elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,260
- 9,698
Kwa taarifa tunazosikia ni kwamba uchumi wa Ethiopia ni kati ya uchumi ambao unakuwa kwa kasi. Wanajenga miundombinu safi, wamezindua train safi ya umeme na mambo kadha wa kadha.
Ila siku zote nilikuwa najiuliza, ni kwanini kila mara waethiopia wanahatarisha maisha yao, wanakubari kubebwa kwenye makontena kupita Tanzania kwenda Afrika ya Kusini na wengine wanafia njiani.
Siyo hao tu kuna wa Ethiopia walichinjwa na ISIS huko Libya wakiwa wanajaribu kufikia bahari ya Mediteranean wapate kuvuka kuingia Italy.
Katika pitapita zangu huko mtandaoni nikajiunga na group la Waethiopia, katika kuchat na mmoja ndipo akaniambia yeye kamaliza degree, ameajiriwa serikalini kama messenger.
Mshahara wake ni kama USD 50 kwa mwezi. Nikashangaa maana kuna muda nimemtajia USD 500, akasema huo ni mshara wake wa miezi kumi. Akaanza kunieleza kuwa serikali inajenga miundombinu, ikitaka aminisha dunia kuwa uchumi unakuwa lakini maisha ya raia wa kawaida ni magumu sana sana.
Anadai kupata kazi ni vigumu labda uwe una pesa ya kuhonga au unamjua mtu mkubwa serikalini.
Akaniambia yeye ana degree ila ni messenger ila boss wake pale kazini ana diploma. Akaniambia ya kwamba watu wengi hawana chakula hawajui watakula nini, ila watawala wanajilipa mishara mikubwa na wanaishi maisha ya kifahari.
Uhuru wa kuongea hakuna ukileta kelele kukuua hawaoni hatari.
Anadai kukiwa na mikutano ya kimataifa, omba omba na watu wanaonyesha umasikini wanaondolewa wote addis ababa mpaka mkutano utakapoisha huwezi kuona masikini na omba omba. Nimekaa nikatafakari nikaona maendeleo na maisha bura siyo train wala fly overs tu, inabidi vyote viende sambamba na kuboresha kipato cha mwananchi wa kawaida.