Charles Kimei: Serikali itoe 'special stimulus' sekta ya utalii

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Charles Stephen Kimei amewasikisha maombi matatu serikalini alipokuwa akichangia bajeti ya wizara ya mali asili na utalii bungeni ambazo ni:

1. Ameomba serikali kufikiria upya ombi la wananchi wa jimbo la Vunjo na majimbo mengine ya mkoa wa Kilimanjaro yanayoizunguka hifadhi ya Taifa Kilimanjaro (KINAPA) kuhusu matumizi ya eneo la msitu wa nusu maili kwa ajili ya shughuli za ufugaji nyuki, kupata dawa za asili, kusafisha mifereji ya asili inayoanzia msituni, kupata makanisani ya mifugo na kuni kwa wakina mama. Anaamini serikali ya awamu ya sita ni sikivu hivyo katika kuendelea kuimarisha ujirani mwema baina ya wananchi na hifadhi hii basi serikali italizingatia ombi hili.

2. Ameiomba serikali kuona namna itatoa motisha maalum 'stimulus package' kwa mawakala na makampuni ya utalii nchini ili waweze kukabiliana na athari zilizotokana na ugonjwa wa virusi vya korona ikiwemo kutoa msamaha au unafuu katika ulipaji wa malimbikizo ya tozo na kodi, pamoja na kuwaongezea muda wa marejesho ya mkopo bila kuwaongezea riba ili kuwawezesha kuwa sawa na kuendelea vizuri na biashara hii ya utalii.

3. Ameiomba serikali pamoja na kuweka utaratibu wa maslahi kwa wanaofanya kazi ya upishi, ubebaji mizigo ya wageni na waongoza watalii bado anaona ipo haja ya serikali kujipanga zaidi kwa kutoa elimu kwa makampuni yetu juu ya maslahi ya makundi haya muhimu sana kwa utalii wetu. Sheria ya hifadhi za milima hazimtambui mpagazi (porter -mbeba mizigo ya watalii) kuwa porter au mpagazi akishatoka nje ya hifadhi hizi sasa sheria ya aina hii zinachochea kundi hili kutolipwa stahiki zake kama inavyostahili.

VUNJO KAZI INAENDELEA. PAMOJA TUNAWEZA

2697575_IMG-20210208-WA0044.jpg
#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom