LEMA ni zaidi ya MALEMA!

LEMA ni zaidi ya MALEMA!

Kwa kweli sishangai kwanini watu wengi wa arusha wanasema kuwa lema ni raisi wao.... kimsingi huyu jamaa anakubalika sana
 
Preta, mbona wamtetea sana Lema,
Watu maarufu wanatakiwa wawe na wake wengi au ????
 
Nini? Wee chalie acha kulinganisha bajaji na vogue!
Godbless Lema anapendwa jamani. Kaeni msikie tu,wengine tumejionea. Jana nilishindwa kuhudhuria kwenye kesi ya mteja wangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.Nilijikuta nimefika viunga vya Mahakama Kuu(kwakuwa Mahakama ya Rufani nayo uliketi humo jana) kushuhudia na kusikiliza kusikilizwa kwa Rufaa ya Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini.

Kwakuwa katika Rufaa hiyo kumewasilishwa Pingamizi la Awali kuwa Rufaa ni batili,Mahakama ya Rufaa jana ilianza kusikiliza pingamizi hilo kama inavyopasa. Pingamizi liliwekwa na upande wa Wajibu Rufaa ukioongozwa na Mawakili Wasomi Alute Mughwai na Akida. Kwa siku itakayopangwa,kutatolewa uamuzi wa pingamizi hilo baada ya maelezo juu ya suala hilo kutolewa jana Mahakamani hapo. Uamuzi huo wa pingamizi utafanya Rufaa ya Lema iendelee au isiendelee. Ni hivi,kama pingamizi litakubaliwa rufaa itatupwa yote. Kama pingamizi likitupwa,usikilizaji wa Rufaa utaanza.

Godbless Lema,kwa hapa Arusha,hufananishwa na Malema wa Afrika Kusini. Eti kwakuwa wote ni 'vipenzi' wa vijana nchini mwao. Lakini,kadiri nimjuavyo Malema wa kwa Mandela na Lema wa Tanzania,Lema yuko juu. Arusha nzima ilisimama jana.Mimi nisiwe msemaji sana.Ujumbe wangu ni kuwa Lema ni kiboko. Wana-Arusha bado wanamhitaji sana. 'God bless our King' wameandika bangoni wana-Arusha.
 
mkuu hata wewe huyajui hayo!
Hivi kuna Mhalifu anayejulikana na Polisi wasiwe na data zake? au unajitia upofu kwamba hujui CCM inahaha usiku na mchana kutafuta namna ya kumzima Lema lakini wanashindwa? Otherwise labda uniambie huo uhalifu anashirikiana na JK ndio maana vyombo vyote vya dola vinamuogopa.
 
Matola umeona siasa za magamba. Wakishindwa kutetea hoja wanakuja na ujinga kuwa Lema ni mhalifu na ana record ya uhalifu
Kama ana hiyo record hiyo kwa nini wanasubiri muda wote wasimpeleke ndani au wakamfungulia kesi ya aina hiyo
Mapimbi watupu achana nao.
 
Hivi kuna Mhalifu anayejulikana na Polisi wasiwe na data zake? au unajitia upofu kwamba hujui CCM inahaha usiku na mchana kutafuta namna ya kumzima Lema lakini wanashindwa? Otherwise labda uniambie huo uhalifu anashirikiana na JK ndio maana vyombo vyote vya dola vinamuogopa.

Sidhani kama atakuwa na cha kuongeza !
 
Preta, mbona wamtetea sana Lema,
Watu maarufu wanatakiwa wawe na wake wengi au ????
 
Preta;

Kamanda ni wa makamanda wote haijalishi jinsia.
Tutamuozesha kama zuma kimila basi
 
Inategemeana na aina ya viajana wanaobeba mabango hayo. JULIUS MALEMA mimi ninavyojua, huwa vijana wazee na makundi mbalimbali wanaacha kazi maofisini, biashara zao na kwenda kumsikiliza. Ni aibu kubwa sana kufananisha kazi anayoifanya JULIUS MALEMA kwa waafrika kusini na huyu jamaa wa arusha. LEMA ana mambo mengi sana anayojificha kupitia kivuli cha siasa. umaarufu wa LEMA hauna hata miaka miwili na kila mtu anajua kabla ya hapo alikuwa anafanyakazi gani tena kazi zinazohatarisha maisha ya raia wasiokuwa na hatia. Binafsi najua mji wa arusha unaweza kuwa wa kwanza kwa matukio ya uhalifu , so LEMA lazima atakuwa na marafiki wengi sana wanaotaka kujificha kupitia yeye na kwa maana hiyo wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa sana kwa vijana katika kufanya fujo na ikaonekana kuwa anashangiliwa LEMA.

