Lengo la kuanzisha hifadhi ya Burigi - Chato lilikuwa ni nini?

Aladeen04

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
3,519
5,683
Wakubwa zangu habari ya majukumu?

Leo katika kuangalia Channel yetu ya kizalendo Tanzania Safari Channel kuna documentary inaelezewa ya wanafunzi wa Chuo cha Mwika ambao wamepelekwa kwenda kufanya utafiti kule hifadhini, kiuhalisia mpaka sasa naona vijana wa watu wamepelekwa kuteseka kule kwa sababu wanyama hakuna na kuna mwanafunzi kaelezea kuwa wanyama wakiona watu wanakimbia kwa hofu ya kuwindwa.

Lengo kuu la kuanzisha hifadhi ile ni lipi? Kuna watalii ambao huwa wanaenda kule kutalii?
 
Bila Shaka hiv majuzi umesikia Basi la kigoma lililotekwa juzi na watu kuvuliwa nguo .

Hilo pori halipaswi kuachwa hivyo hivyo tu na Kuna barabara kuu ya kuelekea bukoba na Uganda inapita

Acha tu liwe hifadhi ya taifa wataweza kucontrol ule ujambazi. Halafu Kuna wanyama mule ambao pia hawako managed vzr
 
Wakubwa zangu habari ya majukumu?
Leo katika kuangalia Channel yetu ya kizalendo Tz Safari Channel kuna documentary inaelezewa ya wanafunzi wa chuo cha MWEKA ambao wamepelekwa kwenda kufanya utafiti kule hifadhini, kiuhalisia mpaka sasa naona vijana wa watu wamepelekwa kuteseka kule. Lengo kuu la kuanzisha hifadhi ile ni lipi? Kuna watalii ambao huwa wanaenda kule kutalii?

Dada Suu Matunguli na Jiwe ndio wanajua.
 
Sijajua viability yake ila kipi kinaanza Watalii au Sehemu ya Kutalii ?
Kwa akili yangu najua ni sehemu ya kutalii, ila kwa hali ya Burigi-Chato ilivyo inawezekana watalii wakaenda kule? Na wakienda wanaenda kuangalia nini maana kuna mwanafunzi ameeleza wanyama walioko kule wanahofu ya kuwindwa muda wote wakiona watu ni mbioooo.
 
Wakubwa zangu habari ya majukumu?
Leo katika kuangalia Channel yetu ya kizalendo Tz Safari Channel kuna documentary inaelezewa ya wanafunzi wa chuo cha MWEKA ambao wamepelekwa kwenda kufanya utafiti kule hifadhini, kiuhalisia mpaka sasa naona vijana wa watu wamepelekwa kuteseka kule. Lengo kuu la kuanzisha hifadhi ile ni lipi? Kuna watalii ambao huwa wanaenda kule kutalii?
Ile mbuga ilikuwapo siku nyingi sana hata kabla ya uhuru, kilichofanyika ni kuitangaza ijulikane tu; siyo kuwa ilianzishwa majuzi tu.
 
Kwa akili yangu najua ni sehemu ya kutalii, ila kwa hali ya Burigi-Chato ilivyo inawezekana watalii wakaenda kule?
Sijajua kama nilivyosema sijafanya upembuzi yakinifu huenda alihujumu uchumi..., au huenda kabla ya kuongeza hifadhi angeboresha zilizopo (ila hakuna kinachoshindikana hata kuna watu waliamua kujenga mahoteli kwenye jangwa....) Leo ndio Las Vegas
 
Lengo lilikuwa

1. 'kama kuna hifadhi Moshi na Arusha why not Chato'?
2. Kama hifadhi ndio zinawatia kiburi hawa ma mangi subiri sasa tuone, ngoja na sisi tuwe nazo.

Ujinga mtupu!
Hiyo sio sababu kwani mbuga Moshi ama Arusha zina mchango mdogo sana kwenye utalii.

85% ya watalii wanaokuja Tanzania hua wanakuja kwa ajili ya Serengeti na hao 15% ndio mbuga nyingine zote.

So hiyo sio sababu.
 
Sijajua kama nilivyosema sijafanya upembuzi yakinifu huenda alihujumu uchumi..., au huenda kabla ya kuongeza hifadhi angeboresha zilizopo (ila hakuna kinachoshindikana hata kuna watu waliamua kujenga mahoteli kwenye jangwa....) Leo ndio Las Vegas
Huko kwenye Las Vegas mkuu umeenda miles nyingi sanaaaa kaka yangu hali yetu huku kwetu tunaijua.
 
Back
Top Bottom