Lema ukicheza utapoteza Arusha mjini for good

Mimi siku hizi nikiona habari za mgogoro wa madiwani Arusha huwa sizisomi, leo nimesoma kwa bahati mbaya tu! Ni kwa sababu naiona CHADEMA hiyoo inaenda kuangukia pua Jimboni Arusha Mjini kama watawafukuza hao Madiwani! CHADEMA wameingia kwenye mtego wa Magamba wa "Migogoro Syndrome" uliokimaliza NCCR na TLP! Namshangaa hata Dr Slaa hakuweza kujifunza baada ya kumpoteza kizembe kijana mahiri Kafulila hadi akaenda NCCR Mageuzi! Mabavu kwenye siasa hayasaidii siku zote!
 
Nazungumza kama supporter mkubwa wa CHADEMA na niliyemchagua Godbless Lema kama mbunge wangu. Niko mjini na niko mobile sana huwa nazunguka katika kata kadhaa za hapa mjini. Wananchi wengi ukiwasikia wanasema lazima waonyeshe support kwa madiwani wao waliowachagua kutokana na uamuzi waliotangaza jana. Mambo ya kamati kuu ya CDM haimsaidii mwananchi wa Kata ya Kimandolu, Sekei, Kaloleni n.k. ambao wanachotaka ni maendeleo na si migogoro ambayo haimaliziki. Wananchi walio wengi including viongozi wa dini wanaunga mkono muafaka na dhamira safi ya madiwani ya kutaka kuendelea mbele katika kuwatumikia wananchi na kuachana na malumbano.

Kutokana na mgogoro huu Lema ameanza si tu kupoteza umaarufu bali hata ushawishi kwa wakazi wa manispaa ya Arusha. Wengi tunaanza kumwona yeye na CHADEMA taifa kama watu wanaotafuta mambo yao binafsi na si kuwatumikia waliowachagua.
Naomba wajue wananchi wamechoka na hakuna mtu yuko tena interested na mvutano ambao siyo tu hauna mwisho bali ambao hauchangii hata asilimia 1% ya maendeleo katika kata zao.
Madiwani wameshikamana na wananchi kuliko Kamati kuu ya CDM inavyofikiri na kama watakosea wakawafukuza hawa madiwani basi wajue wamepoteza jimbo la Arusha kwa sababu watu hawa hawa ndio waliompigia Lema kura na hawatakuwa tayari kumpigia tena 2015.

Watu wanataka iwepo way forward na wasahau ya nyuma tujenge manispaa yetu na siyo kila wakati kutaka kuonyeshana misuli ya kisiasa kana kwamba ndilo lengo kuu la kuingia madarakani.

Please Lema anza kushughulikia malengo makuu ya maendeleo kama mbunge kwa mustakabali wa watu waliokuchagua kinyume na hapo tutakuona uliingia kwenye ubunge kwa personally motivated agenda na si vinginevyo. Kama hautafanya kazi kwa matakwa ya wananchi ndugu yetu hatutakuwa na jinsi zaidi ya kumtafuta mtu atakayeweza kufanya hiyo kazi.

Lastly but not the least namuomba sana Dr. Slaa asiwatishe tishe madiwani tuliowachagua kwani hakuwachagua yeye na hii ni sawa na kututisha sisi tuliowachagua. Dr. Slaa ni mtu mzima na atumie hekima na busara kulishughulikia hili suala haraka iwezekanavyo na kwa manufaa ya wananchi waliowachagua hawa madiwani. Tutaendelea kumheshimu Dr. Slaa kama atatuheshimu na kuelewa wale madiwani wana watu nyuma yao waliowachagua.

Sioni dhambi kukaa meza moja na CCM wakati huko bungeni mko na CCM na mnacheka nao. Sisi tuko nao pia huku mitaani, mahotelini, kwenye mabasi, kwenye nyumba za ibada n.k. Hawa ni wenzetu na tumetofautiana tu itikadi lakini hatuna uadui mkubwa kiasi hicho ambacho Lema anataka kuonyesha hapa Arusha. Ninamuomba Lema akue na aache mambo ya kuonyeshana ubabe ili tujenge nchi yetu kwani safari iliyoko mbele ni ndefu na kazi bado ni kubwa. Nitakuwa na uchungu mkubwa sana kama uzembe wa CDM utalifanya jimbo hili kurudi tena mikononi mwa CCM na mtakuwa mmepoteza sana credibility na support kwa jinsi ambayo itakuwa ngumu ku- reverse.

Mungu Ibariki Tanzania
Tumechoka na pumba za Chatanda. Waambie hao madiwani waende Tanga wakagawane nyadhifa.
 
Ndo maana mimi nataka wagombea Huru hivi vyama vyote vinamambo ya kipuuzi puuzi kama watu hawajaenda shule kabisa.
 
Aisee mwanakwetu umenigusa hasa. Jana nilisikitika sana nilipoangalia TV kumbe hawa madiwani wetu bado hawajaanza kazi. Barabara walizoahidi kutengeneza ziko taabani na ahadi nyingine nyingi bado hata kuanza kuzitendea kazi bado. Wananchi ni kweli tumechoka kusikia magomvi na sasa tunataka kusikia mipango na mikakati ya utekelezaji. La sivyo tutawaweka kiporo hadi 2015 tuashangaze CDM tuwape CUF nao wajaribu.
 
u real hv unabled mind
Dr Slaa lini aliamua yeye binafsi kuhusu issue ya ARUSHA?
yeye anasoma/anaweka hewani kilichoamuliwa na KAMATI au ulitaka shangazi yako ndiye awe mtoa taarifa za KAMATI?

Marytina lakini mgogoro wa Arusha unaotaka kunukia ndani ya chama ni kwa masilahi ya nani?
 
lema apoteze jimbo mara ngapi? Ajiandae 2015 kuja kufanya kazi za kichama tu makao makuu
 
Ndo maana mimi nataka wagombea Huru hivi vyama vyote vinamambo ya kipuuzi puuzi kama watu hawajaenda shule kabisa.
Mkuu usemayo ni ukweli mtupu kwani hawa madiwani wangekuwa wagombea binafsi kazi ingekuwa ishaanza na isingekuwepo Kamati kuu wala nini
 
Nafikiri Lema amesahau kuwa waliomweka hapo ni wananchi si Dr Slaa. Sasa ni lazima asome alama za nyakati kama walivyosoma madiwani wa Chadema.

Wananchi hawataki malumbano bali wanataka usalama, amani na maendeleo yya mji wao wa Arusha.
 
Nazungumza kama supporter mkubwa wa CHADEMA na niliyemchagua Godbless Lema kama mbunge wangu. Niko mjini na niko mobile sana huwa nazunguka katika kata kadhaa za hapa mjini. Wananchi wengi ukiwasikia wanasema lazima waonyeshe support kwa madiwani wao waliowachagua kutokana na uamuzi waliotangaza jana. Mambo ya kamati kuu ya CDM haimsaidii mwananchi wa Kata ya Kimandolu, Sekei, Kaloleni n.k. ambao wanachotaka ni maendeleo na si migogoro ambayo haimaliziki. Wananchi walio wengi including viongozi wa dini wanaunga mkono muafaka na dhamira safi ya madiwani ya kutaka kuendelea mbele katika kuwatumikia wananchi na kuachana na malumbano.

Kutokana na mgogoro huu Lema ameanza si tu kupoteza umaarufu bali hata ushawishi kwa wakazi wa manispaa ya Arusha. Wengi tunaanza kumwona yeye na CHADEMA taifa kama watu wanaotafuta mambo yao binafsi na si kuwatumikia waliowachagua.
Naomba wajue wananchi wamechoka na hakuna mtu yuko tena interested na mvutano ambao siyo tu hauna mwisho bali ambao hauchangii hata asilimia 1% ya maendeleo katika kata zao.
Madiwani wameshikamana na wananchi kuliko Kamati kuu ya CDM inavyofikiri na kama watakosea wakawafukuza hawa madiwani basi wajue wamepoteza jimbo la Arusha kwa sababu watu hawa hawa ndio waliompigia Lema kura na hawatakuwa tayari kumpigia tena 2015.

