DaveSave
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 442
- 649
MAISHA ya William Malecela yanaakisi tafsiri ya binadamu mwenye sifa nyingi ndani ya mwili mmoja.
Msomi na kichwa ngumu. Mtu wa misingi na ndimilakuwili. Mpambanaji na mtoto wa baba. Hustler na gangsta with American spirit.
Msomi; makala alizokuwa anaandika kwenye gazeti la Jambo Leo, zilimpambanua. Msoma vitabu. Alijua vitu vingi. Alijenga hoja kwa depth reference.
Kichwa ngumu; yes, alipoamua kuukataa ukweli, ungedhani mbumbumbu.
Jambo Leo liliponunuliwa na Quality Group, mimi nikiwa Mwandishi Senior wa "Special Projects", niliona upungufu wa vionjo kwenye pullout ya siasa. Nikashauri tuwe na battle ya kalamu.
Nikapendekeza kwa Cheif Makunga, watafutwe Willy na Godlisten Malisa. Wapewe ukurasa, washindane ki-CCM na upinzani.
Ungeuona ukichwa ngumu wa Willy. Alipokosa hoja za kisomi, angebisha kama mbumbumbu wa mtaani. Ukurasa ulivutia.
Mtu wa misingi; Willy angeijua haki na kama hakuwa na masilahi ya upande, angenyoosha ukweli kwa ujasiri utadhani mjukuu wa malaika.
Ndimilakuwili; hakuwa na aibu leo kukugeuka hata kama jana alikusifu kwa mapambio ya kimungu.
Mpambanaji; mtoto wa waziri mkuu aliyepambania ndoto ya ubaharia, akafanya kazi ya udereva ili kujisomesha. Aliporudi Bongo, akakomaa na mitandao mpaka ikampa fedha.
Mtoto wa baba; yes, alikuwa "Daddy's Boy". Ungemsikia "my dad hivi au vile". Willy alimpenda sana baba yake.
Hustler; alipotaka chake alijishusha na hata kujitoa ufahamu.
Gangsta; angeamua kukufungulia ukauzu wake, hakuwa na msamiati wa woga kichwani. Alimvimbia jambazi mwenye bunduki Komakoma, Mwananyamala, mpaka alidata. Alimwambia: "Kama unashuti shuti, kama huwezi ondoka."
Aliingia kwenye mitandao kwa style ya majivuno (swank). Alilinda identity mpaka pumzi ya mwisho. Five Star dinner, lunch au bed moments. "Flying with My Bebe. You Know!" Alikuwa King of Swank.
Kifo cha Le Mutuz, kinaniambia one of our social media shapers, ameondoka. Alishepu mitandao kwa namna yake.
Nje ya mitandao; alikuwa muungwana, mwenye hisia. Aliumia alipoumizwa.
Mitandaoni; alionekana asiyejali chochote. Alitaka jamii imtambue kuwa Mfalme wa Social Media.
Usiku Mwema William a.k.a Le Mutuz.
Ndimi Luqman MALOTO