Join Date : 1st October 2012
Posts : 20
Rep Power : 305

Likes Received : 3
Likes Given : 0

...
Magambaz at work..
 
nang'atuka bora usiongee kitu ambacho huna uhakika nacho
Kama huyo Lema unayesema ni mhalifu kuna vyombo vya sheria ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana. Kuna usalama wa taifa ambao iwapo watataka record za Lema wasingeshindwa kuzipata wamfungulie mashtaka. Tume ya taifa ya uchaguzi iliyompitisha Lema kugombea ubunge ina record zake. Kama ni muhalifu wasingeshindwa kumzuia kugombea. Hata hao waliofungua kesi wangekuwa na la kusema kuwa huyu ni mhalifu sugu hapaswi kugombea.
Katika mashtaka yake hilo halijaongelewa. Kuwaambia watu wote wanaompenda Lema kuwa eti ni wahalifu na kuna watu wanajificha nyuma ya Lema ni kuwakosea adabu watu wa Arusha. Na hilo unalosema kuwa wanaomshabikia ni vijana nafikiri unakosea sana maana wapiga kura wa Arusha sio vijana peke yao wapo watu wazima wenye shughuli zao.
Ungeangalia umati wa jana wakati wanatoka mahakamani au watu walioacha shughuli zao watu wazima na vijana kabla ya kuja hapa kutoa conclusion yako kuwa wanaomshabikia ni kikundi cha wahalifu wanaojificha nyuma yake.

Mkuu Mr Rocky hawa jamaa wa magamba kila siku wanashuhudia umati mkubwa wa watu wa Arusha wanaojitokeza katika mikutano ya Lema na kufika mahakamani kufuatilia kesi yake.

Kinachowaumiza kichwa ni kwamba Lema amefanikiwa kuwafunika kabisa wanaccm wote walioko Arusha pamoja na fedha zote walizonazo huku wakisaidiwa na vyombo vya dola. Kujaribu kuktaa ukweli ulio dhahiri kwamba Lema anaungwa mkono na wananchi wengi sana wa Arusha si vijana tu bali wazee na watoto wake kwa waume ni dalili za wazi za siasa za mtaroni wa maji ya chooni kama anavyosema Matola.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita Maranya kuna watu wanaongea vitu ambavyo hata uchunguzi hawajafanya. Yaani wanawafanya wakazi wa arusha hawana akili au malimbukeni na wanashabikia mtu ambaye ana record za uhalifu
Na kwa maana hiyo hata umati uliokuwa mahakamani ni kichaka cha wahalifu wanaojificha nyuma ya Lema
 
Last edited by a moderator:
Inategemeana na aina ya viajana wanaobeba mabango hayo. JULIUS MALEMA mimi ninavyojua, huwa vijana wazee na makundi mbalimbali wanaacha kazi maofisini, biashara zao na kwenda kumsikiliza. Ni aibu kubwa sana kufananisha kazi anayoifanya JULIUS MALEMA kwa waafrika kusini na huyu jamaa wa arusha. LEMA ana mambo mengi sana anayojificha kupitia kivuli cha siasa. umaarufu wa LEMA hauna hata miaka miwili na kila mtu anajua kabla ya hapo alikuwa anafanyakazi gani tena kazi zinazohatarisha maisha ya raia wasiokuwa na hatia. Binafsi najua mji wa arusha unaweza kuwa wa kwanza kwa matukio ya uhalifu , so LEMA lazima atakuwa na marafiki wengi sana wanaotaka kujificha kupitia yeye na kwa maana hiyo wanaweza kuwa na ushawishi mkubwa sana kwa vijana katika kufanya fujo na ikaonekana kuwa anashangiliwa LEMA.

