Lengo la sisi kuwa hapa duniani ni nini?

Tunazaliwa, tunakua tunazeeka tunakufa!

Lengo la sie kuwa hapa duniani ni nini?

Kwa nini tuko hapa na tumetokea wapi, kwanini tunaishi hapa??

Kwa nini tunazaa watoto?

Tunawazaa Waje wafanye nini hapa wakati mwisho wao nikufa??

Siku zote tunaangaika na maisha kupata fedha ili kupata chakula cha asubui mchana na jioni, then tuna lala tunaamka tunaendela kutafuta fedha kwa ajili ya chakula cha asubui mchana na jioni tuna lala tena, siku zinakwenda tunazeeka tuna kufa, mzunguko unaendelea nini maaana yake???

Kuna haja ya kuzaa mtoto ili aje kupitia mzungukuko huu wa maisha?

Yaani kuamka asubui kwenda kutafuta, kula, kulala na kusubiri kufa??

NINI MAANA YA MAISHA, KWA NINI TUNAISHI?

Tunafanyaa meeengi, yote ni kama kujisahaulisha hitimisho letu (kifo)!!

Utajenga jumba kubwa kuliko yoote, utafanikiwa kupita binadamu wooooote duniani, utakuwa na pesa nyiiiingi sana mpaka hujui cha kuzifanyia lakini unakufa, sasa kwanini tunaishi hapa duniani??? Kulikua na ulazima gani wasie kuwepo hapa duniani kama tunakufa?

JeTunaishi ili tufe???

Nini maana ya maisha???View attachment 1575137
Ili kupata jibu sahihi ni lazima kwanza ujue ulikotoka na wapi utaenda baada ya kifo.

Angalizo ni kwamba sayansi haina majibu hapa maana nje ya uhai wa kimwili sayansi haipo.

Ivyo basi,jibu ni la kiroho zaidi maana roho inaishi nje ya uhai wa kimwili na hasa nje ya kifo. Ivyo lengo kuu la kuishi lipo kiroho zaidi na hapa duniani ni mapito mafupi sana yenye kuweka mstakabari wa kesho yako baada ya kifo...kwamba unaelekea kuzuri au kubaya jibu ni kupitia uliyoyafanya na unayoyafanya sasa,God is real not theory,He exists...try death you'll see this fact!
 
KUSUDI LA KUISHI NA KUFA NI KWAAJILI YA KRISTO

Biblia inaeleza wazi, "Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida."
Wafilipi 1:21 SUV

Kama hujaokoka kuishi kwako hakuna kusudi lolote la kudumu milele, ila kama umeokoka basi kuishi kwako kuna kusudi la milele. Hata Rick Warren ameandika katika kitabu chake cha "Maisha yanayoongozwa na malengo" kwamba lengo kuu la kuishi ni kumtumikia Mungu kupitia Yesu Kristo.

TUNAISHI kwaajili ya Kristo, kama yeye alivyokuja kuishi na kufa kwaajili yetu (2 Kor. 5:21). Ukitubu na kumwamini Kristo, uzima wa milele unaingia ndani yako basi unaanza kuishi kwaajili ya Kristo tu. Yaani kila unachowaza, unachosema na unachotenda kinakuwa na lengo la kumtukuza Kristo, kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.Flp 2:13 SUV

TUNAKUFA kwaajili ya Kristo, kwa sababu mtu aliyeokoka akifa, mwili unaenda kaburini ila yeye anaenda peponi kukaa pamoja na Kristo (Lk. 23:43), kusubiri mbingu mpya na nchi mpya iumbwe aingie humo. Ila mtu ambaye hajaokoka akifa mwili wake unaenda kaburini ila yeye anaenda kuzimu, akisubiri siku ya hukumu, ili ahukumiwe na Kristo, Kristo atawahukumu wenye dhambi kwenda motoni (Ufu. 20:11-15). Kuna aya ya Quran inayounga mkono pia kwamba Isa Bin Mariam ndiye atakayehukumu.

Kusudi la kuishi ni Kristo. Kwa sababu usipomcha Mungu yaani usipoishi maisha ya wokovu basi atakayekuhukumu ni Kristo utake ama usitake, na ukimcha Mungu utaenda peponi kuishi na Kristo.

Kristo ndiye kusudi la kuishi.
Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
Mdo 17:28 SUV
 
Hilo swali ni kama vile kuuliza kwanini mafuta ya kwenye injini yapo kwenye mzunguko yanaenda yanachomeka, yanazungusha injini na yenyewe yanakuwa Moshi. Lengo lipo la maisha ya binadamu ni kuitawala na kuiongoza Dunia na mambo mengine yaweze kwenda. We komaa tafuta pesa acha kukata tamaa kisa kuna kifo.
 
