Usifungashe viroba vya konyagi kwenye carry-on bag kama una pombe au liquid yoyote weka kwenye sanduku....Ndio kama hapo juu,utaratibu ndio upi jamani mi natokea mwanza naenda dar na cjawahi kupanda,vp kuhusu mavazi nackia kuna baridi ndani wananwasha air condition,kwa aliyewahi panda jmn tusaidiane
Ndio raha ya JF hata sisi ambao hatujawahi kupanda 'mwewe' tunanufaika! Ingawa ushauri mwingine mmh! Za mbayuwayu..
Kwani shida iko wapi si kama basi tu? We nenda kaa waiting room, mtaitwa na kupanda kibasi chao hadi kwenye ndege. Ingia kimya kimya kaa bana mkanda usubiri kunyanyuka tu. Pale mnapocheck in utakaguliwa mara mbili kabla ya kuingia kwenye waiting room. Kama una mzigo mkubwa ukisha ukabidhi na kuupima wakakupa ile boarding pass ingia ukaguliwe mara mbili wala usiulize mzigo uko wapi, utakutana nao Dar kwenye mkanda unaozunguka.
Unaogopa kipupwe kwenye ndege? Wala usiogope ni cha kawa tu na ukitaka unaweza kukizima. Usijifanye mgeni sana hapo airport nenda kwa upole kama mzoefu huku ukipiga chabo (ukiangalizia wengine wanafanya nini). Wakati wa kupaa usijepiga kelele ukidhani utumbo umetoka. Kama ni jioni au usiku wala hakuna shida ila kama ni mchana ukiangalia nje hasa wakati wa kutake off unaweza kuhisi kuzunguzungu. But usijali utazoea tui, bon voyage!!!
Ndio kama hapo juu,utaratibu ndio upi jamani mi natokea mwanza naenda dar na cjawahi kupanda,vp kuhusu mavazi nackia kuna baridi ndani wananwasha air condition,kwa aliyewahi panda jmn tusaidiane
nimecheka sana !!
Napanda 540 sky nilitumiwa nauli na mjomba anakaa dar huko ana hela sana ,
Ukiwa angani, ukichoka kukaa, unaweza kufungua mlango tu, ukatoka nje kupunga upepo. Kwenye ndege raha sana..
Napanda 540 sky nilitumiwa nauli na mjomba anakaa dar huko ana hela sana ,
This has been really fun. Uzuri wa jf ukijifanya zombie utakuta waliokuzidi
Bora kuuliza mwaya!