Acheni vitisho. Suala hapa la msingi ni lazima CDM wafuate kanuni na sera za chama, wakienda kwa mwendo wa kuwafurahisha madiwani na wananchi ndio kwanza watadharaulika. HAO MADIWANI WAFUKUZWE KABISA KWENYE CHAMA, HAWAWEZI WAKABISHANA NA KAMATI KUU YA CHAMA WAKATI HATA HUO UDIWANI WENYEWE WAMEUPATA KWA KUWA WANACHAMA WA CDM. Dr Slaa msipoteze muda waondoeni haraka kabla mambo hayajaharibika. Maendeleo ya Arusha yatakuja tu, after all maendeleo ya TZ kwa ujumla yamechelewa sana.
Kwa wageni na wenyeji siasa za Arusha.
Je unafahamu Lema hakuwa wanazungumza na Diwani Malla na Diwani Bayo muda wote wa uchaguzi hadi walipowaomba wazee wenye busara ili kutogawanya chama?Je unafahamu sio mara ya kwanza Lema kuwatishia kuwafukuza Malla na Bayo kwa kupitia shemeji yake mkuu wa chama?
Je unafahamu Bayo na Malla walishawahi kumpiga marufuku Lema kwenye mikutano yao ya kampeni?
Je unafahamu kuwa Lema alituhumiwa kuwaweka rafiki zake kuwapinga Diwani Malla,Diwani Bayo,Diwani Mpanda(Rasta) pamoja na Diwani Ngowi pamoja na kupitishwa na chama?Ni baada ya kuona maji yamezidi unga ndipo alipoenda mwezi wa mwisho kujidai kuwauza kwa wananchi?
Je unafahamu slaa alipokuja arusha alifikia kufanya mkutano kwa diwani Malla sio kwa kuwa alikuwa anahitaji msaada ila ni kwa kuwa ndiye alikuwa na nguvu zaidi kwa madiwani wote wa chadema?Je unafahamu Diwani Malla pekee aliipa chadema kura 5,000+..
Je unafahamu kuwa hawa ndio madiwani ambao walitumia fedha zao na nguvu zao binafsi kufanikisha kupata udiwani bila hata senti tano toka kwa Chadema?
Je unafahamu kata zote lema alifanya vikao vingi vya kampeni ikiwemo sombetini na mjini kati Chadema ilipoteza?
Je unafahamu Lema ndiye aliyevuruga mchakato wa kupata viti maalum arusha kinyume na utaratibu wa Chadema?
Je unafahamu kuna tuhuma rushwa za ngono zilitumika kwenye uchaguzi wa viti maalum?
Tafakari