In simple term.

Kusudi la wewe kuwepo hapa ni "kujaribiwa" na kujifunza ama kwa kimombo kuwa tested, to learn.

Na kama utayqshinda majaribu haya basi utapewa Taji (Crown).

Kule ulipokuwepo kabla haujaja hapa hakukua na forum ya wewe kujaribiwa na kujifunza ndo mana umeletwa hapa .
 
Wewe ndiye unaelala usiku. Mda huu watoto wanamezeshwa dawa ya usingizi ili wafanye yao, wengine wapo nje wanalinda,wengine wapo pub na wengine wapo na ibada kwenye masina gogi
 
KUSUDI LA KUISHI NA KUFA NI KWAAJILI YA KRISTO

Biblia inaeleza wazi, "Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida."
Wafilipi 1:21 SUV

Kama hujaokoka kuishi kwako hakuna kusudi lolote la kudumu milele, ila kama umeokoka basi kuishi kwako kuna kusudi la milele. Hata Rick Warren ameandika katika kitabu chake cha "Maisha yanayoongozwa na malengo" kwamba lengo kuu la kuishi ni kumtumikia Mungu kupitia Yesu Kristo.

TUNAISHI kwaajili ya Kristo, kama yeye alivyokuja kuishi na kufa kwaajili yetu (2 Kor. 5:21). Ukitubu na kumwamini Kristo, uzima wa milele unaingia ndani yako basi unaanza kuishi kwaajili ya Kristo tu. Yaani kila unachowaza, unachosema na unachotenda kinakuwa na lengo la kumtukuza Kristo, kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.Flp 2:13 SUV

TUNAKUFA kwaajili ya Kristo, kwa sababu mtu aliyeokoka akifa, mwili unaenda kaburini ila yeye anaenda peponi kukaa pamoja na Kristo (Lk. 23:43), kusubiri mbingu mpya na nchi mpya iumbwe aingie humo. Ila mtu ambaye hajaokoka akifa mwili wake unaenda kaburini ila yeye anaenda kuzimu, akisubiri siku ya hukumu, ili ahukumiwe na Kristo, Kristo atawahukumu wenye dhambi kwenda motoni (Ufu. 20:11-15). Kuna aya ya Quran inayounga mkono pia kwamba Isa Bin Mariam ndiye atakayehukumu.

Kusudi la kuishi ni Kristo. Kwa sababu usipomcha Mungu yaani usipoishi maisha ya wokovu basi atakayekuhukumu ni Kristo utake ama usitake, na ukimcha Mungu utaenda peponi kuishi na Kristo.

Kristo ndiye kusudi la kuishi.
Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
Mdo 17:28 SUV
Ushahidi huu sina uhakika kama unatoa majibu ya muulizaji. Single based evidence ni weak lete ushahidi mwingine nje ya vitabu hivi ambavyo uki reason unakitupa
 
Hatukuzaliwa Kwa bahati mbya kuna kusudio maalum lkn Weng ukweli wanaukimbia labda kwaajili ya kupumbazwa na dunia ambayo muda wte watu wako busy kutafuta mali mwishowe hazina maana yeyte tena tuna jiuliza Kesho tutakula nin lkn atujiulizi tukifa kinaendelea nin
 
Utaishi humu Duniani ukifa utazaliwa kwingine!! na mtu mwingine yeyote!! na mahali pengine popote, kuna waleee wanakufa wakiwa maprofesa kwa bahati nzuri ile kumbukumbu inabaki, basi hapo ujue

ndo wale watoto wanaofanya maajabu Duniani km mbugua!! kitoto hakijasoma popote lkn kinajua Computer science vibaya sana! zaidi ya mtu mwenye degree! ...kila mtu kuna wakti anaota ndoto akiwa mahali asipopajua kabisaaa!

mpaka unajiuliza ivi hapo nilipoota nikiwapo ni wapi? basi jua huko usipo pajua maishani ndo maisha utakayoishi kifoni ukitaka kuhakikisha hili andika mahali ndoto zako uone.....

hata wkt mwingine unaota watu hujawahi kuwaona lkn unawaota!! sasa ujue ile ni roho yako inazurula huku na huko hailali hata ukifa leo wewe utajiona mzima tu!

inawezekana mleta mada alisha kufa miaka miingi sana!! lkn yupo!! ndo maana unaweza kwenda sehemu tofauti kabisa humu Duniani lkn unaona km ulisha fikaga hapo!!! ...au ukamuona mtu tu!! ukajiuliza niliwahi muona wapi huyu ntu?
 
