Leo katika|#SimuliziZa116|

Leo katika|#SimuliziZa116|

Sema Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2016
Posts
251
Reaction score
466
Mnamo tarehe 10 mwezi januari 2019, Namba 116 ilipokea simu kutoka kwa jirani akiarifu kuhusu mtoto wa miaka 12 aitwae Olivia. Olivia alihitimu darasa la saba mwaka 2018, matokeo yalipotoka alikidhi vigezo vya kujiunga elimu ya sekondari, hata hivyo wazazi wake waliamua kumuozesha kwa mwanaume mtu mzima badala ya kumuendeleza kielimu. Huduma ya simu kwa mtoto ilitoa taarifa kwa Afisa Ustawi wa jamii, kwa msaada wa jirani mtuhumiwa alikamatwa na mtoto kutolewa kwenye ndoa na kuandikishwa shule. Huduma ya simu kwa mtoto ilifuatilia suala hili kwa mkuu wa shule na alithibitisha kuwa Olivia ameanza shule na anahudhuria vipindi.
 
Back
Top Bottom