Leo nimemvulia pendo rasmi Manka

Leo nimemvulia pendo rasmi Manka

Nawasalimu kwa jina la JamiiForum.

Miezi takribani mitatu kama sio miwili kuna dada nlitokea kumpenda, ni dada wa kichaga ambaye nilibahatika kukaa nyuma yake wakati tukifanya jaribio. Kufahamiana na huyu dada kulikuja wakati mie nikiwa nimeingia kwenye hall ya mtihani na kwakuwa niliingia late basi nikakaa nyuma na ndio nilikuwa mtu wa mwisho. Nilifika moja kwa moja nikampa hi huyo dada kwa kumshika bega na kumuambia ntaangalizia kwako usifiche majibu kama unavojua kwenye chumba Cha paper lolote linaweza tokea mambo yakiwa magumu lazima ujue majirani mnasaidianaje, ilikuwa ni salamu tu na wala sio kama nilivomuambia.
Ikumbuke niliingia kwa mlango wa nyuma, kwahiyo sikuweza kumjuaa anasura gani, kupitiaa kumjulia hiyo hali akaweza geuka ndipo nlipoona uzuri wa yule binti.

Uzuri wa sura yake ni mithili ya kina Jokate Mwegelo, na alikuwa na bonge la tabasamu ,kichwani kaweka nywele za gharama na vidole vya mikono virefu na laini kwa kuvitazama(vidole virefu ndo ugonjwa wangu kwa mdada).
Tuligawiwa paper, lilikuwa ni multiple choices, nikapiga chap ,karatasi la kusaini likaja nikaweza kuona na jina lake kwakuwa ye allikuwa mbele yangu na mie ndo full back Kama Yondani. Nikaenda kusanya paper langu huku nikiwa na shauku ya kutaka kujuana nae awe hata rafiki yangu tu kama Christian Bella alivoimba.

Nikaanza kuisaka namba yake kupitia majamaa zangu ambao niko nao programme tofauti, mwishowe nikaipata namba, nikaja kumtext na kujitambulisha , sikumbuki alijibu nini ila hakuwa na response nzuri kihivyo akidai kuwa hanikumbuki vizuri.

Nikamfungukia mtoto wa kichaga huku nikiamini, bora nitupie karata yangu mapema nione inakaaje. Mtoto akawa sio muelewa yani, sms anadelay kujibu, convo ya kawaida tu salamu mnaweza chati hata siku 3 haijaisha.
Basi nikamkumbuka Alikiba na song lake la kuforce mapenzi, nikaona isiwe mbaya dhahiri huyu binti hana interest na mie lakini pia nikakumbuka Bob Marley ashasema kama mwanamke ni wa thamani hutompata kirahici, ukimkatia tamaa inamaana hukuwa mtu sahihi kwake ..... .Nikajipa moyo ngoja nikomae nione inakuajee.

Katika pitapita zangu nikakutana na uzi unasema "Je ulishawahi kumlazimisha mtu abaki kwenye maisha yako, rafiki au mpenzi" nikachungulia humo nikakutana na nondo kinoma zikanijaza upepo , comments zilikuwa ziko kama hivi.
1.Mwanamme kukaa unambembeleza mwanamke huo ni unyonge.
2.Samaki baharini wako wengi kwann ukomaee na mmoja.
3.Ukiona hujibiwi sms kwa wakati ujue hupendwi hapooo nk

Hizo comments zikanijaza upepo lakini pia kulikuwa na comments kama hizi za kunifafiji.
1.Kuna mdada nimefukuzia ndani ya miaka miwili ndo amenikubalia majuzi.
2.Kabla ya kukata tamaa hakikisha umejarbu namna zote.
3.Mwanamke anaejiheshimu hawezi kukubali kiharaka asije onekana malaya.

nilivopima kwenye mizani nikaona bora nimteme.

Inaendelea wakuu ndani ya dakika kadhaa.
Mitihani mingi wanaandika namba!!
ni mtiani gani huo?
 
Tafuta saiz yako, mm pia chuo nlivyokuwa chuo saiz zilizokuwa sio zangu zilinishinda km ww hvyo hvyoo hauna pesa achanaee huyooo
sawa kaka nimekupata lakini kuna ambao hawana pesa lakini wanachuka magoma makali au ndo mwenye kisu kikali ndio anakula nyama
 
MWISHO

Juzi kati nikamtext hakunijibu nkajifafiji kwa kuwa nimemtext kwa simu ndogo kuna muda huwa kanajaaa sms ,zikijaa ukijafuta sms za saa 2 zinafika saa 7 huko. Lakini wapi binti yule hakunijibu bwana weeee.

Jamaa yangu ambae nimemtaja huko juu kaacha chuo baada ya kuona mambo ni magumu na anamitikasi yakumuingizia pesa home, jana akanitafuta katika kuchati nikamtania kwa kumuita baba Manka akacheka kuwa mbona huyo ni wako nimekuachia ,nikamiambia yote akasema kama hajibu sms kawaida kwa wadada , akaanza nae kunipa wosia.

1.Mdada kama yule kwanza anafatwa na wengi alafu hataki kuonekana ni mrahici mtamuona malaya, nikasema may be hio ni sababu.
2.Akanambia yeye alifeli baada ya kujikuta star, kwamba hataki kugharamia kama kumcheki cheki kila mara Manka na vitu vingine, nkamuuliza kama kala tayari akanambia hapana, nikafurahk.

3.Nijaribu kumtoaa hata out au nimualike hata dinner or nimpelekee hata vi chocolate wadada wanapenda sana na sio kumuambia habari za kwenda kucheki mpira sijui
4.Akanambja kuwa na akili usioteze sana muda wako kwake. Mazungumzo yakaisha jamaa akaenda mpirani.

Nikachakata chakatua kama ngoma ya Kiba, kusema nimtoe out kiukweli kifedha muda huu boom bado nashindia mlo mmoja kwa siku nikaona nitafeli nikijiingiza kwenye gharama zisizo na lazima na kuna kipindi nilimchana huyu Manka ,mie nakupenda ila hela sina nahic hapa napo nilijishushia pointi kabisa kwa mtoto yule wa kishua, nikaona may be nifanye last attempt Leo nione atarespond vipi kwa kumtext hizo outing hapana labda apelekewe chocolate tu.

Leo tulikuwa na test, nime delay kwenda nikafika formation zishapangwa watu na watu wao wa kuponea, ile naingiaa paaap class namuona binti kakaaa nyuma kuliaa akaniangalia nkamuangalia then tukapotezeana ikabidi nikakae mbele kabisa. Paper imekuja simple nikapiga chaap nikakusanya.

Nimeenda room nkaona nijifanye kama naulizia hali yake ya kukohoa maana hata jamaa tajwa hapo juu alinambia ni mgonjwa kifua huwa kinamzingua, nikatext mambo Manka, vp unaendeleaje na kikohoz. Sikupokea reply kwenye namba yake ikaja badaee namba ngeni ikanijibu poa vp, nikamuuliza we ni manka ndo hadi saiv sijajibiwa lolote.

Kiufupi haka ka binti ka model nimekapenda aisee kapo simple sana kana mapigo mazuri kanajua kutupiaa lakini kanisumbua sana nimejaribu kujiweka karibu naye lakini wapii imeshindikana.
Nimempa siku 2 awe amejibu sms asipojibu ntajua hapa sitakiwi tena na nina lazimisha mambo ,hapo nafuta namba na chatings zote I hope sitomkumbuka.

Naombeni mniombee katika hili wana JF.

Wale mnaoulizia kuhusu umri wangu nakaribia 25 soon na wale mtao comment kuhusu kusoma ,kusoma nasoma sana lakini haya mambo mengine yanakuja automatically.
View attachment 1807513
mkuu sasa swali langu ni mja tu vipi anakujua kwa sura kwani
 
sawa kaka nimekupata lakini kuna ambao hawana pesa lakini wanachuka magoma makali au ndo mwenye kisu kikali ndio anakula nyama
Komaa mwanangu ila inabidi uwe real tu kwake inawezekana mimi nlizunguka mwaka mwsho nlishinda
 
mkuu sasa swali langu ni mja tu vipi anakujua kwa sura kwani
ananijuaa sura ndio nshawahi mfata nikapiga nae story ila hayuko comfortable kwa face to face conversation ni binti fulani mwenye aibu hivi ila kwa simu mjanja.
 
daaah kaka kwa saiv ngoja nitulie kidogo nimeshajaribu lakini naona bado mambo hayasomeki nilijipa moyo hivyo hivyo kuwa labda atabadirika lakini mapuuza yamezidi. Inshort pale SIPENDWI
 
MWISHO

Juzi kati nikamtext hakunijibu nkajifafiji kwa kuwa nimemtext kwa simu ndogo kuna muda huwa kanajaaa sms ,zikijaa ukijafuta sms za saa 2 zinafika saa 7 huko. Lakini wapi binti yule hakunijibu bwana weeee.

Jamaa yangu ambae nimemtaja huko juu kaacha chuo baada ya kuona mambo ni magumu na anamitikasi yakumuingizia pesa home, jana akanitafuta katika kuchati nikamtania kwa kumuita baba Manka akacheka kuwa mbona huyo ni wako nimekuachia ,nikamiambia yote akasema kama hajibu sms kawaida kwa wadada , akaanza nae kunipa wosia.

1.Mdada kama yule kwanza anafatwa na wengi alafu hataki kuonekana ni mrahici mtamuona malaya, nikasema may be hio ni sababu.
2.Akanambia yeye alifeli baada ya kujikuta star, kwamba hataki kugharamia kama kumcheki cheki kila mara Manka na vitu vingine, nkamuuliza kama kala tayari akanambia hapana, nikafurahk.

3.Nijaribu kumtoaa hata out au nimualike hata dinner or nimpelekee hata vi chocolate wadada wanapenda sana na sio kumuambia habari za kwenda kucheki mpira sijui
4.Akanambja kuwa na akili usioteze sana muda wako kwake. Mazungumzo yakaisha jamaa akaenda mpirani.

Nikachakata chakatua kama ngoma ya Kiba, kusema nimtoe out kiukweli kifedha muda huu boom bado nashindia mlo mmoja kwa siku nikaona nitafeli nikijiingiza kwenye gharama zisizo na lazima na kuna kipindi nilimchana huyu Manka ,mie nakupenda ila hela sina nahic hapa napo nilijishushia pointi kabisa kwa mtoto yule wa kishua, nikaona may be nifanye last attempt Leo nione atarespond vipi kwa kumtext hizo outing hapana labda apelekewe chocolate tu.

Leo tulikuwa na test, nime delay kwenda nikafika formation zishapangwa watu na watu wao wa kuponea, ile naingiaa paaap class namuona binti kakaaa nyuma kuliaa akaniangalia nkamuangalia then tukapotezeana ikabidi nikakae mbele kabisa. Paper imekuja simple nikapiga chaap nikakusanya.

Nimeenda room nkaona nijifanye kama naulizia hali yake ya kukohoa maana hata jamaa tajwa hapo juu alinambia ni mgonjwa kifua huwa kinamzingua, nikatext mambo Manka, vp unaendeleaje na kikohoz. Sikupokea reply kwenye namba yake ikaja badaee namba ngeni ikanijibu poa vp, nikamuuliza we ni manka ndo hadi saiv sijajibiwa lolote.

Kiufupi haka ka binti ka model nimekapenda aisee kapo simple sana kana mapigo mazuri kanajua kutupiaa lakini kanisumbua sana nimejaribu kujiweka karibu naye lakini wapii imeshindikana.
Nimempa siku 2 awe amejibu sms asipojibu ntajua hapa sitakiwi tena na nina lazimisha mambo ,hapo nafuta namba na chatings zote I hope sitomkumbuka.

Naombeni mniombee katika hili wana JF.

Wale mnaoulizia kuhusu umri wangu nakaribia 25 soon na wale mtao comment kuhusu kusoma ,kusoma nasoma sana lakini haya mambo mengine yanakuja automatically.
View attachment 1807513
Soma umalize utafute hela dogo,mapenzi yapo tu, after all mke wako ndy kwanza yuko daraa la 5 sa hv, mwenzenu kwa ujinga kama huo kanyonga mtu huko Iringa na huwenda akatumia maisha yake yote yaliyobaki nyuma ya nondo.
 
Chuo gani hiko mnaandika majina.hahhaha....hivi vyuo inabid mama ndalichako afute kabisa. Ndo product zenyew hiz
kuna ubaya gani mko mnafanya test mkaandika maiina na reg number zenu. Kama kwenu hamkuwa mnafanya hivyo sie kwenye TEST zetu tunafanya hivo.
 
Soma umalize utafute hela dogo,mapenzi yapo tu, after all mke wako ndy kwanza yuko daraa la 5 sa hv, mwenzenu kwa ujinga kama huo kanyonga mtu huko Iringa na huwenda akatumia maisha yake yote yaliyobaki nyuma ya nondo.
Asante kaka saivi nimepiga chini rasmi, kama kuna mrejesho ntaja leta badae.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom