Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,760
Kwenye nyekundu tukopamoja kabisa...Dr. Slaa ni mtu mzima na atumie hekima na busara kulishughulikia hili suala haraka iwezekanavyo na kwa manufaa ya wananchi waliowachagua hawa madiwani. Tutaendelea kumheshimu Dr. Slaa kama atatuheshimu na kuelewa wale madiwani wana watu nyuma yao waliowachagua.
Sioni dhambi kukaa meza moja na CCM wakati huko bungeni mko na CCM na mnacheka nao. Sisi tuko nao pia huku mitaani, mahotelini, kwenye mabasi, kwenye nyumba za ibada n.k. Hawa ni wenzetu na tumetofautiana tu itikadi lakini hatuna uadui mkubwa kiasi hicho ambacho Lema anataka kuonyesha hapa Arusha. Ninamuomba Lema akue na aache mambo ya kuonyeshana ubabe ili tujenge nchi yetu kwani safari iliyoko mbele ni ndefu na kazi bado ni kubwa. Nitakuwa na uchungu mkubwa sana kama uzembe wa CDM utalifanya jimbo hili kurudi tena mikononi mwa CCM na mtakuwa mmepoteza sana credibility na support kwa jinsi ambayo itakuwa ngumu ku- reverse.
Kuhusu kukaa meza moja na CCM siyo tatizo kwa CHADEMA kwani CHADEMA ndiyo walikuwa wakitafuta mwafaka tatizo kubwa ni maamzi ya mwisho ya mwafaka huo..CHADEMA taifa wanasema hawakujua nini kinaendela lakini ukiongea na waliokuwa kwenye kamati ya mwafaka huo wanasema walikuwa wanapelekewa kila kilichokuwa kinaendelea na katibu alitoa mapendekezo yakiwemo 1. uchanguzi ufanyike upya 2. kugawana uongozi...hivyo waliokuwa kwenye kamati wanajiona kama waondiyo wana saritiwa na chama Taifa, Tukija kwenye ubabe wa Lema kama ulivyosema hapo juu binafsi sioni ubabe wa Lema hapo kwani alichokidai ilikuwa ni msimamo wa chama taifa na si kugawana madaraka na kama walibadiliaka basi inaelekea hakukuwa na mawasilianao ya Lema na madiwani waliokuwa kwenye kamati ya mwafaka.........Naomba nimuombe Dr. Slaa alifanyie kazi swala hili madiwa tuliwachagua sisi na mbunge tulimchangua sisi, tunakuwa kwenye wakati mungu kutenganisha watu hawa labda tuhakikishiwe kuwa makosa ya huyu ni a,b,c... hatutasita kuchukua maamzi...