Leo matapeli wa simu wamechachamaa

MJUKUU WANGU HONGELA KWA KUONA MAFANIKIO KAMA NILIVYOKWAMBIA KUWA MAFANIKIO YA NDAGU YANGU HAICHUKUWI MDA MLEFU NASHUKULU NYOTA YAKO HAIJASUMBUA NDIO MANA NAKWAMBIA NDAGU NILIO KUKABIZI NI NZULI KILICHO BAKI NIKUPATIE ZINDIKO MVUTO WA BIASHALA NA NIWEZE KUKUVALISHA HII PETE YA BAHATI YANI HII NI YA KUVUTA MALI
 
Leo kweli wameamua mwingine huyu......

Your mobile number has been Awarded 960,000 Euros in the 2017 Toyota Xmas Award Grants. To receive, contact Dr. Marcus via email: toyotaxmasgrants@gmail.com


nilichomjibu siri yangu.
f6e72c542cd90edd02f8a2d626fba218.jpg
 
Mwingine huyu anayetumia namba hii, anadai yeye ni customer care wa tigo
‭0659 071 000‬
 
Nyingine nimepata usiku toka namba : 0753501913
super feo nasikitika sana nimekupa ndagu na umefuata masheriti na ukawa tajili mkubwa na unaniheshimu babu yako ukumbuke wewe na mwenzako mwendamseke pamoja na manyanya niliwasaidia bure na baada ya kufanikiwa muli kuja kunishukuru tena nimewapa kitu ambacho siyo cha kumwaga damu lakini mwenzako wa mwanza nimemusaidia akiwa mbali simufahamu anifahamu ila kwa heshima yako nimemusaidiya amefanikiwa hatak kuja kushukuru ananitumia pesa tu mwambie asione


SWALI HIVI HAWA WATU KWELI UWA WANAPATA WAJINGA WA KUTAPELI?
 
Mimi kuna mmoja aliniliza laki sita taslimu..... alinipigia simu akinitaja jina langu ,ananikumbsha vile tumesoma wote DIT, akawa ananisifia kwa kufungua kampuni yngu ya ukandarasi...... akawa amesema anafanya kazi sehemu akanitaarifu kuwa wana miradi takribani 14 hivo natakiwa kununua tender document, kila moja laki moja.... akanisihi ninunue docs 6 maana yeye ana uwezo wa kuzipitisha na hatimaye nkapata kazi..... na submission akadai ni jumatano ili hali siku hiyo ilikua ni ijumaa, so ikabidi chap chap niingie nmb mobile, fasta nkamtumia baada ya kuwa nimejiridhisha na michoro ya kazi zenyewe pamoja na documents nyingine kuhusu mradi.......... nilivomaliza kutuma hela kilichofuata ni mimi na mungu wangu ndo tunajua.... teh teh teh
 
Me Kuna taperi moja la kike limenilazimisha kuwa eti kwenye zebra alama ya wavuka kwa miguu eti sijasubiri wamalize hatua ya mwisho kuvuka ati nimeondosha gari tumebisha sana hadi akanipa kosa lingine la abiria hajafunga mkanda nayo nimeshangazwa mimi nihusike kwa lipi. Mwisho wa mwaka mataperi yanatafuta pesa kinguvu. Elfu 30 zangu zimechukuliwa bila jasho lao kutoa..walaaniwe sana
 
Kuna mpumbavu mmoja anatumia namba 0789133055 amenipigia leo asubuhi alichobugi aliniambia anafanya kazi UNICEF. Nikamuuliza Unicef ndo mji gani akasema ni kampuni ya kulea watot yatima. Hapo nikajua kabisa huyu ni tapeli coz UNICEF naijua na shughuli zake nazijua vizuri sana. Alichonichosha ni kuniambia kuwa unicef inanunua mahindi so inabidi niwe suplier wa madawa ya kuua dumuzi. So madawa yenyewe aliyonielekeza yako kwenye liquid form. Nikajiuliza tangu lini dawa ya kutreat mahindi makavu iwe kwenye liquid form? Halafu watu wa chakula huwa ni FAO na UNHCR. Kilichofuata nilimshauri kuwa kama fursa hapa Tz zimeisha ni bora aende Mombasa akauze al dubri aka T.I.G.O.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom