Lema: Tutapokea kigogo wa CCM

Lema: Tutapokea kigogo wa CCM

Anakuja na mtaji wa kura 800,000 (laki nane) za wale wanachama wa CCM waliomdhamini. Duuuh! CCM kama wanajuta vile!
 
Mbunge wa Arusha Mjini,Godblees Lema, amesema watapokea "kigogo mkubwa" kutoka CCM pamoja na wenyeviti wa mikoa na wilaya katika mkutano utakaofanyika Dar-es-salaam.

Mkutano huo utafanyika wiki ijayo kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Chanzo:Mtanzania

CCM mwaka huu lazima mtafute mchawi wakati mchawi/wachawi mlicheza nao mziki pale ukumbini.
Mkuu taarifa yako imejawa na tunga tata. Watapokea kigogo toka CCM kama mtu anaekuja kujiunga na CHADEA? au watapokea kigogo toka CCM kama mgeni Rasmi katika mkutano wao?
 
Waondoke tu hao mafisadi. Hawana chao CCM

Kipindi kile mliilaumu chadema kuwa waliwaita wanaoondoka cdm ni wasaliti sasa mnasema kila anayeondoka ccm ni fisadi. Hivi hii ni kweli? Sio kwamba wanachama wenu wanapinga kupindishwa kanuni kipindi cha uteuzi wa mgombea urais? Kila mtu anajua kuwa haki na demokradia haikutendeka ktk chama kikongwe cha ccm kinachojisifu kuwa kinajua demokrasia. Kwa nini kamati ikate watu? Tena bila kuwahoji? Hata mimi ningehama.
 
Si atangaze rasmi tujue!
Kila saa mnatutia mshawasha tu. Ila wasimpe uraisi!
 
Kama chadema wamefika hatua ya kumwalika lowasa kwenye chama chao, basi ni hatari. Kwa lugha nyingine wanamualika chenge, rostam na wengine wa aina hiyo! Watakuwa ni wapumbavu, binafsi nakatishwa tamaa na siasa za bongo hasa ninaposikia kuwa sasa lowasa ni mbeba bendera wa chadema. Sasa baada ya uchaguzi watatuambia kuwa wanapinga ufisadi?

Hivi Mchawi anapotubu na kuchoma tunguri zake zote na kua muumini safi wa Msikitini au Kanisani je ataendelea kua Mchawi?
CCM ni genge la mafisadi na wala rushwa au ni sawa na kundi la wachawi na walozi hivyo yoyote aliyepo huko hata kama si mla au mtoa rushwa lazima atakua mla na mtoa rushwa tu na hii ni kutokana na mfumo wake.
CDM ni iko tayari kuwapokea/kumpokea yeyote toka CCM kwani mfumo wake hauruhusu matendo ya kifisadi hivyo basi wewe kama ni type ya CCM ukiingia CDM mfumo utakubadilisha tu na utakua mtu safi na utakemea matendo maovu ambayo ulikua ukiyafanya kabla.
Lowassa na Team yake yote ambao mnawaita mafisadi ambao wamefikishwa hapo na mfumo wa CCM wakiingia CDM watakua sawa na mtu aliekua mchawi kisha akakata shauri na kumrudia Mungu.
CDM wakiwakataa watakua wamemkosea Mungu kwani lengo la Mungu ni kuwapokea wenye dhambi ili waachane na matendo yao maovu ili wawe mfano kwa wengine.
 
Anakuja na mtaji wa kura 800,000 (laki nane) za wale wanachama wa CCM waliomdhamini. Duuuh! CCM kama wanajuta vile!

Siyo hao tu kumbuka wenyeviti wa mikoa,wilaya nao pia wana watu wao
 
Itakua ni uchu wa uraisi uliopitiliza lakini pia it aleta chachu ya maendeleo isiyopimika. Twende kaz. Tanzania kwanza vyama baadae
 
Kipindi kile mliilaumu chadema kuwa waliwaita wanaoondoka cdm ni wasaliti sasa mnasema kila anayeondoka ccm ni fisadi. Hivi hii ni kweli? Sio kwamba wanachama wenu wanapinga kupindishwa kanuni kipindi cha uteuzi wa mgombea urais? Kila mtu anajua kuwa haki na demokradia haikutendeka ktk chama kikongwe cha ccm kinachojisifu kuwa kinajua demokrasia. Kwa nini kamati ikate watu? Tena bila kuwahoji? Hata mimi ningehama.

Daaaaa,ccm sasa wanatamani warudie mchakato upya
 
mapanya buku ya lumumba ni razima yatawanyishwe ata kwa kumshusha shetani.Atuna namna nyingine.
 
Teh Teh Dr.W.Slaa jitokeze hadharani utwambie utamfuta lini Lowasa kwenye orodha ya aibu?

Dr.W.Slaa naomba ujitokeze hadharani utwambie kama bado Lowasa ni fisadi au lah....
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom