Lengo la vita ni nini?

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
11,136
19,871
Wakuu habari zenu, natumai mu wazima endapo kuna walio na shida Mungu atawapeni wepesi..
Lengo kuu la uzi huu ni kama kichwa kinavyojieleza, kwa mda nimekuwa nikitafakari sana juu ya lengo hasa la wanadamu kufanya mapambano ya kivita: maswali yaliyo jitokeza ni kama, je, vita ni udhaifu wa wanadamu katika kutatua migogoro? Au vita ni toshelezo la dhamira( satisfaction of desire)? Au ni mbinu sahihi ya kupata haki? Je vita huleta amani?

Tukirejea katika maandiko matakatifu, biblia ina onyesha jinsi wana wa Israel walivyopigana vita katika taifa lao, pia Quran inaonesha jinsi vita vitakatifu vilivyopiganwa (Jihad wars) huko medina na mtume Muhammad S.A.W, je vita inaruhusa toka kwa Mungu? Je vita huleta haki?
Karbuni wanajamvi tujadili jambo hili kwa mapana ya Kisiasa, falsafa (philosophy), pia kiimani.
 
Vita ni biashara, mimi natengeneza zana za kivita aina fulani, na wewe unatengeneza aina fulani, tunatengeneza mgogoro sehemu fulani mfano DRC tunauza silaha.
Dah!! Hatari sana kama watu wanatenga eneo kuwa eneo la migogoro ili kufanya biashara za silaha za kivita.
 
Vita huanza mkubwa kutaka kumuonea mdogo. Mdogo huwa na mali na mkubwa anayo nyingi kuliko ya mdogo lakini uroho na uchoyo wa mkubwa ndio husababisha vita. Kutokana mkubwa hofu yake anaona kuna siku huyu atanifikia level yangu na anaweza kunishinda. kwahio mkubwa atatafuta kila aina ya mbinu ampige mdogo ili ajimilikishe mali yeye. Vita huanzishwa kwa tamaa ya madaraka na mali.
 
Sawa mkuu, vp lakini kuhusu vita vya kidini vimekaaje.
 
Moja ya mashambulizi ya Israel huko Gaza July 2014
264884d33782f22132d1e1809d642c38.jpg

Russia gunship Mi-24 helicopter attack in Syria
555664fa3950b392e697872ccd062404.jpg
 
Mawazo yote wazeni lakini vita sio tukio ila ni roho tena yenye nguvu na shetani ni mtumishi wa vita, sio shetani ndio mwenye vvita lahasha vita ndio vina mtumia shetani maana ni roho yenye nguvu sana.
 
Shida sana, wanadam tunajisumbua kwa maengi yasiyo na tija kwetu, shetani hupenda sana umwagikaji damu katika vita.
 
vita zina malengo mengi tu ikiwemo kutaka kutawala,kutaka mali,kuonya,sababu za kibiashara,kutiana adabu n.k
 
Back
Top Bottom