Kuna kipindi niliwahi kusema siasa za Arusha wanaozijua ni wana-Arusha wenyewe kwamaana wananchi hao hao wanaeleza kuwa wanakabiliwa na matatizo lukuki kwasababu hakuna utendaji mzuri wa Mbunge wao.
Jambo ambalo linasifiwa na wananchi ni kuhusiana na suala la machinga, angalau kidogo wanaeleza kuwa wamefanikiwa kukaribia kutimiza malengo yao (aliwapigania kwa kiasi flani kwamaana wkuna watu wanaouza bidhaa kwa kujihami ili wasije wakanyang'anywa mali zao) Pia angalia kilio cha akina Mama kufukuzwa nje ya Soko la Kilombero, Soko Kuu walipokuwa wanafanyia shughuli zao wanavyonyanyaswa na mamlaka husika hadi sasa, Mbunge halioni hili ili wafanyabiashara wadogo wafanye kazi zao kwa uhuru?
Ilifikia kipindi wananachi walimchukia Lema na baadhi ya viongozi wa Chadema kutokana na hali ya usalama jinsi ilivyokuwa na mauaji yaliyotokea, sasa tujiulize kuwa walioathiriwa na vurugu za maandamano, mabomu na lile tukio la mkutano wa Chadema Soweto, sasa hivi wamesaidiwaje na Mbunge tukiachilia nafasi ya Chama?
Nimefikiria hayo machache tu, mengi wanayo wana-Arusha.
Labda nikujuze kitu kimoja tu, Hapa Chuga watu ni waelewa wa kila kinachofanywa na serikali yako ya mabavu.
Ni lini Lema alileta bomu akawarushia wananchi wake? Jibu unalo na wanachuga tunaelewa vizuri sana.
Ni lini Lema aliwafukuza kina mama wa kilombero au soko kuu, wamama kule boma road, india road, goliondoi road n.k? Jibu unalo na wanachuga tunajua.
Soko la kilombero limegharimu hela nyingi ambazo siyo kweli.
Sokokuu tangia limejengwa kumefanyika upanuzi mdogo sana tena wa kitoto wakati mahitaji yameongezeka maradufu lkn hakuna jitihada zilizochukuliwa na halmashauri ya jiji zaidi ya kutafuna hela.
Lema aliwaambia wamachinga na wamama wasibugudhiwe, cha kufanya ni kuwatafutia sehemu yao Ya kufanya biashara.
Lilipokuwa soko original la kilombero mafisadi mkaja mkalimega mkaanza sijui ujenzi gani, Lema aliwaambia machinga na wamama eneo lenu la biashara ni hili hapa, watu wakajipangia sehemu zao mbona mlinywea?
Holo eneo ndiyo TIB wameridhika kuja kutoa mkopo wa kujenga soko pale. Sasa hiyo ni kidogo tu.
Kikubwa ni kwamba Lema katupa wigo mpana zaidi wa kuweza kufikiri, kujua na kukabiliana na maisha haya mnayotunyonga nayo.
Kumbuka:Mbunge hakupi hela, dawa, maji ya azam, barabara, hakupelekei mtoto shule. Mbunge anaisimamia serikali itoe na kuboresha huduma zote za jamii ktk eneo lake.
Nitaanza shule hapa nadhani