G'taxi
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 6,565
- 8,427
Ktk mambo kama haya ndipo hua nasema waTanzania wamezoe kuiponda nchi yao na kusifia vya nje ilihali ukipata mwanya wa kutembea nchi kadhaa duniani hasa hizi hizi za Africa ukijitambulisha kua unatokea Tanzania wanafurahi na kuona wewe unatokea Kaanani.hapa kwetu ni kweli kuna mapungufu kibinadamu na kimaisha kwa ujumla hutakosa changamoto lakini bado tuna nafuu kuliko mataifa mengi sana,cha msingi kwetu labda Serikali ingetilia mkazo wa kuwekeza kwenye kilimo tungetoka,lakini hizi nyimbo za kila siku za wasomi kusema wanatoka vyuoni na hakuna ajira,hii haitabadilika duniani kote,ni ngumu kuikuta Serikali inatoa ajira mamilion ktk kila mwaka wanaomaliza vijana masomo vyuoni.ushauli wangu kwa vijana tujikite kua na shughuli binafsi hasa kilimo bila kujali usafi wa mwili,elimu yako wala uwezo kifedha.nguvu za mtu na akili yake inaweza kuzaa matokeo ya kiuchumi maana hata Serikali ikiona umetandaza shamba la mahindi hapo yaliyopendeza,mpunga,maharage,heka za kutosha.Serikali kupitia idara zake ktk halimashauli wanaweza kukupeni mkono wa msaada.tatizo sisi waTanzania tumekalia lawama tu bila kutenda kwanza kwa nguvu zetu na kuonyesha uwezo wa kufikili ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
JAH RASTAFARI MORNING AFRICA