Leo imetimia miaka 100 baada ya kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia.

kibol

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
4,514
2,730
Tar 11 Nov 1918 ndio ilikuwa mwisho wa kadhia hii iliyoondoka na mamia kwa maelfu ya roho za walimwengu wa dunia hii ikiwemo na wa Tanganyika wenzetu waliopigana upande wa mkoloni wao, muhimu ni kuwakumbuka na kuwaombea roho zao huko waliko.
 
The world has never been the same ever since...thanks to Adolph Hitler...konki master wa kizungu.
Kila mmoja ana namna yake ya kuacha legacy huku duniani, historia ya mtu huandikwa na yeye mwenyewe, wengine huja kuinakili tu.
 
Uzalendo unapopitiliza huzaa chembechembe za uchoyo,unaosababisha uroho na hatimaye maumivu..nachofurahia ni kuwa wazungu hawaitaki kabisa hii mbegu kustawi kwao.
 
Siku zote ubinafsi, umimi haujawahi kumuacha mtu salama, muhimu ni kujifunza kutokana na madhila haya ili kuepukana na majanga kama haya siku za usoni, and there comes umuhimu wa kujifunza historia.
 
Vita duniani zimekuwa zikiwepo tangu zamani na
bado zipo mpaka sasa. Tofauti ni kwamba hii
inaitwa kuu. Tuzidi kumuomba Mungu Dunia iwe
maali pa amani.Tuziombee nchi zenye vita na
watu wanao na walio athirika na vita. Maana vita
si nzuri madhara yake tunayaona na yanaathiri
vizazi na vizazi.
 
Akili za kushikiwa ni shida sana, wewe unaamini kwamba dunia haikuwahi kupigana vita kabla ya hio? Na inakuwaje ya dunia wakati ilikuwa vita baina ya makabila ya kizungu?
 
Vita zilikuwepo nyingi kabla ya hii na baadae zimeendelea kuwepo na bado zitaendelea kuwepo ata baada ya sisi kupita, swali ulilotakiwa kujiuliza hapa ni kwa nini hii iliitwa vita kuu ya kwanza ya dunia? Usipoandika historia yako mwenyewe wengine watakuandikia.
 
Ina maana kizazi chetu ndio kinaisha bila hata kuona ka vita kamoja ka Dunia? Not fair.
 
Vita duniani zimekuwa zikiwepo tangu zamani na
bado zipo mpaka sasa. Tofauti ni kwamba hii
inaitwa kuu. Tuzidi kumuomba Mungu Dunia iwe
maali pa amani.Tuziombee nchi zenye vita na
watu wanao na walio athirika na vita. Maana vita
si nzuri madhara yake tunayaona na yanaathiri
vizazi na vizazi.
Haya yanafanyika ili kutukumbusha tulipotoka, vita yoyote ile inaacha makovu yasiyofutika kwenye jamii husika, tuendelee kupinga kwa nguvu matumizi yoyote yale ya nguvu miongoni mwa jamii za ulimwengu huu, tuzidi kumuomba Mungu dunia yake hii iendelee kuwa sehemu salama zaidi ya kuishi kuliko huko tulikotoka.
 
Ina maana kizazi chetu ndio kinaisha bila hata kuona ka vita kamoja ka Dunia? Not fair.
Hujawahi kuona madhara ya vita ndio maana hujui unachokiomba, nenda ata hapo Rwanda tu ukajionee madhara ya vita ile ya kimbari, mtu kapoteza familia yake nzima, wengine wamepata ulemavu wa kudumu nk nk, tusiombe vita kabisa.
 
Fighting iko kwenye plan ya Mungu ndio sababu hata Israel Bado wanapigana hadi leo.
 
Tar 11 Nov 1918 ndio ilikuwa mwisho wa kadhia hii iliyoondoka na mamia kwa maelfu ya roho za walimwengu wa dunia hii ikiwemo na wa Tanganyika wenzetu waliopigana upande wa mkoloni wao, muhimu ni kuwakumbuka na kuwaombea roho zao huko waliko.
Tumekaririshwa kuwa hiyo ni vita vya dunia lakini kiukweli ni vita vya mataifa ya Ulaya. Sisi tuliingizwa tu kupigania ushindi wa wakoloni waliotutawala, aidha upande wa wajerumani au waingereza.
 
Upo sahihi kabisa, ni vita vya mataifa ya ulaya vilivyokuwa na lengo la kugombea makoloni mbali mbali hasa huku Africa, nafikiri mapinduzi ya viwanda huko ulaya kipindi hicho yaliyopelekea uhitaji wa maeneo mapya ya uwekezaji, malighafi, masoko, vibarua wa bei nafuu nk ndio kichocheo kikubwa cha vita hii.
 
Fighting iko kwenye plan ya Mungu ndio sababu hata Israel Bado wanapigana hadi leo.
Naona umeamua kutumia Bible ili kupotosha intentionally, gharama ya vita inaenda kizazi hadi kizazi, unajua kwa nini Israel na hao Palestinians wanapigana mpaka leo? Ni kwasababu walishapigana huko nyuma, wazungu wanamsemo mmoja wanasema ""war begets war""" vita huleta vita.
 
Wapo wengi tu mkuu
Am not sure, pengine kama wapo basi watakuwa wazee sana, kama vita iliisha mtu akiwa kwenye mid 20 plus hii miaka 100 iliyopita tangu vita yenyewe iishe huoni ni miaka mingi sana kulingana na life expectancy ya mwanadamu inafahamika mkuu.
 
Back
Top Bottom