chikakatata
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 220
- 98
kila siku nimekuwa nikifuatilia mijadala hapa jf hususan kuhusiana na mbunge wa nzega, dkt. Hamis kigwangallah, uhusiano wake na ofisi ya mke wa rais (wama) na kupewa mkopo kwa ajili ya kufanya biashara. Nimefanikisha kupata orodha ya makampuni yaloyopewa stimulus package na kukuta kampuni ya msk solution ltd ambayo inamilikiwa na dkt. Kigwangalla haimo, hivyo habari zote kuwa alipewa shavu na mama kikwete kupitia mfuko huu ni uongo. Pia nimepata taarifa kutoka kikao cha wafanyabiashara, wakulima na bodi ya pamba na waziri wa kilimo prof. Maghembe kilichokaa pale bungeni dodoma j2 iliyopita na kufuatiwa na kikao kingine leo hapa mwanza kuwa wanalalamika kwa kutopewa wenyewe na badala yake kupewa makampuni yasiyojihusisha na biashara hiyo na hivyo kumuomba rais aangalie jinsi mchakato huu ulivyoendeshwa ili kunusuru masoko ya wakulima wa zao hili nyeti kanda ya ziwa.