LEMA mikononi mwa LISSU...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Nimefarijika sana niliposikia kuwa Wakili Msomi Tundu Antipas Mughwai Lissu atajiunga na Wakili Msomi Method Kimomogoro kujenga hoja mbele ya Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa kuonesha mapungufu ya Hukumu ya Jaji Rwakibarila wa Mahakama Kuu. Wakili Lissu ananipa matumaini mapya. Matumaini ya kutendeka haki. Hapa Kimomogoro,hapa Lissu...pataeleweka tu. Wakili Lissu anampigania Lema na haki ya wana-Arusha kuwa Mbunge wao waliomchagua. Viva Mnadhimu Lissu...
 
Uzuri Lissu anawafahamu majaji wote nje ndani.Na wao wanamjua vizuri hivyo
hawatakuwa tayari kujichafulia taaluma yao.Hukumu itakayotolewa nahisi
itakuwa ya haki.Ukiona magari ya washawasha yanaanza kuingia Arusha basi
ujue wanataka kuchakachua hukumu.Hivi Nape yuko wapi mbona hii rufaa hajaitolea
hukumu kama alivyofanya mwanzo?
 
Lissu anaenda mbele ya jopo la majaji ambalo hana imani nalo!

so anataka wakihukumu kinyume na matarajio yake apate kigezo cha lawama?
 
Mbona ambao aliwataja wameondolewa na wambaki wale wenye sifa. Kama wewe ni mfatiliaji mzuri, utakuwa unafahamu kuwa Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ni mmojawapo aliyetajwa na Lissu ambaye hakuwa hata na degree moja ameondolewa kusikiliza rufaa ya Lema kama ilivyopangwa awali. Badalayake ameingia Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman ambaye ataungana Majaji wa Mahakama ya rufaa, Natalia Kimaro na Salum Massati ambao wote ni wa ukweli. Lissu hakusema majaji wote ni feki, ukisoma taarifa yake aliyoipeleka bungeni aliwataja wote kwa majina na mapungufu yao. Nashauri wakati mwingine tuache ushabiki wa kitoto.
 
Muu pia ilitakiwa awe na mwanasheria Ridhiwani Kikwete kwani kijana kasoma sheria na anaijua vizuri kabisa na uwepo wa kamanda Ridhiwani utasaidia na kurahisha ushindi wa Lema.
 
Kuonesha kwamaba Lissu alikuwa sahihi na issue ya majaji, yule jaji kihyo walimtoa na mbadala wake ni mkuu mwenyewe wa Mahakama, hiyo moja pili/mbili, Hivi si kuna uzi humu ndani unatoka kwenye gazeti la The Citizen likiwakariri viongozi wa TLS kwenda kwa mkuu wa kaya, topic ikiwa hi hii ya majaji vihiyo? Sasa ndo nimeelewa kwanini Kikwete aliomba, Bora Dr. Slaa aendelee na Ubunge lakini sio Tundu Lissu, kumbe alikuwa akimfahamu, Big up Jembe la ukweli.
 
Mbona ambao aliwataja wameondolewa na wambaki wale wenye sifa. Kama wewe ni mfatiliaji mzuri, utakuwa unafahamu kuwa Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ni mmojawapo aliyetajwa na Lissu ambaye hakuwa hata na degree moja ameondolewa kusikiliza rufaa ya Lema kama ilivyopangwa awali. Badalayake ameingia Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman ambaye ataungana Majaji wa Mahakama ya rufaa, Natalia Kimaro na Salum Massati ambao wote ni wa ukweli. Lissu hakusema majaji wote ni feki, ukisoma taarifa yake aliyoipeleka bungeni aliwataja wote kwa majina na mapungufu yao. Nashauri wakati mwingine tuache ushabiki wa kitoto.

mkuu lyimo, msamehe bure maundumula. kwa lugha ya kwetu maundumula ni mapovu hasa yale ya sabuni ya unga.
 
Maundu usipotoshe umma. Huyo dogo lissu hakusema kwamba hana imani na majaji wote nchini.

Lissu anaenda mbele ya jopo la majaji ambalo hana imani nalo!

so anataka wakihukumu kinyume na matarajio yake apate kigezo cha lawama?
 
Mda wote huu ccm wamechelewesha maendeleo ya watu arusha. Hakika wanayumba na kutapatapa.
 
Lissu anaenda mbele ya jopo la majaji ambalo hana imani nalo!

so anataka wakihukumu kinyume na matarajio yake apate kigezo cha lawama?

Chande ameshtuka na kumuondoa yule jaji mwenye sifa za kuwa hakimu wa mahakama ya mwanzo, kukosa kufanya hivyo, tasnia ya sheria ilikuwa inaandika kitabu kipya.

Tusubiri kuona vitambaa vitakavyolowa kwa kufuta majasho chande akitumia uwezo wa ziada asiaibishe MUHIMILI, akijua kuwa hata tusiosomea sheria tunajua kuwa lwakibarila kamkuta mtuhumiwa na hatia ya kukojoa hadharani kama mashtaka yanavyosema, lakini kamuhukumu kwa kosa la ujambazi wa kutumia silaha.

Chande kabebeshwa kiroba cha up.upu, kujikuna ni lazima!
 
Lissu anaenda mbele ya jopo la majaji ambalo hana imani nalo!

so anataka wakihukumu kinyume na matarajio yake apate kigezo cha lawama?

Ni moja ya tabia za Watanzania aina yako...husoma vichwa vya habari bila kuyatafuta maudhui ya habari yenyewe kwa undani wa habari yake...Itafute ile ripoti uone ilivyokuwa imeandaliwa...tena kwa kutaja na majina na si mifano ambayo mda fulani huwa ni ya kusadikika...Kawataja kwa majina na uchafu wao....Ila ki ukweli sikushangai kwa matazamo wa kimakengeza...
 
Muu pia ilitakiwa awe na mwanasheria Ridhiwani Kikwete kwani kijana kasoma sheria na anaijua vizuri kabisa na uwepo wa kamanda Ridhiwani utasaidia na kurahisha ushindi wa Lema.
huyu tungempeleka igunga akaokoe jahazi lilofumuliwa
 
Ni moja ya tabia za Watanzania aina yako...husoma vichwa vya habari bila kuyatafuta maudhui ya habari yenyewe kwa undani wa habari yake...Itafute ile ripoti uone ilivyokuwa imeandaliwa...tena kwa kutaja na majina na si mifano ambayo mda fulani huwa ni ya kusadikika...Kawataja kwa majina na uchafu wao....Ila ki ukweli sikushangai kwa matazamo wa kimakengeza...
Hapo kwenye ni mapungufu yao, kukosa sifa si uchafu
 
Lema anaudi kwa kishindo na yale makato yake kule bungeni anarudishiwa yote. Ni kati ya tarehe 20 na 22 Sept 2012
 
Back
Top Bottom