Mimi kuna mmoja aliniliza laki sita taslimu..... alinipigia simu akinitaja jina langu ,ananikumbsha vile tumesoma wote DIT, akawa ananisifia kwa kufungua kampuni yngu ya ukandarasi...... akawa amesema anafanya kazi sehemu akanitaarifu kuwa wana miradi takribani 14 hivo natakiwa kununua tender document, kila moja laki moja.... akanisihi ninunue docs 6 maana yeye ana uwezo wa kuzipitisha na hatimaye nkapata kazi..... na submission akadai ni jumatano ili hali siku hiyo ilikua ni ijumaa, so ikabidi chap chap niingie nmb mobile, fasta nkamtumia baada ya kuwa nimejiridhisha na michoro ya kazi zenyewe pamoja na documents nyingine kuhusu mradi.......... nilivomaliza kutuma hela kilichofuata ni mimi na mungu wangu ndo tunajua.... teh teh teh