Leo nimepata jibu kwanini Waethiopia wanakimbia nchi yao

Kwa taarifa tunazosikia ni kwamba uchumi wa Ethiopia ni kati ya uchumi ambao unakuwa kwa kasi. bura siyo train wala fly overs tu, inabidi vyote viende sambamba na kuboresha kipato cha mwananchi wa kawaida.
Ethiopia na Somalia zinatuchanganya wengi.
 
Ni kweli kabisa nchi nyingi za ulaya zimepitia mambo mabaya zaidi, kama kunyanyaswa wanawake, ajira/vibarua vigumu ujira mdogo, child labour ambayo haielezeki, wakati huo watawala wafalme na familia zao,au koo zao wanatukuzwa kama miungu, ILa baada ya miaaka mingi ya kupaza sauti na harakati za kupinga uonevu na unyanyasaji wa watawala leo hii nchi nyingi za ulaya Kuwa kiongozi wa kisiasa ni kujitolea zaidi maana hakuna maslahi makubwa kuliko wajiliwa wengine wa serikali, pia hata wala huwi mtu wa kuogopwa sana

ila sisi badala ya kujifunya mema tunataka tupitia huko walipopita wao, wanasiasa wetu wajiona wao ndio first class citizen hapa nchini, wanalipana mishahara na maposho makubwa hata maprof, mainjinia, ma dr hawaoni ndani, ndio maaana watalamu wote tz wanataka kuwa wanasiasa kupata easy money maaana wanasiasa hamna kitu wanafanya pale dodoma mjengoni, zaidi ya kupiga umbea tu......

Nchi yetu wanasiasa (wabunge,mawaziri, wateule wa raisi dc,rc,ma ceo uchwara maana tasisi zetu ziko hoi kwa rushwa na ineffeciency. Makatibu wakuu, mabalozi na nk) mishahara yao pamoja na posho nizaidi ya 50% ya wage bill yote ya watumishi wa umma (yaaani hela zetu za kodi zinawahudumia hawa tu kwa kiasi kikubwa)
Umemaliza kabisa, na mwisho wa siku lazima yetokee madaraja ktk jamii yetu,madaraja ya kudumu. Kama hayo ya Ethiopia. Hapo ndiko yaliyo tukia ufaransa yatakuwa hayazuiliki kutukia.
 
Nchi za magharibi zlifuata mtindo huu zamani. Ni mapinduzi ya Ufaransa ndiyo yaliamsha watu. Viongozi walianza kuiangalia social benefits kama kishawishi kwa wapiga kura.

Kila kiongozi alikuja na manifesto ya elimu, afya, makazi, ajira na pesa za kujikimu kwa wasio na kazi.

Raia wanapopata mahitaji muhimu hawana muda wa kuilalamikia serikali. Mipango makubwa ya maendeleo inapata nafasi.
nakupenda sana mdada upo knowledagable sana huwa unanifurahisha sana
 
Back
Top Bottom