Acheni propaganda uchwara hakuna mtu aliyeumbwa na kiumbe anaitwa Mungu ,watu walikuwepo na kutokea
Kwa mfumo wa nature na waliishi kama primitive wakuitwa Zamadam hapa East Afrika hasa maeneo ya Oldupai gorge baadae Sana wakaja viumbe kutoka galaxies za juu wakuitwa Annunaki wakashukia kush wakamwongezea DNA primitive akawa homo sapiens Sapiens na akatumika kama man power wa kusaidia uchimbaji dhahabu na ndio kush dhahabu ya kwanza inagunduliwa na baadae Annunaki wanaamua kuchukua DNA zao wakichanganya na zetu maabara wakamproject Caucasians ambaye ni mzungu na jamii zake ,ndio ustaarabu wa kwanza watu na binadamu unaanzia hapo zinazaliwa civilization za kale kama Sumerians Assyrian Babylon Egyptian Kush Aztec Maya Peru Indus valley nk
Tulikwepo duniani Kwa kazi Moja TU kuchimba dhahabu na baada ya project kuisha Annunaki wakarudi kwao na kutuacha tukitanga Tanga TU bila mchunga ndio hapo nadharia za miungu zinazaliwa binadamu na watu kuabudu viumbe kutoka Juu wakitengeneza Hadith na mapokeo ya kwamba ipo siku watarudi wale miungu walio wafanyia project
Wazungu wanaujua ukweli huo na ndio maana huoni wakihangaika na mambo mengine Zaidi ya kujiimarisha na wao wasepe Sayari za mbali huko kama walivyosepa Annunaki hawafanyi vitu Kwa bahati mbaya
Mwenye kuelewa na aelewe na mwenye masikio na asikie na atie akili huu sio wakati wa kuendelea kua watumwa wa fikra amkeni tumechelewa Sana!
 
Toba!😀
 
Kuna thread moja nilijaribu kuelezea mawazo yangu juu ya hiki kitu sema mods wakaitumbukiza kwenye jukwaa la dini huko.

Ila kwa mimi naamini kuwa; tupo duniani si kwa mapenzi yetu. Sisi ni kamq mimea shambani kwa mwenye shamba. Mimea hiwezi ikajua kwa nini ipo hapo ila itishi kulingana na utaratibu na kanuni za asili yake, lakini mwenye shamba ndiye anajua kwa nini mimea hiyo ipo shambani.
Inafikirisha sana!!

Lakini huyo mwenye mimea yake , kwa nini atupatiashe tabu hivi ,
Au ni kama sisi tunavoamua kufuga kuku, unawalisha na kuwatunza wao wana kuwa na mipango yao kumbe wewe unasubiria sikukuu uwachinje!!!
 
Hapo mwisho sasa, hahahaha kwamba nsha fanyajeeeee?
 
Tunazaliwa, tunakua tunazeeka tunakufa!

Lengo la sie kuwa hapa duniani ni nini?

Kwa nini tuko hapa na tumetokea wapi, kwanini tunaishi hapa??

Kwa nini tunazaa watoto?

Tunawazaa Waje wafanye nini hapa wakati mwisho wao nikufa??

Siku zote tunaangaika na maisha kupata fedha ili kupata chakula cha asubui mchana na jioni, then tuna lala tunaamka tunaendela kutafuta fedha kwa ajili ya chakula cha asubui mchana na jioni tuna lala tena, siku zinakwenda tunazeeka tuna kufa, mzunguko unaendelea nini maaana yake???

Kuna haja ya kuzaa mtoto ili aje kupitia mzungukuko huu wa maisha?

Yaani kuamka asubui kwenda kutafuta, kula, kulala na kusubiri kufa??

NINI MAANA YA MAISHA, KWA NINI TUNAISHI?

Tunafanyaa meeengi, yote ni kama kujisahaulisha hitimisho letu (kifo)!!

Utajenga jumba kubwa kuliko yoote, utafanikiwa kupita binadamu wooooote duniani, utakuwa na pesa nyiiiingi sana mpaka hujui cha kuzifanyia lakini unakufa, sasa kwanini tunaishi hapa duniani??? Kulikua na ulazima gani wasie kuwepo hapa duniani kama tunakufa?

JeTunaishi ili tufe???

Nini maana ya maisha???View attachment 1575137
Tunazaliwa tunakufa ili kuendeleza uhai dunian , sababu ya kuwepo Ni kuendeleza uhai nakuitunza dunia
 
Back
Top Bottom