napenda kuungana nanyi katika kusherehekea miaka 3 ya ndoa na miaka 11 ya mahusiano na my wife wangu. Ni jambo dhahiri kuwa kufikia hapa tumevuka milima na mabonde mengi lakini kila wakati sala imekuwa ndo nguzo yetu. mungu ameijalia ndoa yetu watoto waiwili wa kiume na kike. nazidi kuwaombea wote waliopo kwenye ndoa na wale pia wanaotarajia kujiunga na chama hili kheri na baraka tele. Mungu awe kiongozi wenu daima.
 
Kila heri na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu, awajalie amani, upendo na furaha siku zote katika ndoa yenu.
 
Hongera sana kaka Mungu awabariki na azidi kuwapigania mzidi kuzidisha upendo kwny ndoa yenu!
 
Ngangali & Aggrey nashukuru kwa matashi yenu mema
 
Miaka 3 ya ndoa, 11 ya mahusiano? Imekaaje hapa, ufafanuzi plz. Anyway hongeren sana, na mwenyezi Mungu awajaalie hata zaidi.
 
aisee kwa hali ya sasa hongereni sana kwa moyo mkunjufu napenda kusema mungu awe nanyi na baraka tele awajazie
 
Congratulation 7.gif
Hongera sana.
 
Wapendwa wana wa JF, napenda kuungana nanyi katika kusherehekea miaka 3 ya ndoa na miaka 11 ya mahusiano na my wife wangu. Ni jambo dhahiri kuwa kufikia hapa tumevuka milima na mabonde mengi lakini kila wakati sala imekuwa ndo nguzo yetu. mungu ameijalia ndoa yetu watoto waiwili wa kiume na kike. nazidi kuwaombea wote waliopo kwenye ndoa na wale pia wanaotarajia kujiunga na chama hili kheri na baraka tele. Mungu awe kiongozi wenu daima.

Hizo bluu zimenipa wasiwasi sana
 
Hongera sana mwenyezi mungu aendelee kuwalinda na kuwaongoza katika ndoa yenu
 
Unastahili Pongezi... ila kumbuka you still have a long way to go...
 
Miaka mitatu ya ndoa kwa kipindi hiki ni mingi sana!
Wazazi wetu kipindi chao miaka mitatu ndoa ilikuwa bado mbichi sana hata uwezi kuitwa kutatua mgogoro hata wa mbuzi.
Hongereni sana
 
Hongera sana. Mungu awajaalie maisha mema. Furaha itawale familia yenu.
 
Back
Top Bottom