Leo namsafisha Kigwangallah: Kampuni yake haikupata Stimulus Package!

chikakatata

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
220
98
List of Companies.jpg List of companies 2.jpg
kila siku nimekuwa nikifuatilia mijadala hapa jf hususan kuhusiana na mbunge wa nzega, dkt. Hamis kigwangallah, uhusiano wake na ofisi ya mke wa rais (wama) na kupewa mkopo kwa ajili ya kufanya biashara. Nimefanikisha kupata orodha ya makampuni yaloyopewa stimulus package na kukuta kampuni ya msk solution ltd ambayo inamilikiwa na dkt. Kigwangalla haimo, hivyo habari zote kuwa alipewa shavu na mama kikwete kupitia mfuko huu ni uongo. Pia nimepata taarifa kutoka kikao cha wafanyabiashara, wakulima na bodi ya pamba na waziri wa kilimo prof. Maghembe kilichokaa pale bungeni dodoma j2 iliyopita na kufuatiwa na kikao kingine leo hapa mwanza kuwa wanalalamika kwa kutopewa wenyewe na badala yake kupewa makampuni yasiyojihusisha na biashara hiyo na hivyo kumuomba rais aangalie jinsi mchakato huu ulivyoendeshwa ili kunusuru masoko ya wakulima wa zao hili nyeti kanda ya ziwa.
 
Mbona wamsemea yeye yupo hapa hata hivyo hiyo ni pepar ambayo inaweza kuwa tayari edited so wacha mchezo na mafisadi.
 
View attachment 52884View attachment 52885
kila siku nimekuwa nikifuatilia mijadala hapa jf hususan kuhusiana na mbunge wa nzega, dkt. Hamis kigwangallah, uhusiano wake na ofisi ya mke wa rais (wama) na kupewa mkopo kwa ajili ya kufanya biashara. Nimefanikisha kupata orodha ya makampuni yaloyopewa stimulus package na kukuta kampuni ya msk solution ltd ambayo inamilikiwa na dkt. Kigwangalla haimo, hivyo habari zote kuwa alipewa shavu na mama kikwete kupitia mfuko huu ni uongo. Pia nimepata taarifa kutoka kikao cha wafanyabiashara, wakulima na bodi ya pamba na waziri wa kilimo prof. Maghembe kilichokaa pale bungeni dodoma j2 iliyopita na kufuatiwa na kikao kingine leo hapa mwanza kuwa wanalalamika kwa kutopewa wenyewe na badala yake kupewa makampuni yasiyojihusisha na biashara hiyo na hivyo kumuomba rais aangalie jinsi mchakato huu ulivyoendeshwa ili kunusuru masoko ya wakulima wa zao hili nyeti kanda ya ziwa.

Usichezee akili za watu. Kule kwenye jukwa la Wanabidii, Kigwangala mwenyewe alikwishakiri kuwa alipata fedha la Stimulus Package lakini akaijitetea kuwa kampuni yake ilistahili kupata, leo na wewe sijui umetokea wapi, unatuletea porojo. Wewe ni kuwadi? Kwa nini asijitetee mwenyewe?
 
maandalizi ya uwaziri haya!kila la kheri Dr hamis nakutakia utafunaji mwema wa nchi.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Haya nayo mambo. Kwamba mtu anasimama na kusema namsafisha fulani. Ama kweli hata mimi nitasimama na kusema namsafisha mkulo na mawaziri wenzake.
 
Huyu mheshimiwa nilisoma naye na alikuwa mpiganaji toka shuleni. Amekuwa ni mtu wa kujituma yeye mwenyewe binafsi. Hata kabla ya kuwa mheshimiwa alikuwa ni mtu wa kujitoa sana kwa wana nzega katika shughuli mbalimbali.
 
Usichezee akili za watu. Kule kwenye jukwa la Wanabidii, Kigwangala mwenyewe alikwishakiri kuwa alipata fedha la Stimulus Package lakini akaijitetea kuwa kampuni yake ilistahili kupata, leo na wewe sijui umetokea wapi, unatuletea porojo. Wewe ni kuwadi? Kwa nini asijitetee mwenyewe?
acha uongo, hata mimi niko wanabidii na sijawahi kuona kama alishawahi kusema alipewa. acheni chuki binafsi
 
Haya nayo mambo. Kwamba mtu anasimama na kusema namsafisha fulani. Ama kweli hata mimi nitasimama na kusema namsafisha mkulo na mawaziri wenzake.
kama una data njoo 4wd na umsafishe yeyote yule umtakaye kwani umeshikwa mkono?
 
ahadhali wadau leo wameuweka wazi ukweli kuhusu stmulus package maana Mh Kigwangallah amekuwa akihangaika sana kujitetea hapa lakini haeleweki bora leo wameleta ushahidi tumeuona
 
Ati 'leo namsafisha HK'

Msafishe tu!!
hako ka-attachment kenyewe hata hakaonekani!!
 
ahadhali wadau leo wameuweka wazi ukweli kuhusu stmulus package maana Mh Kigwangallah amekuwa akihangaika sana kujitetea hapa lakini haeleweki bora leo wameleta ushahidi tumeuona

Who is you by the way!!
Unasafisha watu kwa kibali cha nani, Hosea?, Utouh?
 
Ati 'leo namsafisha HK'

Msafishe tu!!
hako ka-attachment kenyewe hata hakaonekani!!
mbona sisi tumesoma? jaribu kuka-click katakuwa kakubwa utaona kama kampuni ya MSK Solution (ambayo ndiyo ya Mh Kigwangallah) imo au haimo
 
acha uongo, hata mimi niko wanabidii na sijawahi kuona kama alishawahi kusema alipewa. acheni chuki binafsi

Hakuna chuki binafsi hapa. Lazima tuwaambie ukweli hata kama unauma na hampendi.

Kampuni ya Kigwangalla MSK Solutions Ltd ilinufaika na fedha za stimulus package kimagumashi. Haikuwa na vigezo vya kuifanya ipate fungu lakini ilipitishiwa dirishani na kuingizwa kwenye list ya watakaonufaika na hatimaye walichota mamilioni ya shilingi.

Kama hiyo haitoshi wakanunua pamba kwa bei ya chini sana hivyo kuzidi kuwaumiza wakulima wa pamba.

Sijui mtamsafisha na sabuni gani ili atakate. Kifupi ni kwamba katika hili wala hasafishiki!
 
Na nimeamini kwa kuwa huyu jamaa ameshalamba pesa hizi hawezi hata siku mwoja kumfunga paka kengele!!

Tunashukuru mleta mada kwa kuanika hii list hapa!!
 
Haya yote yanasababishwa na njaa, sisi wanaJF tunaendelea kulumbana wenzetu wanakula nchi. Kifupi tu ni asilimia kubwa ya watu waliofanikiwa kimaisha ni wale ambao mishe zao sio za halali, wana mkono wa polisi, TRA, wanasiasa wakubwa nk. Na ukichunguza sana jinsi haya makampuni yanavyopata tenda utaelewa nini nazungumzia hapa.

Sisi na njaa zetu tunabaki kulalama bila msaada, hatutafika mbali tukiendelea kulalamika badala na sisi tutafute kwa mbinu hizi hizi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom