Lengo la vita ni nini?

Lengo la vita ni nini?

Adui wa Adui yangu ndie rafiki yangu na rafiki wa adui yangu ndie atakua adui yangu pia. Vita husambaa kwa style hiyo, chanzo ni utawala, dhuruma, biashara, ubinafsi, tamaa ya kukalia madaraka, katiba mbovu, wananchi kuichoka serikali yao icyojali wananchi husika, rushwa , ufisadi, udini ,ukabila, mapenzi( ushauri kutoka kwa 1st lady), uasi wa kijeshi, kuhakiki utendaji kazi wa zana za kivita n.k
 
Lengo la vita inategemea na sababu yenyewe iliyopelekea kwa mfano wengine wanapigana vita kugombea ardhi, sasa kila mmoja anajiona anahaki kuliko mwingine

Pia kuna vita kama ile ya Iraq na U.S ilitokea kwasababu U.S akidai Sadam ni dikteta sasa kama anawaokoa raia wa Iraq

Kimsingi vita huwa lengo kuu ni kuweka usawa au namna ambayo inaonekana ndio sahihi kwa nguvu

Kwa mfano vita zinazohusiana na dini, wale watu amabao watakua hawaamini na kupinga kwa vitendo basi watapigana na hao wenye dini yao either kwa kujilinda au kuwakomesha
 
Vita ni biashara, mimi natengeneza zana za kivita aina fulani, na wewe unatengeneza aina fulani, tunatengeneza mgogoro sehemu fulani mfano DRC tunauza silaha.
Hivi umadhani sehemu kama Congo, pale luna silaha yoyotw ya maana inatumika,ile vita ni vile vifaa vilivyokuwa outdated ndio vinatupwa pale,ndio maana inakuwa ya kuviziana.Hamna technology yoyote ya maana pale,iko kienyeji mno,ukianza na Maimai mpaka kule kwa Kagame,yaani imekaa kiusanii mno.
 
Wengi wanaokufa kwenye vita ni wanaume kwa hiyo lengo la vita ni kuweka idadi ya wanaume in check, maana wanaume wakiwa wengi kuliko wanawake ni hatari, ni bora wanawake wawe wengi kuliko wanaume
Dah! Ecosystem nini mkuu!!
 
Isambe kama umeifuatilia kwa kina vita ya Congo DRC inatengenezwa, pale inapokaribia kuisha lazima itokee incidence ya kutengenezwa. Kwa mfano mwaka jana Kabila alipoona anatakiwa aachie ngazi akaanzisha utaratibu wa sensa, na kwakua wananchi walikua wakipinga suala layy kuendelea kukaa madarakani ,ikabidi vikundi vya waasi viwe financed na impowered na watu kutoka ktk serikali ya Kabila(North Kivu - Kamanda wa Kombania aliasi na akaingia na kikundi + vifaa msituni na inasemekana alienda kuongeza nguvu kwa ADF NALU).. Hiyo ni sehemu ya usanii unaochezwa ili kuofanya vita iwepo, na ukiichimbs kwa ungpdani unakuta kuna mkono wa France na Belgium ktk vita ile, na chanzo kikubwa ni utajiri wa madini na mazao ya misitu yanayopatikana Congo DRC..
 
kwa sasa hivi vita hutokea kwa sababu yingi kama vile
1. pale maelewano yanashindwa kufikiwa kwa reason
2. kwa ajili ya tamaa ya kupata mali na nguvu ya kitawala, mfano huku Africa vita nyingi husababishwa na tamaa kuwa na nguvu ya kiutawala kati ya makundi yenye nguvu, na frustration za wale wanaokandamizwa
Hoja yako ya kwanza inathibitisha kuwa vita ni matokeo ya udhaifu wa wanadamu katika kutatua migogoro yao.
Hoja yako ya pili inathibitisha kuwa lengo la vita ni kupata haki iliyominywa na wachache kwa hiyo vita ni faida.
 
Ubinafsi na ufahari

Maana vita huanzishwa ili kupata "kitu" kwa kimdhuru mwingine(ama kumtokomeza kabisa), na baada ya vita kuna ushindi, alieshinda hujisikia fahari sana, kwamba yeye ni zaidi ya mwingine.
Sawa mkuu, kumbe na kuuana kote jambo la msingi ni ufahari tu,
 
Hoja yako ya kwanza inathibitisha kuwa vita ni matokeo ya udhaifu wa wanadamu katika kutatua migogoro yao.
Hoja yako ya pili inathibitisha kuwa lengo la vita ni kupata haki iliyominywa na wachache kwa hiyo vita ni faida.
mkuu kuna watu kutokana na tamaa zao, ego zao au pride zao hawataki kutawaliwa na watu wa jamii nyingine
mfano kuna waasi huko DRC, Nigeria, South Sudan n.k ukicheki sababu za kupigana kwao ni upumbavu wa pande zote mbili, vita inaweza kuwa na faida au hasara kutokana na yale matokeo yake, sio kila vita ina faida
 
vita ni hatua ya mwisho ya kudai haki..
au kurudisha heshima iliyokejeliwa..
wakati mwengine kutuliza wenge la anaejifanya mbabe na kutaka kudhibiti wengine kumbe badala ya nguvu ana povu..
hivyo mnamfuta povu abaki na upepo..
 
