It's ver true, serikali iliyoshindwa hata kununua vidonge vya panadol kwa baadhi ya zahanati zake vijijini, leo hii unaipachika jukumu zito la kununua madege ya Boeing 767, ni serikali ya aina hiyo ya ubabaishaji itaweweseka tu!!
Ni jambo ambalo ni next to impossible, kuona nchi kubwa kama TZ, iliyosheheni utajiri wa kila aina wa rasilimali tulizojaaliwa na Mungu, kama vile madini ya uranium, dhahabu, tanzanite, almasi na madini mengine mengi yenye thsmani, na pamoja nchi yetu kujaaliwa kuwa na gesi nyingi sana pamoja na mafuta, lakini ni jambo linaloshangaza kupita kiasi kuona nchi yetu shirika letu la Taifa la ndege la ATCL likiwa halina hata ndege hata moja, nchi jirani kama Rwanda, ambbako ni kanchi kadogo sana kenye eneo dogo sana linalofanana na mkoa wetu mmoja tu wa Singida, na kanchi ambacho hakina rasilimali zozote kilichojaaliwa na Mungu, kanchi hako kanatushinda kwa kwa kuwa na ndege zaidi ya nne wakati sisi tuna ndege ZERO!!!!
kuna mudau alitahadhalisha kuwa kuwa wengi hawatamwelewa..
Zile picha bado zina msumbua Lema kamamchezo hako nadhani kana mpashida
Kamanda Crashwise umemsoma huyu,kwa masikitiko makubwa nakuomba usomee hii post
Huyu Mtu sijui ana akili ya wapi! Kama alijua kuwa Shule hazina madawati, Hospitali hazina vitanda etc Mbona anapokea Posho ambazo angeweza kuamrisha zielekezwe kwenye shuguli nyingine za maendeleo? Mbona alipokea Milioni tisini ya shangingi? etc Godbless J Lema , na wabunge walalamikaji aina yake ni wanafiki na wanapoteza sifa za kuongoza wananchi kila uchao.
Lema amejenga hoja kisomi,
Tatizo wewe huwa unachangia bila kuwa na hoja. Kama ulimsikiliza Lema alisema Mh Raus anateua watu kwa kuangalia vyeti badala ya yfanusu na uwajibikaji. Hiyo ya usomi ni mawazo yaki. Avatar ---- inaonyesha upeo wako wa mawazo.Kwahiyo na LEMA ni mmoja wa wasomi nchi hii?
Lema hana uwezo wa kujenga hoja ikajengeka, labda vioja: Kumbuka hivi majuzi, Kenya Airways, imenunua Ndege mbili aina ya B777-300ER zenye uwezo wa kubeba abiria 400 kila moja. Lema anataka kusema nchi jirani ya kenya hakuna changamoto za HOSPITALI wala ELIMU? Je Kenya hakuna changamoto zozote za Kimaisha? Ifike mahali LEMA ache ujinga, wakati anaongea bungeni awaze kabla, asije akadhani kuongea bungeni ni kama anaongea na wahuni wenzie.
Huyo Mbunge mwingine aliyekataa posho - posho zake zimeshanunua madawati? mshauri arudishe zile USD250000 kila mwezi alizokuwa akitumiwa Germany.LEMA amekuwa ni mmoja wa wabunge vikwazo katika kampeni ya "SAY NO TO POSHO".
Mara kadhaa tumeshasoma comments za LEMA hapa jamvini alivyokuwa akimshambulia mbunge mwenzie ambaye amekataa kuchukua posho.
Kwahiyo na LEMA ni mmoja wa wasomi nchi hii?