Lema ukicheza utapoteza Arusha mjini for good | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema ukicheza utapoteza Arusha mjini for good

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Kwetu, Jul 21, 2011.

 1. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Nazungumza kama supporter mkubwa wa CHADEMA na niliyemchagua Godbless Lema kama mbunge wangu. Niko mjini na niko mobile sana huwa nazunguka katika kata kadhaa za hapa mjini. Wananchi wengi ukiwasikia wanasema lazima waonyeshe support kwa madiwani wao waliowachagua kutokana na uamuzi waliotangaza jana. Mambo ya kamati kuu ya CDM haimsaidii mwananchi wa Kata ya Kimandolu, Sekei, Kaloleni n.k. ambao wanachotaka ni maendeleo na si migogoro ambayo haimaliziki. Wananchi walio wengi including viongozi wa dini wanaunga mkono muafaka na dhamira safi ya madiwani ya kutaka kuendelea mbele katika kuwatumikia wananchi na kuachana na malumbano.

  Kutokana na mgogoro huu Lema ameanza si tu kupoteza umaarufu bali hata ushawishi kwa wakazi wa manispaa ya Arusha. Wengi tunaanza kumwona yeye na CHADEMA taifa kama watu wanaotafuta mambo yao binafsi na si kuwatumikia waliowachagua.
  Naomba wajue wananchi wamechoka na hakuna mtu yuko tena interested na mvutano ambao siyo tu hauna mwisho bali ambao hauchangii hata asilimia 1% ya maendeleo katika kata zao.
  Madiwani wameshikamana na wananchi kuliko Kamati kuu ya CDM inavyofikiri na kama watakosea wakawafukuza hawa madiwani basi wajue wamepoteza jimbo la Arusha kwa sababu watu hawa hawa ndio waliompigia Lema kura na hawatakuwa tayari kumpigia tena 2015.

  Watu wanataka iwepo way forward na wasahau ya nyuma tujenge manispaa yetu na siyo kila wakati kutaka kuonyeshana misuli ya kisiasa kana kwamba ndilo lengo kuu la kuingia madarakani.

  Please Lema anza kushughulikia malengo makuu ya maendeleo kama mbunge kwa mustakabali wa watu waliokuchagua kinyume na hapo tutakuona uliingia kwenye ubunge kwa personally motivated agenda na si vinginevyo. Kama hautafanya kazi kwa matakwa ya wananchi ndugu yetu hatutakuwa na jinsi zaidi ya kumtafuta mtu atakayeweza kufanya hiyo kazi.

  Lastly but not the least namuomba sana Dr. Slaa asiwatishe tishe madiwani tuliowachagua kwani hakuwachagua yeye na hii ni sawa na kututisha sisi tuliowachagua. Dr. Slaa ni mtu mzima na atumie hekima na busara kulishughulikia hili suala haraka iwezekanavyo na kwa manufaa ya wananchi waliowachagua hawa madiwani. Tutaendelea kumheshimu Dr. Slaa kama atatuheshimu na kuelewa wale madiwani wana watu nyuma yao waliowachagua.

  Sioni dhambi kukaa meza moja na CCM wakati huko bungeni mko na CCM na mnacheka nao. Sisi tuko nao pia huku mitaani, mahotelini, kwenye mabasi, kwenye nyumba za ibada n.k. Hawa ni wenzetu na tumetofautiana tu itikadi lakini hatuna uadui mkubwa kiasi hicho ambacho Lema anataka kuonyesha hapa Arusha. Ninamuomba Lema akue na aache mambo ya kuonyeshana ubabe ili tujenge nchi yetu kwani safari iliyoko mbele ni ndefu na kazi bado ni kubwa. Nitakuwa na uchungu mkubwa sana kama uzembe wa CDM utalifanya jimbo hili kurudi tena mikononi mwa CCM na mtakuwa mmepoteza sana credibility na support kwa jinsi ambayo itakuwa ngumu ku- reverse.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima mbele Mwana Kwetu.

  Mkuu umenena haswa sina cha kuongeza wala kupunguza.
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Maridhiano ya ARUSHA ni batili cdm taifa haiwezi kuyaridhia.

  Kama swala ni wanainchi na madiwani wao inakuwaje hao madiwani waliomba at first CDM makao makuu mpaka ikaandaa maandamano?
   
 4. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna chochote we ni mamluki Wa hao madiwani Kama kweli mbona siku lie ya sherehe ya kuwapongeza ilikwama?
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Teh teh! Nilimsikia Makinda akimwambia Lema nimekumiss!
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  u real hv unabled mind
  Dr Slaa lini aliamua yeye binafsi kuhusu issue ya ARUSHA?
  yeye anasoma/anaweka hewani kilichoamuliwa na KAMATI au ulitaka shangazi yako ndiye awe mtoa taarifa za KAMATI?
   
 7. peri

  peri JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Umenena mkuu, tatizo baadhi ya wanchadema hwataki kuambiwa ukweli. Wanataka kuwa kam magamba wanopenda kusifiwa tu bila kuambiwa wanapokosea.

