Eti ni kweli Rais wetu amesafiri na watu 50 & Freeman?

Status
Not open for further replies.
Apr 27, 2006
26,588
10,376
Haya jamani, je hizi habari ni za kweli kuwa rais wetu amesafiri na ujumbe wa watu 50, kwenda Uganda, Uarabuni, France, na sasa yuko huko US?

Kama ni kweli, huo ujumbe sio mkubwa mno kwa nchi masikini kama yetu? Mbona Mwinyi alipoenda Brazili na kundi kama hilo kulikuwa na makelele makubwa mno? This time arround mbona hatujasikia kitu kutoka media yetu mbuzi?

Now waht is Freeman doing with him kwenye ndege moja? Please I need a help to understand? Kama ni kweli?
 
Mzee ES,
Unajua nilikuwa nimepania sana kwenda kumwona JK huko DC. Atakutana na wananchi kwa balozi jumapili jioni saa 11 lakini yaonyesha nitashindwa... hadi hivi sasa bao bila bila maanake najiuliza kwenda kwangu huko kutabadilisha nini? kuna faida gani hasa ya mimi kumwona JK zaidi ya kusikiliza hotuba, kamba n.k.... Kutokana na msemo wako ktk mada ya mwendawazimu najikuja mnyonge. Mwenye nguvu mwache apite!...
Watu 50 hilo tena sina usemi kwani sifahamu hao wote wana kazi gani! pia kuna intro zinatakiwa ktk kuhamasisha wawekeshaji.. sii unajua tena wizara zenyewe zipo millioni.

Ikiwa Freeman yupo hii kidogo inanipa tena nguvu ya kwenda kumwona Free maanake miaka hatujaonana na mengi ya msingi tutazungumza.
 
Mzee ES na Mkandara ni kweli amesafiri na karibu idadi hiyo ya watu lakini siyo kama inavyosikika. Yaani hakuwa na kundi la watu hamsini katika msafara mzima. Aliondoka na wachache hadi uganda, wengine wakamtangulia UAE wakarudi nyumbani, wakati huo huo wengine wakatangulia Ufaransa wakarudi nyumbani na alipokuwa anakuja US wengine wakamtangulia Huku. Kwa upande wa Upinzani safari yake ya US yupo Mzee Cheyo UDP. So, siyo kundi la watu hamsini aliokuwa akizunguka nao kila mahali.
 
That makes a sense!, ila bravo kwa JK nasikia amekataa kufikia zile hoteli za dola $ 5,000 kwa siku alizokuwa akifikia mzee Ben, I mean what else could we ask from our president, nothing but understanding! Bravo na viongozi wengine ni lazima waige huu mfano, na waache mchezo wa kusafiri first class na business, matokeo yake safari ya dola 1500, inaishia kuwa $ 10,000 watu wawe na huruma na hela za wananchi!
 
kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuwasalimu wanabodi wote bila ya kusahau wale wenzangu waliotoka BCS ! Wanabodi kwa muda mrefu tangu JK achaguliwe kuwa rais amekuwa akimwagiwa sifa kem kem hapo nchini , na nimekuwa nikijiuliza maswali mengi nini hasa kilichowavutia wazalendo ?

Juzi nilipata habari ya kuwa JK angehutubia watanzania hapo Washington , basi bila ya kusita nilisafiri mpaka DC ili kuweza kupata nafasi ya kumsikiliza Rais wangu , kusema ukweli nimesikitshwa sana na speech yake ya kitoto aliyoitoa zaidi na jinsi walivyotastage maswali !

Maswali yaliyoulizwa ni mawili ,na yaliulizwa na wazee wa chama ambao instead ya kuuliza maswali walitumia nafasi hiyo kumpongeza kuchaguliwa kwake ! Jamani hotuba aliyoitoa ni ya kitoto na dhahiri inaonyesha ni jinsi gani alivyo shallow minded .Hotuba ya JK ilibase katika vitu vitatu watz tusisahau nyumbani na tuheshimu sheria za marekani.
 
Tausi,

Naomba utuletee briefly alichosema maana umetoa kidogo sana. Duh! umenishangaza sana kama rais hawezi kutoa muda wa maswali zaidi ya mawili!!!! kweli hatuna viongozi, mi nilifikiri mnaenda kuongea kama watu wa nchi moja na ikibidi si lazima uulize kwenye kadamnasi!!

Kwa hiyo zile hotuba zake tanzania ni za kuandikiwa kisha anasoma na kukariri??

FD
 
Tausi karibu! tuendeleze malumbano,

Now hebu tuwekee aliyoyasema kwa kifupi!, maana huku bongo tunaambiwa kuwa hata Bush eti anazimia naye? Je alimuona alipokuwa huko? Mbona picha hatujaona? Tumemuona nc Coondoleza lakini hatujamuona na mzee Bush? Je babu misifa angekutana na Bush bila picha?

Lakini tuwekee aliyoyasema, halafu mbona NY kaogopa kunana na watu? Hao wazee wawili waliotumiwa ni kina nani tuwekee tuwapatie maana wote huko wabongo tunawajua! Waweke hapa tuwapatie vipande!
 
Mzee E.S. : Bado nawasiliana na watu wa chama nyumbani ili nijue kama kweli Freeman yupo kwenye msafara na anafanya nini hasa! Nimepigisha bongo kujua mantiki ya Freeman kuwa katika huu msafara (kama kweli alikuwemo)bado sijapata logic!

Tausi itakuwa vizuri kama walivyosema wengine ukitupa angalau kwa muhtsari aliyoongea JK na mwaswali gani hasa wale wazee waliuliza. Karibu tena kwenye malumbano haya.
 
Mzee ES ,

Wazee walioluiza maswali ni wawili mmoja nasikia anatoka DC pale ubalozini na mwingine anatoka philadephia . Hawakuuliza maswali bali walitoa maoni ya kumsifia kikwete kuchaguliwa kwake na hii yote inaonyesha dhahiri ya kuwa maswali yote haya yalipangwa .

Watu wanasema nimeeleza kwa kifupi sana kutoka kwenye hiyo hotuba yake ,hakuna kitu cha kuelezea pale ulikuwa ni upotevu wa muda tuu . Vijana wengi walikuwa wakilaumu kupoteza muda wao kwani wengi waliacha kuhudhuria graduation mbali mbali na kuangalia mechi ya NBA iliyokuwa ikiendelea.

Mimi kilichonihudhi zaidi ni JK kutufanya watoto kwanza kwa kutusimulia kwa muda mrefu kwamba tukumbuke nyumbani , tusaidie nyumbani na tuheshimu sheria za huku . Sisi ni watu wazima tuambie unataka kufanya nini katika miaka mitano na jee sisi kama watz tuna nafasi gani ya contribute huko nyumbani. Tatizo ni kuwa huyu mtu alibebwa tuu na kuweka pale na amekuwa akivionga vyombo vya habari kwa muda.

Mzee es unasema bush aliongea na JK , hakuna Bush alimintroduce tuu kwa dick cheney na sababu kubwa ni kuwa Tanzania ni mjumbe wa baraza la usalama la umoja wa Taifa, kwa hiyo wamarekani wanavizia kura tuu katika mambo ya Iran

Wanabodi hata kama watu wanamchukia BWM lakini tumpe sifa kidogo, the guy was smart na alikuwa astage maswali !
 
Mzee ES,
Nasikitika sana sikuwepo ktk mkutano huo na sababu kubwa ni kwamba sisi wenyewe hapa tulikuwa na kijimkutano chetu ktk kuanzisha upya jumuiya ya Watanzania.
Aliyosema Tausi ni habari zinazovuma North America na hakika hata mimi nimejaribu sana kupata habari hizi kwa kirefu lakini imekuwa shida. Vijana wengi naofahamiana nao hawakwenda. Habari za Bush kukutana na JK, kusema kweli nimeziona tu ktk magazeti ya Bongo. Sijaona hata artical moja toka gazetini, tovuti wala radio inayosema hivyo zaidi ya Dick na C. Rice.
Tausi,
Umezungumzia kuhusu Mkapa, sijui kama umesahau kwamba ni JK akiwa kama waziri wa mambo za nje ndiye alikuwa akijibu sana maswali ya Mkapa. Mkapa mwenyewe jeuri na mara nyingi alijiepusha hasa nchi za nje.
Kusema kweli Tausi nadhani mimi nitasikitishwa sana na nyie kwa sababu hamkujiandaa.. JK hawezi kujibu maswali ambayo hayakuulizwa. Rais yupo pale kusikia wewe matatizo yako na kuyawakilisha kwa wahusika! nadhani mlitakiwa kudondosha swala la Uraia wa nchi mbili...
 
Jamani msiwe na wasiwasi.. kuna mambo ambayo Kikwete ameambiwa kabla ya mkutano huo na WaTZ.. Alipokutana na baadhi ya wabongo wakati wa kutiwa sahihi ile changamoto ya milenia... kuna watu walimwambia kuwa Balozi wa Tanzania US hafai, na ubalozi wetu hautetei maslahi ya wabongo kwani unatufanya tujisikie kama vile si ubalozi wetu... hayo yalisemwa kwa Kikwete mbele ya Balozi Daraja.... (ambaye alikasirika sana......)...
 
Kama hakutoa nafasi ya kuuliza maswali hilo ni tatizo kubwa sana. Mkandara sidhani kama watu hawakujiandaa; kama nafasi ya maswali haikuwepo wahudhuriaji wangefanyeje sasa hapo?
 
Mwanakijiji,
Shukran kusikia kuna watu wameyazungumza hayo... na kwa bahati nzuri nimesikia pia JK ameweka msisitizo wa kuwepo na jumuiya za Kitanzania ktk nchi za nje. Jumuiya ambazo zitakuwa na mawasiliano na balozi zetu kupitia uongozi wa hizo jumuiya..Huu ni uvumi unaoendelea kila kona na kwa bahati nzuri sana kumpaka balozi mbele yake ni dalili nzuri ya kutoonyesha unafiki..
Imekuwa bahati mbaya pia sikuweza kuhudhulia matanga ya ndugu yetu Max yaliyofanyika hapo Motown, hata hivyo ipo siku tutakutana. Ally na Kufakunoga hawa washikaji wangu wa karibu sana..
Mwanasiasa,
Kusema kweli mimi naifahamu sana tabia yetu wabongo..Tunasema sana nje lakini inapofika wakati wa mikutano na hasa kipindi cha maswali wengi hutoa hoja zao binafsi, sifaa nyingi na wakati mwingine pumba. real issues tunazikimbia kwa sababu ambazo hazifahamiki. Tunapenda sana kujikomba na kuonyesha usomi ili tupate mwaliko wa dinner na huko pia huwa vichekesho vitupu..Wote unaowategemea huvimba nakujiona keki kukaa na wakubwa meza moja.
kifupi hakuna hata siku moja maswali yanayohusu mapungufu ya rais mwenyewe ktk utawala ama mwelekeo wa serikali. Na yule anayeuliza maswali muhimu wengi hushangilia pale rais atakapo mtoa nishai muuliza swali, na record itawekwa vichwani mwa wabongo. Tunafurahikia sana pale kumetokea fedheha kwa hiyo unapotaka kuuliza hakikisha unashinda.
Ebu fikiria hizo nafasi za maswali mawili tu zimetumika ovyo! Naposema hamkujiandaa nina maana jumuiya yenu inatakiwa kuandaa maswali kabla..maswali ambayo yanawahusu wote na kwa faida ya Watanzania waishio Marekani ama DC. Swali kuhusu siasa za Bongo mtashindwa tu, politics sii mchezo mdogo kwa mtu anayeishi Marekani na hata siku moja huwezi kupata jibu. Mnatakiwa kukusanya data na kuyaweka maswali ktk orodha ya ratiba ya mkutano huo mapema na muhimu zaidi yawe maswala yanayowahusu nyie. Kumbuka hawa jamaa wanazo data zote kimaandishi na rahisi wao kutoka washindi..epukeni uvumi na habari za mtaani unless ndio hali halisi ambayo wao hawaifahamu. Hata huko white house maswali yote yanayoulizwa na waandishi wa habari huwa wanafahamu toka mwanzo kuna nafasi ngapi na vitu gani vitazungumziwa. Kwa hiyo labda hili fundisho kwetu kwamba kila tunaposikia kuna ugeni toka TZ tuwe makini na kujiandaa kwa maswal yanayowakiliwa UUMA. Sio kila mtu na swali lake kama vile mnada wa vitu. nasikia El yupo njiani pia kwa ziara nyingine DC kwa hiyo jiandaeni mapema.
 
Wajameni,
Nilikuwepo kwenye hafla ya JK nyumbani kwa Balozi hapa Washington jana. Lakini kwanza nisahihishe a few facts. Freeman hakuongozana na JK. Freeman aliwahi hapa siku mbili kabla ya JK. Hawakusafiri ndege moja na hivi niandikapo hawajaonana na wala sidhani wataonana kwani Freeman anaondoka kesho kurudi Bongo.
Mzee ES, juu ya JK kukutana na Bush mwandishi wake amepotosha kidogo. Lakini ukiisoma ile makala yake utaona kwamba JK alikuwa kwenye mkutano na VP Cheney na Bush dropped in, said a few pleasantries and then left. This was a working visit and not a state or official visit kama ilivyoandikwa. Pia State Dept imenote idadi kubwa ya delegation kukiwemo vijana 15 wa protocal ambao waliwasili wiki moja kabla eti kwa ajili ya kuwezesha safari. Lakini nilichoona wanafanya ni kubeba vifurushi tu vya shopping.
Mkandara, next time you plan to come to DC let me know. Would be happy to know you
 
Mwanakijiji, :D
Kwa kiongozi ambaye anasema alikuja kujitambulisha kwa Wamarekani inashangaza kwamba alikataa mahojiano na Washington Post na CNN. Lakini amekubali mahojiano na VOA kwa masharti kwamba ayaone maswali kwanza. Mahojiano yenyewe yamefanyika jioni hii na labda sehemu yatapeperushwa kesho na mahojiano kamili baadaye katika wiki.
 
Wazee wote,

Shukrani kwa info zote, jamani mzee Boaz vipi hakuwepo kwenye mkutano? Maana hata mzee BM alikuwa kabla ya kuja DC lazima atoe agizo la huyu mzee Boaz kutoruhusiwa kuuliza maswali?

Mzee Mwanakijiji,

Una sound kama apologist wa JK, kulikoni? Yaliyokusibu?

Mzee Jasusi,

Ninajua kuwa uko-on top ya hii issue na ninakubali kuwa unasema ukweli, lakini Free safari hii mbona hakutangaza safari yake kama kawaida? Halafu huko ubalozini DC kuna nini? Tunasikia makelele mengi mno! Mimi mzee Daraja nilikuwa ninamuamini kumbe naye bomu? Nasikia anaajiri kina dada wabongo anaotembea nao? Vipi JK aliambiwa, kwa ubalozi unazorota kwa sababu kina dada hapo chakula cha balozi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom