Wiki hii Ni wiki ya mtikisiko. Hivi ndiyo unavyoweza kuelezea hali itakavyokuwa nchini kutokana na matukio makubwa ya kisiasa yanayotazamiwa kutokea ndani ya wiki inayoanza leo ambayo yanaweza kubadili mwelekeo wa siasa za Tanzania.
=========================
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anasema kwamba wiki hii itakuwa ni wiki ya mtikisiko kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa viongozi 950 wa CCM wanahamia Chadema. Viongozi hao ni kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na taifa.
Taarifa hizi Lema amezitoa wakati akiwapokea vigogo watatu na wananchama 30 kutoka CCM jana. Lema anasema kuanzia kesho (Jumatatu) kimbunga cha viongozi na wanachama wa CCM kuhamia chama cha ukombozi (Chadema) kitavuma kila kona ya nchi.
Vigogo hao ni Diwani wa Kata ya Moshono, Paul Matthysen na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Terat, Simon Mollel wote wa jijini Arusha.