Ndio maana nimesema kuwa kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mambo mengi katika mtandao huu na kugundua kuwa baadhi yao hata kama ni wa vyama vingine ila upumbavu umewatangulia mbele zaidi ya kile wanachokifikiria.
Kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kusimama mbele za watu na kusema kuwa wale walionekana pale mahakamani walikuwa ni vijana wahuni tu!! mbona na wazee wenye umri wao nao walikuwepo??! Kwanini tusikubali kama mtu amekutangulia umuite Kaka au Mama au Baba......!! Wewe endelea na mtazamo wako huo mfu lakini CDM ndio kwanza inachapa mwendo.
 
mmhhhhhhhhhhhhhhhh kuna upofu wa kuzaliwa na wa kujitakia kazi ipo! Jamani umaarufu wa Lema zaidi ya Arusha upo wapi? Si alijaribu M4C kwenye vitongoji vya Dar aliona shuguli ilivyokuwa ngumu; Malema kila kona South Africa ni gumzo na anakubalika na wengi sana acheni kufananisho mlima na kichuguu, kweli Mrisho Ngasa anacheza soka lakini kumfananisha na lionel Messi ni kichekesho na dhihaka kubwa kwa wapenzi wa soka!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
ndio nashangaa CUF wanasema wamekuja kuvunja kambi ya Chadema........

Wataishia chukua aibu ya Mkapa arumeru.Kwa ujumla CUF wamekwenda Arusha jivua nguo ili mahirizi na tatoo za wapenzi wao zionekane.Hata kama watatumika anzisha vurugu wakisaidiana na green guard na wakina X.Wanayo Kazi kubwa.Arusha watu wanaomba Mungu sana,na wapo vijana wa kutosha wanai feel CDM.

Wasichojua CUF ni kwamba Lema Tangu alipokuwa TLP alikuwa na mwendo huu huu.Sasa anajazia karama zote(zake+CDM), plus kuchoka kwa raia.CCM itapendwa Uswazi tuu kwa wale wenye kesi za mgofu ya urithi.
 
CCM wanarecord nyingi za uhalifu:-
1. Kukunjia TWIGA kwenye ndege na kutoroshea nje ya nchi
2.Kupandisha bei ya MAFUTA ili kupata fedha za kugharamia chaguzi zenu
3.Kuiba fedha nyingi Benki Kuu kwa ajili ya kuchakachau uchaguzi
4.CCM mme ua Raia wengi wasiokuwa na hatia; Iringa, Songea, Mbeya, Morogoro, Arusha, Nyamongo, Singida, Usa River, Zanzibar, Mwembe Chai Dar, Igunga nk
5. CCM mmeendelea kuwafelisha watoto wetu makusudi kwa lengo la kuwasababishia umasikini watanzania
6.CCM Mmeingia mikataba ya kukwapua rasilimali za watanzania zikiwemo MADINI ya Dhahabu, Almasi, Tanzanite, Rubi, Uranium, Makaa ya Mawe, Cobalt, Nikel na sasa GAS...CCM mmeweka matrilioni huko uswis

7. CCM mmemtesa Dr Uli sasa Mmenyamazisha kwa kumhonga akae kimya wakati wananchi wanaendelea kufa kutokana na kukosekana kwa huduma muhimu za kitabibu...

8. CCM Mnahujumu bandari yetu na kuikosesha nchi mapato ya dhahiri...


LIST ya UHALIFU WA CCM ni ndefu sana .... CCM mtupe list ya uhalifu wa LEMA...
5.
 
chama kwani huyo wa south africa alianzia umaarufu ghafla tuu na kupanda kama moto wa kifuu. May be wewe ndio kipofu huoni. Umaarufu wa mtu hauanzi kama moto wa kifuu unaanza taratibu kwenye mji then mkoa then unaendelea. Ana muda wake wa kupanda kwenye huo umaarufu unaoutaka wewe.
 
Last edited by a moderator:
Machalii wa Arusha mkishapata supu za ulimi wa ng'ombe mnakaa kwenye vijiwe vyenu na kuanza kumsifia Lema, bila sababu kumfananisha Lema na Malema, ni sawa na kufananisha mlima Kilimanjaro na mlima Tegeta.
 
Ahaaaaaaaaa.....!!! Kumbe nawe ni gumegume lilelile tu!! Subiri mwenye macho haambiwi tule
 
Back
Top Bottom