Watu wanataka iwepo way forward na wasahau ya nyuma tujenge manispaa yetu na siyo kila wakati kutaka kuonyeshana misuli ya kisiasa kana kwamba ndilo lengo kuu la kuingia madarakani.

Please Lema anza kushughulikia malengo makuu ya maendeleo kama mbunge kwa mustakabali wa watu waliokuchagua kinyume na hapo tutakuona uliingia kwenye ubunge kwa personally motivated agenda na si vinginevyo. Kama hautafanya kazi kwa matakwa ya wananchi ndugu yetu hatutakuwa na jinsi zaidi ya kumtafuta mtu atakayeweza kufanya hiyo kazi.

Lastly but not the least namuomba sana Dr. Slaa asiwatishe tishe madiwani tuliowachagua kwani hakuwachagua yeye na hii ni sawa na kututisha sisi tuliowachagua. Dr. Slaa ni mtu mzima na atumie hekima na busara kulishughulikia hili suala haraka iwezekanavyo na kwa manufaa ya wananchi waliowachagua hawa madiwani. Tutaendelea kumheshimu Dr. Slaa kama atatuheshimu na kuelewa wale madiwani wana watu nyuma yao waliowachagua.

Sioni dhambi kukaa meza moja na CCM wakati huko bungeni mko na CCM na mnacheka nao. Sisi tuko nao pia huku mitaani, mahotelini, kwenye mabasi, kwenye nyumba za ibada n.k. Hawa ni wenzetu na tumetofautiana tu itikadi lakini hatuna uadui mkubwa kiasi hicho ambacho Lema anataka kuonyesha hapa Arusha. Ninamuomba Lema akue na aache mambo ya kuonyeshana ubabe ili tujenge nchi yetu kwani safari iliyoko mbele ni ndefu na kazi bado ni kubwa. Nitakuwa na uchungu mkubwa sana kama uzembe wa CDM utalifanya jimbo hili kurudi tena mikononi mwa CCM na mtakuwa mmepoteza sana credibility na support kwa jinsi ambayo itakuwa ngumu ku- reverse.

Mungu Ibariki Tanzania

Madiwani wameisha sema kama hawawajui basi safari hii watawajua na hasa hasa Lema na hawako tayari kutumiwa kwa manufaa ya wachache yakujitafutia umaarufu wa kisiasa, Lema safari hii ameingia choo cha kike
 
lema apoteze jimbo mara ngapi? Ajiandae 2015 kuja kufanya kazi za kichama tu makao makuu
Lema anaona eti akigeuka nyuma atakuwa jiwe la chumvi. Ila mimi nasema afadhali ageuke nyuma awe jiwe la chumvi tutamkumbuka kuliko kuendelea mbele na kugeka vumbi ambalo litaishia kutawanywa na upepo na hivyo kutoweka kabisa. CDM acheni kuwa rigid mtavunjika wanjameni.
 
u real hv unabled mind
Dr Slaa lini aliamua yeye binafsi kuhusu issue ya ARUSHA?
yeye anasoma/anaweka hewani kilichoamuliwa na KAMATI au ulitaka shangazi yako ndiye awe mtoa taarifa za KAMATI?

It is feeble minded characters like these that form the bulk of CDM supporters.
Badala ya kujibu hoja mtu asiye na akili sawasawa anarukia kukejeli hoja.
Mimi si CDM lakini kwa la Arusha CDM inachezea shilingi chooni.
 
Hatua za haraka zichukuliwe kunusuru wananchi, malumbalo yawekwe pembeni.
 
