Leo nimepata jibu kwanini Waethiopia wanakimbia nchi yao

..Uhuru wa kuongea hakuna ukileta kelele kukuua hawaoni hatari.

Ethiopia hata kuaccess social media kama WhatsApp, Facebook etc ni tatizo kubwa na kama huna app nzuri ya VPN, hutopata kitu. Access ya maana ipo kwenye UN compounds tu labda na Hotels zenye hadhi ya kuanzia nyota tatu. Kuna kampuni moja tu ya simu - ya Serikali. Infact wanamonitor communications zote. Uhuru wa kuongea ni almost haupo.
 
Katika pitapita zangu huko mtandaoni nikajiunga na group la Waethiopia, katika kuchat na mmoja ndipo akaniambia yeye kamaliza degree, ameajiriwa serikalini kama messenger.
Mshahara wake ni kama USD 50 kwa mwezi.
umeongea na asiejua kuitumia degree yake vizuri
wanachokimbilia ughaibuni wangeweza kukifanya kwao
 
Poleni waethiopia. Kwakweli nilivyoluwa mdogo sikujua athari ya kiongozi kwa watu. Kuwa uyaone.
 
Nchi za magharibi zlifuata mtindo huu zamani. Ni mapinduzi ya Ufaransa ndiyo yaliamsha watu. Viongozi walianza kuiangalia social benefits kama kishawishi kwa wapiga kura.

Kila kiongozi alikuja na manifesto ya elimu, afya, makazi, ajira na pesa za kujikimu kwa wasio na kazi.

Raia wanapopata mahitaji muhimu hawana muda wa kuilalamikia serikali. Mipango makubwa ya maendeleo inapata nafasi.
asante...!
 
Elmagnifico ulikua hujajua tu all these years na documentary zote zilizojaa mitandaoni? Hao jamaa wanaishi kama wako in hell. Kodi ni nyingi si mchezo, kodi mpaka kwenye biashara kama za genge, ambavyo hapa kwetu ni tofauti.
 
Kweli aisee
 
umeongea na mpumbavu mmoja asiejua kuitumia degree yake vizuri
Akili yao ni ndogo sana wanachokimbilia ughaibuni wangeweza kukifanya kwao
samahani! umesoma hadi kiwango gani? Ulishawahi kusoma pamoja na Waethiopia? usiwadharau watu kama huna taarifa za kina.
Elimu ya Ethiopia ni nzuri sana kuliko ya kwetu na Wakushi wana IQ kubwa sana inawezekana kuliko Wabantu wetu wa huku Bongo. Mimi nimesoma nao hawa majamaa. wapo vizuri sana. Tatizo la Ethiopia ni kimfumo wa uchumi na utawala. Serikali ndo inayomiliki uchumi kuliko raia. Kule serikali ndo yenye hela, imewekeza sana katika Jeshi, uraiani hali ni mbaya sana. Hakuna ajira, fedha hazipo katika mzunguko. Pia kumbuka Ethiopia ina idadi kubwa sana ya watu. Ni ya pili katika Afrika kuwa na idadi ,kubwa ya watu baada ya Nigeria, ikifuatiwa na Misri, Congo DRC then tunafuata sisi Tanzania. Ethiopia upande wa Magharibi na kusini mwa nchi ni jangwa. Ukijumlisha haya matatizo yote ya uwingi wa watu, ukame/jangwa, uhaba wa fedha katika mzunguko, ukosefu wa ajira, ukandamizaji wa kidemokrasia n.k hali inakuwa mbaya sana kwa raia. Ndo maana pamoja uchumi unaosifika kwa ukuaji katika bara la Afrika, raia wake kila siku wanafia njia wakiwa katika harakati za kuzamia nchi zingine.
 
Usichoke kuwahabarisha wasiojua lakini wanadhani wanajua maana ni hatari sana kuliko wasiojua na wanajua kuwa hawajui..
 
Kwa taarifa tunazosikia ni kwamba uchumi wa Ethiopia ni kati ya uchumi ambao unakuwa kwa kasi.
Wanajenga miundinbinu safi, wamezindua train safi ya umeme na mambo kadha wa kadha.
Ila siku zote nilikuwa najiuliza, ni kwanini kila mara waethiopia wanahatarisha maisha yao, wanakubari kubebwa kwenye makontena kupita Tanzania kwenda Afrika ya Kusini na wengine wanafia njiani.
Siyo hao tu kuna wa Ethiopia walichinjwa na ISIS huko Libya wakiwa wanajaribu kufikia bahari ya Mediteranean wapate kuvuka kuingia Italy.
Katika pitapita zangu huko mtandaoni nikajiunga na group la Waethiopia, katika kuchat na mmoja ndipo akaniambia yeye kamaliza degree, ameajiriwa serikalini kama messenger.
Mshahara wake ni kama USD 50 kwa mwezi.
Nikashangaa maana kuna muda nimemtajia USD 500, akasema huo ni mshara wake wa miezi kumi.
Akaanza kunieleza kuwa serikali inajenga miundombinu, ikitaka aminisha dunia kuwa uchumi unakuwa lakini maisha ya raia wa kawaida ni magumu sana sana.
Anadai kupata kazi ni vigumu labda uwe una pesa ya kuhonga au unamjua mtu mkubwa serikalini.
Akaniambia yeye ana degree ila ni messenger ila boss wake pale kazini ana diploma.
Akaniambia ya kwamba watu wengi hawana chakula hawajui watakula nini, ila watawala wanajilipa mishara mikubwa na wanaishi maisha ya kifahari.
Uhuru wa kuongea hakuna ukileta kelele kukuua hawaoni hatari.
Anadai kukiwa na mikutano ya kimataifa, omba omba na watu wanaonyesha umasikini wanaondolewa wote addis ababa mpaka mkutano utakapoisha huwezi kuona masikini na omba omba.
Nimekaa nikatafakari nikaona maendeleo na maisha bura siyo train wala fly overs tu, inabidi vyote viende sambamba na kuboresha kipato cha mwananchi wa kawaida.

Ni nchi gani ya Kiafrika au third World yoyote ile ambayo huwezi sikia stori kama hizo?
 
Mwalimu Nyerere alikua anasema sana kwamba maendeleo ni ya watu sio vitu, kwamba watu ndio wanatakiwa kuendelea. Mpaka sasa niseme tu ukweli, sijawahi kuelewa kwa kauli ile alikua anamaanisha nini!
 
Back
Top Bottom