MWISHO
Juzi kati nikamtext hakunijibu nkajifafiji kwa kuwa nimemtext kwa simu ndogo kuna muda huwa kanajaaa sms ,zikijaa ukijafuta sms za saa 2 zinafika saa 7 huko. Lakini wapi binti yule hakunijibu bwana weeee.
Jamaa yangu ambae nimemtaja huko juu kaacha chuo baada ya kuona mambo ni magumu na anamitikasi yakumuingizia pesa home, jana akanitafuta katika kuchati nikamtania kwa kumuita baba Manka akacheka kuwa mbona huyo ni wako nimekuachia ,nikamiambia yote akasema kama hajibu sms kawaida kwa wadada , akaanza nae kunipa wosia.
1.Mdada kama yule kwanza anafatwa na wengi alafu hataki kuonekana ni mrahici mtamuona malaya, nikasema may be hio ni sababu.
2.Akanambia yeye alifeli baada ya kujikuta star, kwamba hataki kugharamia kama kumcheki cheki kila mara Manka na vitu vingine, nkamuuliza kama kala tayari akanambia hapana, nikafurahk


.
3.Nijaribu kumtoaa hata out au nimualike hata dinner or nimpelekee hata vi chocolate wadada wanapenda sana na sio kumuambia habari za kwenda kucheki mpira sijui

4.Akanambja kuwa na akili usioteze sana muda wako kwake. Mazungumzo yakaisha jamaa akaenda mpirani.
Nikachakata chakatua kama ngoma ya Kiba, kusema nimtoe out kiukweli kifedha muda huu boom bado nashindia mlo mmoja kwa siku nikaona nitafeli nikijiingiza kwenye gharama zisizo na lazima na kuna kipindi nilimchana huyu Manka ,mie nakupenda ila hela sina nahic hapa napo nilijishushia pointi kabisa kwa mtoto yule wa kishua, nikaona may be nifanye last attempt Leo nione atarespond vipi kwa kumtext hizo outing hapana labda apelekewe chocolate tu.
Leo tulikuwa na test, nime delay kwenda nikafika formation zishapangwa watu na watu wao wa kuponea, ile naingiaa paaap class namuona binti kakaaa nyuma kuliaa akaniangalia nkamuangalia then tukapotezeana ikabidi nikakae mbele kabisa. Paper imekuja simple nikapiga chaap nikakusanya.
Nimeenda room nkaona nijifanye kama naulizia hali yake ya kukohoa maana hata jamaa tajwa hapo juu alinambia ni mgonjwa kifua huwa kinamzingua, nikatext mambo Manka, vp unaendeleaje na kikohoz. Sikupokea reply kwenye namba yake ikaja badaee namba ngeni ikanijibu poa vp, nikamuuliza we ni manka ndo hadi saiv sijajibiwa lolote.
Kiufupi haka ka binti ka model nimekapenda aisee kapo simple sana kana mapigo mazuri kanajua kutupiaa lakini kanisumbua sana nimejaribu kujiweka karibu naye lakini wapii imeshindikana.
Nimempa siku 2 awe amejibu sms asipojibu ntajua hapa sitakiwi tena na nina lazimisha mambo ,hapo nafuta namba na chatings zote I hope sitomkumbuka.
Naombeni mniombee katika hili wana JF.
Wale mnaoulizia kuhusu umri wangu nakaribia 25 soon na wale mtao comment kuhusu kusoma ,kusoma nasoma sana lakini haya mambo mengine yanakuja automatically.
View attachment 1807513