Madiwani wameisha sema kama hawawajui basi safari hii watawajua na hasa hasa Lema na hawako tayari kutumiwa kwa manufaa ya wachache yakujitafutia umaarufu wa kisiasa, Lema safari hii ameingia choo cha kike

Ili kuumaliza hili shauri, ningeshauri hivi: Hao madiwani wa CHADEMA waliopata vyeo in exchange for muafaka waandae audience na ndugu & jamaa wa wale marehemu watatu wa January 5 pamoja na majeruhi wote then wawambie sasa 'mambo swafi' tumeshapata vyeo! Wafanya hivyo tu na kama wafiwa na majeruhi watasema hewala basi wananchi na CHADEMA mako makuu wawaunge mkono.
 
Ama kweli magamba kwa kujifanya Chadema! wewe unazungumzia Arusha gani ambayo watu wamepoteza imani na Lema? Hizo kata unazozitzja ni zipi? Kwani sisi tuko huku na hamna kitu kama hicho. Labda wewe ulitembelea tu Pangani basi.
 
Ni upuuzi kuungana na wauaji CCM kwa kupitia kurubuniwa madiwani. Kwani tatizo la muafaka ni suala la madiwani au la chama? Mbona anatajwa Pinda na Mbowe kuwa ndio waasisi wa muafaka; inakuwaje muafaka unafikiwa na madiwani kwa madiwani?

Wamekata kujiuzulu kwa nyazifa chache basi wafukuzwe tu.
 
Madiwani wameisha sema kama hawawajui basi safari hii watawajua na hasa hasa Lema na hawako tayari kutumiwa kwa manufaa ya wachache yakujitafutia umaarufu wa kisiasa, Lema safari hii ameingia choo cha kike

Ebu tufahamishe choo cha kike kikoje?
 
Asante kwa kuleta mada hii, kwa mtazamo wangu kama mkazi wa Arusha na supporter wa CHADEMA. Lema anapoteza umaarufu na umuhimu na hii ni dalili ya kulipoteza jimbo hili 2015. HAjaweza kugusa matumaini ya wapiga kura. Hajawatembelea kusikiliza shida zao, hajui vizuri jiographia ya watu wake hivyo hawezi kujua shida zao na kuzibeba wala kuzizungumzia. Watu wanachangishwa michango ya visima vya maji huku hakuna umeme katika eneo husika lakini hajawahi kulisemea. Ataje amehudhuria mkutano gani la wapiga kura wake kujua kero zake? Madiwani wana mwitikio mzuri kwa wananchi kuliko lema coz wako karibu na wananchi. Si kila malumbano yana tija. Mwalimu Nyerere alicopromise lkn tulipata uhuru
 
Acheni vitisho. Suala hapa la msingi ni lazima CDM wafuate kanuni na sera za chama, wakienda kwa mwendo wa kuwafurahisha madiwani na wananchi ndio kwanza watadharaulika. HAO MADIWANI WAFUKUZWE KABISA KWENYE CHAMA, HAWAWEZI WAKABISHANA NA KAMATI KUU YA CHAMA WAKATI HATA HUO UDIWANI WENYEWE WAMEUPATA KWA KUWA WANACHAMA WA CDM. Dr Slaa msipoteze muda waondoeni haraka kabla mambo hayajaharibika. Maendeleo ya Arusha yatakuja tu, after all maendeleo ya TZ kwa ujumla yamechelewa sana.

Mwisho nawaambia wana Arusha maendeleo hayaji kwa kuweka muafaka na CCM, maendeleo ya nchi hii tutaanza kuyaona tu pale tutakapoiondoa CCM madarakani. MSIDANGANYIKE CDM. MPAKA KIELEWEKE. Kama vipi wamsubiri Nape awape kadi za CCM.
 
Mnaounga mkono hoja hii hamjui siasa. Uchaguzi wa Arusha haukufuata taratibu, hilo ndilo tatizo. Utatuzi wake ni kwamba diwani wa sasa hivi na uongozi wote waachie ngazi, kisha uitishwe uchaguzi wa huru na wa haki. atayeshinda baada ya hapo basi!
 
Back
Top Bottom