Lema ukicheza utapoteza Arusha mjini for good

Lema ukicheza utapoteza Arusha mjini for good

Muafaka kati ya ccm na magwanda ni kwa maendeleo ya watu wa arusha mjini na kata zake sasa mambo ya kamati kuu ya nini imagine ungekuwa hai karatu au kwa lisu hayo mambo madiwani pekee wanaweza kutatua hata bila kumshirikisha huyo lema wa kishumundu sijui ni uru tokea awe mbunge arusha vurugu tupu je wakichukua nchi je si ndo kabisaaaaa any way amebakiza miaka minne sijui atarudi kuwaambia nini wananchi atajivunia toka amechaguliwa migogoro ameongeza jijini arusha ina boa sasa tunataka maendeleo kama vipi municipal iendeshwe na tume tumechoka hatutaki migogoro siye
 
Lema ni mvivu wa kufikiri, tena haendi na wakati, wananchi wa ar wamechoka malumbano yasiyo na tija. Kwa kipindi kifupi wananchi wametambua mbivu na mbichi, cdm inaelekea kubaya!
 
All in all CDM Arusha mambo ni tete kuliko inavyoonekana. Madiwani ni watu wazima acheni kuwapiga mkwara kama watoto. Kamati kuu inatakiwa iwaonee huruma waliowaweka madiwani madarakani. Ukweli Mallah akifukuzwa aingie tu NCCR- Mageuzi au CUF tumpe kura zetu. Hatuko interested na procedures bali kazi ifanyike na ndio lengo la kuwachagua hawa madiwani.
 
LEMA na CHADEMA wako sawa kwa hili..nchi hii HAKI haijawai kupatikana kwa AMANI..

Kama ishu ni kupoteza ubunge bora haupoteze lakini amesimamia kwenye ukweri,sio vyema kuwa mnafiki au kupindisha mambo ili tu ubaki madarakani,huo ni USALITI ..kuusu maendeleo ya ARUSHA,maendeleo yataanza na utawala bora na utawala bora hautatokea chini ya CCM
 
Aisee mwanakwetu umenigusa hasa. Jana nilisikitika sana nilipoangalia TV kumbe hawa madiwani wetu bado hawajaanza kazi. Barabara walizoahidi kutengeneza ziko taabani na ahadi nyingine nyingi bado hata kuanza kuzitendea kazi bado. Wananchi ni kweli tumechoka kusikia magomvi na sasa tunataka kusikia mipango na mikakati ya utekelezaji. La sivyo tutawaweka kiporo hadi 2015 tuashangaze CDM tuwape CUF nao wajaribu.
Budget ilishapita sasa hawajaanza kazi vip? Kwani wao wanatoa hela mifukoni mwao? Nadhani watu hamjui kazi ya diwani mnadhani diwani ndo analeta hayo maendeleo. Maendeleo ni mipango ya halmashauri nzima na ikishapangwa wakakubaliana utekelezaji ni wa watendaji wa halmashauri ambao ni mkurugenzi na watumishi wengine. Madiwani kazi yao ni kuisimamia watendaji wale.Mimi nakataa kwamba mwafaka unachelewesha maendeleo! Hili si kweli naona hawa madiwani wanawapotosha watu kana kwamba wao ndo wanapesa za maendeleo. Kitu kingine ni lazima wajuwe kuwa serikali ya Arusha inaongozwa na ccm hivyo maendeleo si rahisi bila msuli wa kuwa ngangali kuwa bana na ikibidi kwa maandamano ya wananchi. Wananchi wana haki ya kupata maendeleo bila kujali nani anaongoza na kama hawafanyi hivyo wanayo haki ya kuandamana na kudai maendeleo yao.Watu waache kupotosha kuwa hawa madiwani wakifukuzwa eti watakosa maendeleo hiyo siyo kweli hata wakibaki kama wananchi hawatakuwa ngangali kudai ccm wanaweza kuwabania. Lakini wakiwa nagangali mambo yatakuwa sawa tu maana ni haki na kila kitu kinakubaliwa wakati wa budget.Mimi sikatai mwafaka lakini sikubaliani na uongo kuwa mwafaka unachelewasha maendeleo. Huu ni uongo ambao ndiyo unaotumiwa na ccm pia eti tukichagua wapinzani tutanyimwa mawndeleo.Naomba chadema waende arusha wakafanye mkutano kuwaelimisha watu juu ya huu uongo wa madiwani eti watanyimwa maendeleo kisa hajafikia mwafaka. Wananchi wanahaki ya kuandamana kama kutakuwa na upendeleo wa wazi wa kimaendeleo katika baadhi ya kata zinazo ongozwa na ccm na hili lazima litajitokeza tu kwa arusha.Wananchi lazima wafunguke sasa sio ule umbumbu wa kiccm.Come on Arusha? mbona mbona mlianza vizuri tukawaamini kwamba mnajua kudai haki zenu sasa mnataka tena kurudia umbumbumbu uleule? Hizi ni mbinu za magamba kuwachonganisha madiwani na cdm makao makuu maana walijua kabisa viongozi wa cdm taifa hawahongeki ndo maana wakapitia kwa madiwani ambao pengine waliupata udiwani kama dhalri tu lakini hawana msingi imara wa cdm.Hope all will go well ...na so far cdm makao makuu'wametumia busara sana y kuondoa kwanza mtego wa magamba kitu ambacho ndicho kitarudisha credibility ya wana arusha.Mungu ibariki Tanzani na watu wenye mapenzi mema.
 
