Leo nimeona MAMBO!!: TRA mnayajua haya?

Leo nilikwenda kutuma fax kwenye secretarial offices boot (mahali pa kununua huduma za fax nk) mara akaja M-tz mwenye asil ya Asia mzee mtu mzima. Alikuwa na zile karatasi za TRA za kulipia kodi mbali mbali benki. Ile karatasi ya kijani aliyokuwa nayo pale ndiyo iloyonishangaza. Penye sehemu ya mhuri wa benki palibandikwa kikaratasi cha mraba cha rangi nyeupe yenye kuonyesha Akiba Commercial; (nadhani), kilichoendelea ni yeye kuomba itolewe p/copy. P/copy ya kwanza ilipotoka ilionyesha mistari ya mraba (margins) ya ile karatasi nyeupe. Lakini nahisi ni wateja wa mahali pale, kilichofuata ni mtoa kopi kuingia chumba cha ndani, aliporudi kopi aliyokuja nayo haikuwa na zilemargins!! na ilionekana kuwa nakala halisi!!!! Yule Mwasaia lakini alikuwa mda wote akitetemeka. Bei ya payment voucher ile ilikua Tsh 36,000/= tu. Je, ni mangapi yanafanyika kama hayo? kwani niliwahi pia kukuta ikitolewa kopi ya cheti cha kuzaliwa na sehemu nyingine nilikuta cheti cha shule....
Aiseee, hukupaswa kukaa kimya hivyo!! ilitakiwa walau utoe taarifa polisi ili huyo mu-asia na mwenye kutoa hiyo huduma ktk hiyo stationary wawekwe chini ya ulinzi, Huo ni ubadhilifu mkubwa: watanzania tunaibiwa sana. Daima tunatakiwa tuwe jasiri na tuthubutu kupambana na maovu kama hayo.
 
Ndiyo ndiyo nadhani ni duka la mhindi lile. Na mteja niliyemwona pia alikuwa ni Mwasia. wafanyakazi ni waasia na waafrika weusi. jamani ieleweke kuwa daraja la msumbiji na baadhi ya barabara zetu zimejengwa kwa kodi zetu wenyewe, pia bajeti ya mwaka huu tukiwa macho wote tutafaidi poromoko la bei za bidhaa hapa kwetu. Ndo maana tukiona tusinyamaze bali tujadili na vyombo husika vichukue hatua. Ninao mfano hai: NHC wameingia u-joint venture na WATU. Lakini wamesahau kuweka bei za upangaji bayana (kodi) katika nyumba hizo zinazotakiwa kutozwa na JV hao. matokeo yake hapa ninapoishi kuna kitu cha ajabu sana kinafanywa na JVs hawa, mpangaji anapewa bei ya kodi kwa mwezi iliyo maradufu na kisha kuambiwa ajitete, hapo bei hupunguzwa kidogo, akishalipa anapewa risiti ya bei pungufu akiuliza anapigwa chenga siku zinakwenda. Kodi yetu iko wapi? TRA atamkamataje huyu JV kama ushahidi wa kodi hauko bayana?
 
Aiseee, hukupaswa kukaa kimya hivyo!! ilitakiwa walau utoe taarifa polisi ili huyo mu-asia na mwenye kutoa hiyo huduma ktk hiyo stationary wawekwe chini ya ulinzi, Huo ni ubadhilifu mkubwa: watanzania tunaibiwa sana. Daima tunatakiwa tuwe jasiri na tuthubutu kupambana na maovu kama hayo.
Kwani hapa si ni polisi, mahakama, TRA,PCCB, NEC, na mbinguni.
 
Leo nilikwenda kutuma fax kwenye secretarial offices boot (mahali pa kununua huduma za fax nk) mara akaja M-tz mwenye asil ya Asia mzee mtu mzima. Alikuwa na zile karatasi za TRA za kulipia kodi mbali mbali benki. Ile karatasi ya kijani aliyokuwa nayo pale ndiyo iloyonishangaza. Penye sehemu ya mhuri wa benki palibandikwa kikaratasi cha mraba cha rangi nyeupe yenye kuonyesha Akiba Commercial; (nadhani), kilichoendelea ni yeye kuomba itolewe p/copy. P/copy ya kwanza ilipotoka ilionyesha mistari ya mraba (margins) ya ile karatasi nyeupe. Lakini nahisi ni wateja wa mahali pale, kilichofuata ni mtoa kopi kuingia chumba cha ndani, aliporudi kopi aliyokuja nayo haikuwa na zilemargins!! na ilionekana kuwa nakala halisi!!!! Yule Mwasaia lakini alikuwa mda wote akitetemeka. Bei ya payment voucher ile ilikua Tsh 36,000/= tu. Je, ni mangapi yanafanyika kama hayo? kwani niliwahi pia kukuta ikitolewa kopi ya cheti cha kuzaliwa na sehemu nyingine nilikuta cheti cha shule....

Tuache mawazo ya kibaguzi. Rangi ya mtu haina uhusiano na uovu. Hivi leo hao tunaowaita wahindi/waasia wakituhukumu sote kuwa ni vibaka tutawalaumu? Mbona hatusemi kibaka mmoja MWEUSI ameuawa kwa kuiba kura na WEUSI wenzake?

