hali mbaya sana ndugu zanguni. bbc wametoa ramani ikionesha nchi za afrika zinazokubali ndoa za jinsia moja, na nchi zisizo kubali ndiyo hizo. idadi inakaribia kuwa sawa! inasikitisha sana! nchi za kiarabu kaskazini mwa afrika ndoa hizo haziruhusiwi na hukumu ni kifo au kifungo cha maisha. sielewi kwa nini zimewekewa kijivu hafifu (light grey) na siyo nyekundu! sidhani ushoga ndiyo jambo kuu lililomleta Obama. ameletwa kwa sababu za kiuchumi na kisiasa. naamini hata hilo la ushoga ataligusia kama alivyofanya Senegal. katika rasimu ya katiba, tumecopy na kupaste haki za binadamu zote. itabidi iainishwe vizuri kuwa ndoa za jinsia moja ni kifungo cha maisha. la sivyo tutakuja sumbuliwa kwa kisingizio kuwa ni haki ya mtu kuolewa au kuoa yeyote amtakae. jambo la pili, haki za binadamu zinataja haki ya mtu kuishi. lkn zinakosea kuhusu mtu anae mnyima mwenzake haki ya kuishi (anaeua) afanyweje? kwa maoni yangu, kama kaua makusudi, na yeye auawe. TUWE MAKINI NA NENO HAKAI ZA BINADAMU. wazungu wanachezea akili zetu