Nimegundua kuwa humu ndani kuna ma Litle Thinkers wengi sana na sijui wamelipwa dola au paundi maana sipati picha kamili jinsi wanavyolazimisha ndoa ya mkeka kati ya chadema na magamba
 
You are dreaming a folitle dream, Lema na mjomba wake Mbowe hawana mbele wala nyuma, mjomba mtu alimpandikiza ili avae magwanda ya mtu fulani hapo kwenu cdm, ila mwipwa mtu kapwata ile mbaya, hahaaa, kwa hiyo kumuongelea lema, 'you are dreaming a folitle dream'

Upuuzi wako hauna mfano, labda na Mary Chatanda
 
Huu Mjadala unajadiliwa na watu wengi sana waliojiunga mwezi huu na wana POST chache sana ila wabishi hadi unashindwa kuamini kama ni watoto wa JF au tayari ni mijitu ambayo kila sehemu kumeshaota Unyoya.

Hebu chungezeni na nyie muone. Msijekuwa mnabisha na jitu moja ambalo lipo hapa miaka kibao ila siku nzima linashinda liki-LOG IN kwa jina hili na kutoka na baadaye lina LOG IN kwa jina jingine na kujipa Thanks na kujijibu kuwa LINAKUBALIANA.

Lete mpya mkuu, hizo mbona wote tunazijua sasa? Vita inapiganwa Ardhini na si ONLINE.
 
Ndugu MwanaKwetu,

Nimekusoma.

Muafaka feki huo, kwanini hao madiwani hawakufauata utaratibu?

KWa Rushwa Hizo madiwani hao walizokula si itakuwa rahisi kushirikiana na Chama la magamba kula rushwa na kuuzwa kwa viwanja kama kawa??

No way, They must go these Blood Betrayors
 
Tusibishe hata penye ukweli madiwani wako Karibu na wananchi kama wao wameona muafaka ndio suruhisho tuwasikilize. Sometimes we defend things which are not there...
 
Ni vigumu kuelewa wanachofanya CDM Arusha kama wewe si mpambanaji halisi. Mavazi ya CMD yenyewe yanamaanisha ''Man at Work''. Tukubaliane tu mafanikio hayaji bila pain. Hicho ndicho CCM wamekua wakitushinda nacho kila wakati. Mkichagua mpinzani wanabana maendeleo ya eneo husika mpaka mgawanyike/mjutie then next election wanawabeza mlichagua upinzani mlipata nini! Hata hiyo Southern Sudan isingekua nchi kama wangetarajia mafanikio kila baada ya miezi 7 baada ya uchaguzi. CMD wasipokua strong ktk maamuzi dhidi ya wanachama including Madiwani CCM itawarubuni wananchi kirahisi kuwa mnaona mmechagua upinzani na hasara zake? Mbona wao wameongoza majimbo mengi tu toka uhuruna yananuka umaskini wa kutupa
Mkuu tuko pamoja nadhani watu wengi hawajaelewa cdm wanapambana kutafuta nini?Hakuna maendeleo ya kweli bila kuwa na haki kwa kila mtu. Na hiki ndo kitu kikubwa kuliko mabarabara ya Rami na nguzo za umeme. Tunahitaji kila mtu athaminiwe utu wake na apate mgao wa haki wa haya maendeleo. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo wananchi wake wanawaogopa watawala na vyombo vya dola ili hali watawala hawa ni watumishi tu wa hawa wananchi na wanaishi maisha mazuri kwa kodi za wananchi hao. Tunataka wananchi wajione wenye thamani kuliko hawa watawala kwani wao ndo waajiri.Watu humu wanaongelea maendeleo kama ni favour ya watawala kwa watawaliwa. Na hili ndo gamba ambalo limewafunika wananchi wengi hata humu wamo kimbao akiwemo mvumbuzi. Maendeleo siyo favour ni lazima rasilimali na kodi za wananchi ziwaletee maendeleo kila mwananchi. Ni wajibu wa watawara kutumia rasilimali na kodi za wananchi kuwaletea maendeleo. Kama wakishindwa kufanya hivyo wananchi wanayomamlaka ya kudai kwa nguvu na hata kuiwajibisha serikali yao. Swala la maendeleo halitegemei ni chama gani kina tawara, kila mtawala anawajibika kwa kila mwananchi bila kujali alimchagua au la maana rasimali na kodi si mali ya chama wala serikali inayo tawala.Ni lazima tufike mahali tuyaelewa haya ndipo tutafanya upinzani wa kweli. Tukiendelea kuwa mbumbumbu wa kufikiri kuwa maendeleo ni hisani ya watawara na siyo haki yetu basi hatutakaa tuiondoe ccm madrakani na hatutakaa tufikie maendeleo ya kweli tukiendelea na ccm.Ni muhimu kwa cdm na wapinzani wengine kulielezea hili kwa nguvu zote hasa kwa Arusha kwa sasa maana watu waiowema wanatumiwa na magamba kuwadanganya wananchi kuwa maendeleo hayatakuwepo kwa sababu ya chadema. Ni lazima watu waambiwe kuwa wanayo haki ya kudai matumizi ya rasilimali na kodi zao bila kujali nani anaongoza halmashauri ya jiji la Arusha. Wananchi wana haki ya kuandamana na kudai mabadiliko iwapo wataona upendeleo wa wazi wa kimaendeleo katika kata au maeneo yanayoongozwa na madiwani wa magamba.Chadema please nendeni Arusha mkalifafanue hili na ndo itakuwa mwisho wa uongo wa magamba na magenti wao.Brother Lema nadhani unaweza kufanya hii kazi na tunajua itakuwa kitu rahisi kwako maana wewe ni mpambanaji usikubali kushindwa.
 
Acheni vitisho. Suala hapa la msingi ni lazima CDM wafuate kanuni na sera za chama, wakienda kwa mwendo wa kuwafurahisha madiwani na wananchi ndio kwanza watadharaulika. HAO MADIWANI WAFUKUZWE KABISA KWENYE CHAMA, HAWAWEZI WAKABISHANA NA KAMATI KUU YA CHAMA WAKATI HATA HUO UDIWANI WENYEWE WAMEUPATA KWA KUWA WANACHAMA WA CDM. Dr Slaa msipoteze muda waondoeni haraka kabla mambo hayajaharibika. Maendeleo ya Arusha yatakuja tu, after all maendeleo ya TZ kwa ujumla yamechelewa sana.


enhe!! wewe nawe ni mchambuzi wa mambo ya siasa?jamani naona kama wewe ni miongoni mwa washauri wa huyo slaa basi cdm inakufa haraka, matop kama haya unayamwaga hapa bila aibu?
 
Misingi ya maendeleo ni utawala wa sheri, uchaguzi huru na wa haki, <br><br>CCM inakiuka misingi hiyo na madiwani wa CDM wanataka kuungana na wavunja misingi kiasa wanataka kuleta maendeleo, wajiulize CCM ina miaka 50 madarakani lakini hakuna maendeleo, kwanini? Huwa CCM ni mabingwa wa kukiuka misingi ya maendeleo ambayo ni kuheshimu utawala wa shria na wa kidemocrasia.<br><br>Madiwani wa CDM watibu tatizo linalokwamisha maendeleo.
 
Madiwani hawa kama wanaona hakuna democrasia CDM waende CCM ambayo wanaona wana busara wakati ni CCM iliyotucheleweshea maendeleo miaka 50;
 
watu hawa hawa ndio waliompigia Lema kura na hawatakuwa tayari kumpigia tena 2015
Mkuu nakubaliana na hoja zako kwa kiwango kikubwa, na ninaamini hao viongozi uliowataja hasa kutoka makao makuu ni watu makini na watatilia maanani ushauri wako. Lakini si sahihi kulihusisha jimba la Uchaguzi kama mali ya mtu fulani nndio maana nimequote hiyo sehemu ya mchango wako.
Ni ukweli usiopingika kuwa CDM hawakuwa wanapigania madaraka tu pale ARUSHA MJINI bali ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu pamoja na Utawala Bora. Sasa njia pekee ya kupigania hilo si maandamano tu na kauli za kulaani bali ni pamoja nakuchukua hatua stahiki za kisheria kwa wote waliokiuka sheria na haki za binadamu. Je ni kesi gani zimefunguliwa kumshtaki, Mkurugenzi wa manispaa kwa kupindisha sheria? Je AG na IGP kkwa mauaji ya Arusha? Jibu ni hakuna? Sasa what next wakati maisha yanatakiwa yaendelee?

Kimsingi Chama cha Siasa kazi yake ni kupiga siasa lakini ufike wakati tuwe tunaangalia mambo beyond the political eye. Wananchi wanataka wawaone viongozi wao wakiwatumikia kwa kumobilize resources zao kwa manufaa yao, sasa madiwani wangekaa kimya, nini ingekuwa mwisho wa yote.

Halafu Mkuu, Mh. Lema hana hisa kwenye jimbo la Arusha mjini baada ya kipindi chake cha miaka mitano kuisha. Hiyo 2015 ni haki kwa MwanaCDM yeyote kupambana naye kwanza kabla ya kupitishwa na CDM.
 
kitendawili...
Hapo zamani za kale kulikuwa na mgombea wa urais toka chadema ambae alishindwa urais 2010.Mara baada ya kushindwa katangaza kutoutambua uchaguzi wa rais kwa kuwa ulichakachuliwa na usalama wa taifa.Pia aliamua kufanya maandamano nchi nzima ikifuatiwa na wabunge wa chadema kutoka nje ya bunge alipoingia rais kuhutubia bunge mwishoni wa mwaka jana.Kisa hawamtambui Rais aliyechaguliwa kwa kura za wizi na udanganyifu.
Kilichotokea sifahamu ila kimya kimya walianza kumtambua tambua na kuanza kusaini posho bungeni ,kupewa nafasi katika kamati mbalimbali za bunge na kupokea ruzuku ambayo ndiyo inaendesha makao makuu pale Kinondoni mtaa wa mfipa na kutoa mishahara za mgombea huyo zinazofanania na za wabunge a jamhuri ya muungano.
Sasa kama wao walifikia muafaka na Rais wa CCM au hawakufikia hadi kukubali kushiriki wote katika siasa za ngazi za juu itabidi mumuulize yeye kamanda mkuu mtakapomuona.

Ninachouliza kuna tofauti gani kilichotokea uchaguzi wa rais na hili la umeya Arusha.Mbona nyie mlikubali kuendelea na bunge na kusaini ruzuku kama hamumtambui rais.Msitudanganye kuwa kuna utofauti kati ya Rais na Urais..maana lugha naifahamu.Tunafahamu Mhe Marando aligombea Uspika wakati hamuitambui serikali iliyopatikana kwa udanganyifu na kama angeshinda angekuwa spika wa bunge hivi leo.

Kama muafaka ya madiwani ulisababishwa na njaa,nahofia ukaribu wa chadema kwa ngazi ya taifa pia unasababishwa na njaa.
Umeya na Uspika una tofauti gani? Kama wapiganaji kwelikweli msingeingia bungeni na msingemkubali Rais mpaka sasa hivi kama mnavowashauri wana Arusha kwa suala la Meya.
Maslahi ya taifa mbele siasa uchwara nyuma daima.Kuna tofauti kati ya siasa na uanaharakati..
Tafakari na chagua moja
 
Hakuna asietaka muafaka arusha, shida ni kwanini madiwani wa cdm walihongwa ili muafaka ufikiwe? Tusiwe mbumbu wa uelewa, maendeleo yoyote huletwa na chama kilicho madarakani
 
Hakuna asietaka muafaka arusha, shida ni kwanini madiwani wa cdm walihongwa ili muafaka ufikiwe? Tusiwe mbumbu wa uelewa, maendeleo yoyote huletwa na chama kilicho madarakani
Pinda kasema aliongea na mbowe,kuhusu muafaka....tunaomba mbowe akanushe hili,la sivyo CDM taifa inahusika.
Mnakwepa kujadili kiini cha mfarakano huu,....HAMNA MAJORITY ARUSHA!!
Kwa hiyo hamuwezi kuunda serikali ya halmashauri bila kushirikiana na chama kingine,thats the bottom line.
The rest is bullshit!
 
If that is the case why we don't see the END but the new BEGINNING of tensions. Kama ni utawala wa sheria na haki basi tuone haya mambo yakifikia mwisho waanze kufanya kazi. Au nayo hiyo haina deadline? watuambie wanakaa lini kujadili hizo differences na wanamaliza lini? Miaka 5 ni michache hebu angalia mwaka unaisha sasa na bado wako kwenye deadlock. How many years will be required to resolve this conflict?
Kwa nini umeona maendeleo yamechelewa sn kwa hii miezi michache sababu ya mgogoro huu wa Chadema na ccm,vipi kuhusu miaka 50 Serikali yako ya ccm imekufanyia sbb wewe ni mlipaji kodi!!!?
 
Back
Top Bottom