  Wanaona baadhi ya watu ni malaika na hawawezi kuskoesa.
   
 8. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Naunga hoja lakini kwa shingo upande!
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280

  Why shingo upande.
   
 10. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Nilijua sitaungwa mkono katika hili na najua historia inaonyesha watu wengi walioleta changes walikuwa very unpopular kwa sababu upeo wao ulikuwa juu ya wengine na kufikiri kwao hakukuwa motivated by ushabiki. Ukitumia hisia badala ya akili lazima comments zako zitakuwa kama ulizotowa. Hata kama ametumwa na kamati kuu yeye ni sehemu ya hao watoa maamuzi. Kama utaendea kutoa utumbo basi wajaribu kuwafukuza wenyewe mtaona ninayo yasema.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red: Na hilo neno limekuwa linatumika for the last 50yrs! and guess what 70% na ushee wa kaya Tanzania wanakabiliwa na njaa, 14% ya ndio wenye access ya umeme wa MGAO, wengine vibatari! Sitaki ku-doubt ufuasi wako kwa CHADEMA, lakini watu wa ARUSHA na viongozi wa chadema Taifa waliandamana tarehe 5 Jan sio kwa kudai 'maendeleo' peke yake bali kudai utawala wa sheria na haki vitu amabavyo ndio msingi wa hayo maendeleo unayosema. Huwezi kuwa na matawi kama hakuna mti! Na madiwani wa Arusha need to be men enough to admit an error of judgement!
   
 12. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  lema kishapoteza kabisa tumaini la watu wa arusha
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  jMOSI mambo yatakuwa kama hivi


  [​IMG]
   
 14. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Mtu mkweli mara nyingi ni very unpopular na ukweli huungwa mkono na very few people lakini ukitaka upate wapambe wengi basi kuwa mnafiki. Mimi sitataka kuwa mnafiki ila nasema ukweli na ninachokiona. Diwani wetu hawajafanya lolote kusubiria decision za kamati kuu na wananchi wamepoteza uvumilivu na huu ndio ukweli. Wanataka mambo yaishe tujadili agenda nyingine. Kwa wasiokuwa Arusha watanitukana lakini huo ndio ukweli
   
 15. wasaimon

  wasaimon R I P

  #15
  Jul 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 222
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dawa ni muafaka na hili la kubishana na viongozi wa kitaifa halina maana, na tujue ya kwamba madiwani wao wanataka kuthibitishiwa kama walichukua ki2 kidogo kwa uvumi unavyoenezwa...baada ya hapo wako tayari kuachia ngazi, lkn ukweli utatoka wapi?, lkn ni kweli kwamba madiwani waliamua wao pekee kufikia muafaka bila ya viongozi wa chama wa mkoa au taifa kushirikishwa?... nadhani umefika wkt sasa kuyamaliza haya mambo na tuchape kazi kwani 2015 sio mbl kivile.
   
 16. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mimi siamini kama CDM wanachotafuta Arusha ni vujo, makubaliano ni jambo zuri na la kupongezwa lakini lazima kuwe na utaratibu. Watu wakubaliane kwa uwazi na kwa umoja pia. Watu wanatolea mfano maridhiano yaliyofanyika ZNZ lakini wanasahau kuwa ule ulikumwa mchakato ulioshirikisha sio tu wazungumzaji bali na uongozi wa vyama vyote hasa katika kupata taarifa za maendeleo ya mazungumzo. Nakumbuka kuna wakata watu wa CUF walikuwa wanasema kabisa kwamba baadhi ya mambo hatuwezi kuyaamua weneyewe mpaka turudi chamani na CCM walifanya vivyo hivyo.

  Jana nimemuona "Naibu Meya" anasema chama kilikuwa na taarifa kuhusu mazungumzo yao na CCM. Naamini kuna utaratibu katika chama chochote wa kupeana na kuhifadhi taarifa rasmi. Binasfi ningefurahi kama huyo "Naibu Meya" angetuletea angalau mfululizo wa barua au hizo taarifa zilizokuwa zinaenda makao makuu na majibu yake ili tuweze ku-establish hasa ukweli uko wapi. Haitoshi kuongea tu.

  Lastly, sio kila makubaliano yana manufaa, rejeeni historia.
   
 17. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  If that is the case why we don't see the END but the new BEGINNING of tensions. Kama ni utawala wa sheria na haki basi tuone haya mambo yakifikia mwisho waanze kufanya kazi. Au nayo hiyo haina deadline? watuambie wanakaa lini kujadili hizo differences na wanamaliza lini? Miaka 5 ni michache hebu angalia mwaka unaisha sasa na bado wako kwenye deadlock. How many years will be required to resolve this conflict?
   
 18. Mwana Kwetu

  Mwana Kwetu JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 60
  Hapo kwenye RED ndo kila mtu anataka ukweli wake uwekwe wazi.
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu! Naunga hoja mkono kabisaaaa.
   
 20. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  siasa bwana!leo nyota inang'aa kesho inafifia......wajifunze kwa kiranja mkuu wa nchi jinsi alivyokuwa kipenzi cha wengi na leo kageuka kero.
   
Loading...