Ninachoshindwa kuelewa ni pale mleta mada anaposema bei ya PV ni Tsh 36,000/=. Hivi mpaka leo tunauza fomu?! Hii enzi ya mtandao! Kama ni hivyo hata mimi nigetoa kopi maana ni dhuluma na wizi kukuizia fomu ili ulipia kodi. Overheads zao zinatakiwa zilipwe kutokana na hizo kodi au watoze ushuru wa kushughulikia kodi ili tujue moja. Hamna tofauti na kudai posho kwa kufanya kazi uliyoajiriwa kufanya.

Amandla.......
 
Leo nilikwenda kutuma fax kwenye secretarial offices boot (mahali pa kununua huduma za fax nk) mara akaja M-tz mwenye asil ya Asia mzee mtu mzima. Alikuwa na zile karatasi za TRA za kulipia kodi mbali mbali benki. Ile karatasi ya kijani aliyokuwa nayo pale ndiyo iloyonishangaza. Penye sehemu ya mhuri wa benki palibandikwa kikaratasi cha mraba cha rangi nyeupe yenye kuonyesha Akiba Commercial; (nadhani), kilichoendelea ni yeye kuomba itolewe p/copy. P/copy ya kwanza ilipotoka ilionyesha mistari ya mraba (margins) ya ile karatasi nyeupe. Lakini nahisi ni wateja wa mahali pale, kilichofuata ni mtoa kopi kuingia chumba cha ndani, aliporudi kopi aliyokuja nayo haikuwa na zilemargins!! na ilionekana kuwa nakala halisi!!!! Yule Mwasaia lakini alikuwa mda wote akitetemeka. Bei ya payment voucher ile ilikua Tsh 36,000/= tu. Je, ni mangapi yanafanyika kama hayo? kwani niliwahi pia kukuta ikitolewa kopi ya cheti cha kuzaliwa na sehemu nyingine nilikuta cheti cha shule....

Sijakuelewa ningekuwa mimi nisingeandika hii post,ulitakiwa kutoa taarifa polisi haraka sana na hata kusimama kidete mpaka polisi waje.hapo tayari tumepata hasara kama taifa, dawa ya watu kama hawa ni kuwalipua tu kila unapokutana nao.
 
Mkuu nashangaa unashangaa hii issue....
Hivi hujui kuwa Tanzania ni full usaniii from top to bottom?
Kila kitu kinakwenda kiusanii na 10%
Tena ukifata sheria au kujifanya mjanja mizigo yako itaozea bandarini, na pa kushitaki usipaone
Watu wamechoka na hawaoni uchungu na hii nchi wanaona hata kodi wanazolipa haziwasaidii wala hawajui zinapokwenda, Its very sad but that is the reality
 
Bei ya PV nilikuwa na maana kuwa mlipa kodi huyu alitakiwa kupeleka benki Ths. 36,000 tu. Hivyo basi utaona kuwa pesa yenyewe ni ndogo mno kwa mtu kuiibia serikali. Kuhusu rangi si ubaguzi hata kidogo, ukienda pale hospitali ya Muhimbili kadi yako lazima iandikwe kabila lako. Dhumuni huwa ni kujua takwimu ya gonjwa fulani kwa watu wa sehemu moja- kabila, au mkoa na tahadhali kuchukuliwa. Tunapotaja rangi WEUSI/WAASIA tunataka kujua gonjwa hili linabebwa na watu gani na nini cha kufanya kulitokomeza.

Ushauri: usikimbilie kutoa hoja kama hujasoma na kuelewa vizuri walichoandika wenzio. Tabia hii mara nyingi ni matokeo ya kupiga chabo hata darasani kwenye mitihani.
 
Mkuu! Mambo ya kupga chabo yametoka wapi? Bei ni tofauti na thamani. Wewe umesema bei ya PV ambayo ina maana kiasi kinachotakiwa kununua PV. Ungesema THAMANI ya PV, tungeelewa kuwa kilichoandikwa kwenye PV kilikuwa na thamani ya 36,000. Sasa wewe msomi, unaetuambia kuwa kuna mchezo mchafu ulikuwa ukiendelea ulipomkuta mtu akitoa nakala ya PV, hebu tuambie huo mchezo mchafu ungefanyika vipi wakati nakala ya PV iliyopo TRA haijabadilishwa? Huyu, ambae wewe msomi, unataka kutuaminisha kuwa alikuwa anataka kufoji alichotakiwa kulipia benki, angewezaje kudai malipo pungufu atakayoyafanya ( unavyotaka tukuamini) ni sawa na yale ambayo TRA walimwelekeza kulipa?

Pamoja na kujaribu kujitetea, kuingiza kwako kwa neno muasia ulifanya kwa msingi wa kibaguzi ili kujenga hoja kuwa hawa wa-asia ni watu waovu, wanaohujumu nchi yetu. Kutokana na mfano wako wa Muhimbili, basi ingetakiwa vibaka wote wakipatikana watajwe kabila lao ili tujue nchini kwetu ni kabila gani lina ugonjwa huo wa ukibaka kama unavyotaka tujue kuhusu ugonjwa wa kutolipa kodi.

Amandla..........
 
Danniair,

Nimesoma tena ulichoandika na nimeelewa kuwa unachodai ni kuwa kilichokuwa kikifanyika ni mtu kutaka kujifanya amelipa Sh. 36,000 ACB wakati hakufanya hivyo. Ingawa bado nina matatizo na hoja yako lakini naungana na wengine kwa kusema kuwa na wewe unabeba lawama kwa ukimya wako.

Hoja yangu kuhusu ubaguzi bado iko pale pale.

Amandla.......
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom