Lembeli: Muhongo anaiangamiza CCM

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,818
18,241
Kada maarufu wa CCM ambaye pia ni mbunge wa Kahama na mwenyekiti wa kamati ya Maliasili na utalii, Dr James Lembeli ametahadharisha kwamba kitendo cha Prof Muhongo kutowajibishwa au yeye mwenyewe kutoachia madaraka kwa hiyari, kitaiua CCM kabla hata uchaguzi wa mwaka huu haujatangazwa.

Kada huyo amemtaka rais kikwete kumfuta kazi muhongo ili kuinusuru CCM na chuki dhidi ya wananchi na hatimaye kufa kabisa baada ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa oktoba, 2015. Ametolea mfano wa Mwinyi na Lowasa waliowahi kuachia ngazi na hivyo kumshauri mhongo afuate mkondo huo endapo JK atagoma kumfuta kazi.

Amtaka ang'oke kufuta hasira za wananchi

Mbunge wa Kahama (CCM), James Lembeli, amemvaa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akieleza kuwa kuendelea kwake kuachwa kwenye wadhifa huo kunachochea hasira za wananchi.

Akizungumza na NIPASHE mwishoni mwa wiki, Lembeli alisema hajaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali katika kutekeleza maazimio ya Bunge katika kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

"Huwezi kumwambia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini apumzike apishe upelelezi, bosi wake ambaye ndiye mwenye instrument unamwacha," alisema.

Alisema: "Nafarijika kusikia kwamba process inaendelea lakini kadiri wanavyozidi kumwacha Muhongo kwenye hiyo nafasi ndio kadiri Watanzania wanazidi kuchukia, kukasirika na wanapandisha hasira na wanaichukia serikali."

"Nakupa mfano, kuliwahi kutokea kashfa nyingi mojawapo ni ile ya Richmond, Lowassa (Edward) alipewa nafasi ya kujitetea, alipewa nafasi ya kukaa kwenye madaraka wakati uchunguzi unafanyika?" alihoji.

Edward Lowassa alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu mwaka 2008, kufuatia kashfa ya serikali kuipatia kampuni ya kufua umeme ya Richmond zabuni ya kufua umeme wa megawati 100, wakati ilikuwa bandia na haikuwa na uwezo wa kufua umeme.

Lembeli alisema katika sakata la usafirishaji wanyama hai, aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, naye alijiuzulu japokuwa waliohusika kwenye sakata hilo ni maofisa wa taasisi zilizokuwa ndani ya Wizara yake.

"Sakata la Maige ambalo mimi nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi, Maige hakupewa nafasi ya kujitetea, aliondoka. Operesheni tokomeza, mawaziri wanne waliondoka na hawakupewa nafasi ya kujitetea, huyu Muhongo ni nani?" alihoji Lembeli.

Alisema kwa hali ilivyo, hata kama ni msafi, angewajibika kiutendaji kwa kuwa kashfa ya Escrow inahusu wizara anayoisimamia.

"Kuna sababu gani kuwapeleka watu mahakamani eti kuhoji namna walivyopata pesa halafu unamwacha mtu ambaye ndiyo mwenye mamlaka ya ile wizara, hakuna sababu, hawa ni vidagaa tu."

"Muhongo apumzike ni mwana CCM mwenzangu, lakini apumzike kwa sababu rekodi yake miaka ijayo haitakuwa nzuri kwa sababu anang'ang'ania kitu ambacho kitamharibia badae," alisema.

Alisema rais mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, anaheshimika nchini pamoja na kwamba aliwahi kujiuzulu aliokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Alisema kitendo hicho kilimjengea heshima na baadaye alikuwa Rais ambaye hadi leo anaheshima kuwa nchini.

Alisema hajaridhishwa na hatua zilizochokuliwa na serikali kwa kuwa waliopelekwa mahakamani ni vidagaa.

Waliotakiwa kuwajibishwa na ni Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco); Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri Muhongo, ambao walitakiwa kuwajibishwa na mamlaka ya uteuzi.

Wengine ni wenyeviti wa Kamati tatu za Bunge hilo, Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini), William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala) na Andrew Chenge (Bajeti).

Bunge lilishauri kuwa hatua za haraka zichukuliwe na Kamati husika za Bunge kabla ya kuanza kwa mkutano wa 18 wa Bunge.

Hadi sasa aliyefukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete ni Prof. Tibaijuka na huku Jaji Werema akijiuzulu.

Maswi alisimamishwa kazi na Katibu Mkuu, Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.

WALIOFIKISHWA KORTINI
Hadi sasa watumishi watano wa serikali wamefikishwa kizimbani kwa tuhuma za kupokea mgawo wa fedha za Escrow.

Vigogo wa kwanza kufikishwa mahakamani jumatano iliyoputa ni Teophil John, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Teophil walifikishwa mahakamani kwa kudai kudai na kupokea rushwa kutoka kwa James Rugemalira, Jumatano iliyopita.

Ijumaa iliyopita Mkurugenzi wa Fedha wa Benki Kuu (BoT), Julius Angello; Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Urassa na Meneja wa Misamaha ya Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kyabukoba Mutabingwa nao walifikishwa mahakamani.

Chanzo: Nipashe

:israel:
 
Kada maarufu wa CCM ambaye pia ni mbunge wa Kahama na mwenyekiti wa kamati ya Maliasili na utalii, Dr James Lembeli ametahadharisha kwamba kitendo cha Prof Muhongo kutowajibishwa au yeye mwenyewe kutoachia madaraka kwa hiyari, kitaiua CCM kabla hata uchaguzi wa mwaka huu haujatangazwa.

Kada huyo amemtaka rais kikwete kumfuta kazi muhongo ili kuinusuru CCM na chuki dhidi ya wananchi na hatimaye kufa kabisa baada ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa oktoba, 2015. Ametolea mfano wa Mwinyi na Lowasa waliowahi kuachia ngazi na hivyo kumshauri mhongo afuate mkondo huo endapo JK atagoma kumfuta kazi.

Chanzo: Nipashe

:israel:
tpaul wapotee hao tufanye yetu CHADEMA Lembeli ni mtu hatari sana ni kigeugeu asiye na msimamo thabiti hata ndani ya chama chake kwangu mimi namchukulia kama popo! Usishangae akiona anguko la ccm ni dhahiri akageuka na kuwa mwanaukawa tena mzungumzaji hasa
 
Last edited by a moderator:

hayo makapi ya kutoka CCM kama linataka kuja huko na lije tu , Muhongo ni mmoja wa watu ambao watanzania tulikuwa tunawahitaji muda mrefu sana, acheni wivu wenu.
 
Last edited by a moderator:
Lembeli kaisha hana jipya atafute pakutokea mwaka huu hachaguliki tena ndiyo maana anahaha kama anataka kutaga mpeni pole sana siasa siyo mafungu saba.
 
tpaul wapotee hao tufanye yetu CHADEMA Lembeli ni mtu hatari sana ni kigeugeu asiye na msimamo thabiti hata ndani ya chama chake kwangu mimi namchukulia kama popo! Usishangae akiona anguko la ccm ni dhahiri akageuka na kuwa mwanaukawa tena mzungumzaji hasa
Lembeli ni matehemu anayetembea mtakumbuka maneno yangu punde twendeni sawa atalia sana mwaka huu hata iweje hatoki.
 
hayo makapi ya kutoka CCM kama linataka kuja huko na lije tu , Muhongo ni mmoja wa watu ambao watanzania tulikuwa tunawahitaji muda mrefu sana, acheni wivu wenu.
Tena liondoke saa nane za usiku ili liondoke na nuksi zake zote anadhani kuwa na nywele nyeupe ndiyo kupewa uwaziri jk haangalii nywele bali anaangalia uwezo.
 
tpaul wapotee hao tufanye yetu CHADEMA Lembeli ni mtu hatari sana ni kigeugeu asiye na msimamo thabiti hata ndani ya chama chake kwangu mimi namchukulia kama popo! Usishangae akiona anguko la ccm ni dhahiri akageuka na kuwa mwanaukawa tena mzungumzaji hasa

CCM mnashangaza sana. Mtu anayesema ukweli mnamkejeli na kumuona hana maana. Ila wale mafisadi ndio mnawaona wana maana. Chama kinazidi kujifia.
 
Last edited by a moderator:
Tena liondoke saa nane za usiku ili liondoke na nuksi zake zote anadhani kuwa na nywele nyeupe ndiyo kupewa uwaziri jk haangalii nywele bali anaangalia uwezo.

lembeli anasumbuliwa na frustrations, miaka yote ya ubunge hata nyumbani kwake hajafanya kitu achilia mbali kwa wananchi wake. Anatumiwa na Wapinzani ili kudhoofisha majembe ya JK ili CCM ionekane haijafanya kitu
 
hayo makapi ya kutoka CCM kama linataka kuja huko na lije tu , Muhongo ni mmoja wa watu ambao watanzania tulikuwa tunawahitaji muda mrefu sana, acheni wivu wenu.

Akili za kupe hizi. Ng'ombe anachinjwa kupe hana habari, ngozi inachunwa kupe hana habari, ngozi inawambwa kupe hana habari... Ngozi ikianza kukauka kupe ndo anastuka.. haaaa kumbe ng'ombe kafa!!!

Siku ukija kujua ukweli utakuwa umeshachelewa sana mkuu..
 
Tena liondoke saa nane za usiku ili liondoke na nuksi zake zote anadhani kuwa na nywele nyeupe ndiyo kupewa uwaziri jk haangalii nywele bali anaangalia uwezo.

Duh ndo umeandika nini hiki? unaacha kuhangaikia mafuriko ya kule kwenye kibanda chako kwa mikatio unapoteza mda kuandika utumbo hapa...

You are too low!!!
 
Tena liondoke saa nane za usiku ili liondoke na nuksi zake zote anadhani kuwa na nywele nyeupe ndiyo kupewa uwaziri jk haangalii nywele bali anaangalia uwezo.

Jk ndio hana uwezo, tezi dume nalo limemuharibia kabisaaaaaa, anachoweza ni kuchekacheka tu.
 
Tena liondoke saa nane za usiku ili liondoke na nuksi zake zote anadhani kuwa na nywele nyeupe ndiyo kupewa uwaziri jk haangalii nywele bali anaangalia uwezo.
Mbona unakesha humu na mapovu yanakumiminika ukimtetea fisadi mwenye nywele nyeupe kama za lembeli ? Njaa ni hatari sana unatumika bila kujijua .
 
Jk ndio hana uwezo, tezi dume nalo limemuharibia kabisaaaaaa, anachoweza ni kuchekacheka tu.
JK ni jembe maneno yote haya ni ya kumgwaya tu na si vinginevyo, mtamkumbuka sana baba wa demokrasia afrika nzima, enzi za Mkapa mlikuwa hambwabwaji hivi
 
Back
Top Bottom