Hivi umadhani sehemu kama Congo, pale luna silaha yoyotw ya maana inatumika,ile vita ni vile vifaa vilivyokuwa outdated ndio vinatupwa pale,ndio maana inakuwa ya kuviziana.Hamna technology yoyote ya maana pale,iko kienyeji mno,ukianza na Maimai mpaka kule kwa Kagame,yaani imekaa kiusanii mno.
Vita ni vita tu mkuu, na silaha hizo zinanunuliwa, mfano RPG, LMG, AK47, SMG, Artillery motors, n.k, japo sio modernised lakini waasi wanazimiliki hivyo kuwapokonya kizembe siyo rahisi lazima vita vipiganwe.
 
Vita hasa ni kutaka kutawala, hapo zamani kulikuwa hakuna vitendea kazi kwahiyo jamii moja iliitawala jamii nyingine na kuwatumikisha. Walihitaji kupigana vita na kushinda lengo likiwa hilo. Hata leo hii jamii fulani ikijiona inaonewa mazungumzo yakishindikana wanapigana. Kisiasa ni lengo lilelile wanaotawala wanajitahidi kuwakandamiza watawaliwa mpk hapo jamii kandamizwa ikiamka na kupata nguvu inaingia kupigana na inakuwa vita. Na lazima awepo kiongozi naishia hapo kwanza....
 
Isambe kama umeifuatilia kwa kina vita ya Congo DRC inatengenezwa, pale inapokaribia kuisha lazima itokee incidence ya kutengenezwa. Kwa mfano mwaka jana Kabila alipoona anatakiwa aachie ngazi akaanzisha utaratibu wa sensa, na kwakua wananchi walikua wakipinga suala layy kuendelea kukaa madarakani ,ikabidi vikundi vya waasi viwe financed na impowered na watu kutoka ktk serikali ya Kabila(North Kivu - Kamanda wa Kombania aliasi na akaingia na kikundi + vifaa msituni na inasemekana alienda kuongeza nguvu kwa ADF NALU).. Hiyo ni sehemu ya usanii unaochezwa ili kuofanya vita iwepo, na ukiichimbs kwa ungpdani unakuta kuna mkono wa France na Belgium ktk vita ile, na chanzo kikubwa ni utajiri wa madini na mazao ya misitu yanayopatikana Congo DRC..
Kuna kaukweli fulani maana haiwezekani serikali ya Congo drc ikashindwa kuwaangamiza hao waasi mara moja tu, hapo UN wanalipa maelfu ya maasikari wapatao 50,000+ kutoka nchi kibao duniani, kwa hiyo hiyo kitu ni mchongo wenye mlolongo mrefu, hapo ni pa kupigia mkwanja, kuanzia kabila mwenyewe, mataifa ya magharibi, na malipo kwa UN... Lakini bila huruma watu wanakufa kwa njaa na maradhi.
 
Wanasiasa ndio huanzisha majanga ya vita, mwananchi wa kawaida hawezi kujua kuwa vita huanzishwa ili watu waneemeke na familia zao. Tatizo ni hii kinga kwa viongozi wakubwa, its shame kwakweli haya mambo yapo Africa tu.
 
Marekani kuvamia nchi mbalimbali unazungumziaje mkuu japo ya marekani vita vyake huwa vimepangwa, lakini dhana yake ni ubabe wa kijeshi
 
Turudi kwa majirani zetu, wameingia kwenye vita na Al shabab ni kwa7bu serikali ya Kenya ilikubali kuweka US military base nchini kwao, lkn je mwananchi wa kawaida anafaidika nn na hiyo US base?Serikali inafaidika kuanzia kwnye mahusiano ya kimataifa mpaka kiuchumi ila Alshabab nao pia wanawashambulia wakenya kulipa dhambi ya uasi waliofanyiana. Miaka ya nyuma waasi wa Somalia walikua wakisaidiana na askari wa Kenya(biashara ya mkaa) ktk kulipisha pesa ktk vivuko mpakani mwao.
Ukienda Congo Mzee Kabila (baba) alikua porini na Jamal Makulu(ADF Founder) na walisaidiana ktk vita mpaka Kabila baba akaingia madarakani
 
... Tehetehe hapo kwenye biashara ya mkaa umenichekesha mkuu, nikikumbuka jinsi asikari zaidi ya 100> wa Kenya walishambuliwa wakiuza mkaa wakati wa doria, vijana wa al shabaabu wakafanya a successful ambush..
 
Back
Top Bottom