HILI LA JWTZ KUDAIWA KUONEKANA KURANDARANDA OVYO KWA MAKUNDI KATIKA MITAA MBALIMBALI NCHINI NA 'UGENI WA GHAFLA' WA RAIS KIKWETE KENYA ...???
Tangu WaTanzania kushuhudia kero na ukatili wa kihistoria uliovuka mipaka ya Jeshi la Polisi kumfumua utumbo nje mwandishi wa habari, Daudi Mwangosi, watu wengi sana huku uswahilini wala hatujajua kitu tabasamu kwa hili li-serikali li-ovu linaloongozwa na Rais Kikwete.
Hakika tangu damu imwagike machoni mwetu mchana kweupe mkoani Iringa kwa namna ambayo imepata kuitisha ulimwengu mzima, ni wazi kwamba WaTanzani tulio wengi kiwango chetu cha HASIRA DHIDI YA SERIKALI YA CCM hivi sasa imepanda maradufu zaidi ya kule nyuma tulipochakachuliwa kura zetu hivyo kwa sura halisi ilivyo, kamba laweza kukatika wakati wowote penye hata jambo dogo tu ilmradi watu wapate pa kumalizia hasira zao.
Na kama kumbukumbu zetu ni sahihi, kesi ya maonevu makubwa kwa yule Mbunge lulu kwa vijana kote nchini Tanzania ndio kama hivyo inatazamiwa kusikilizwa hivi karibuni. Hii inamaana kwamba karibia wote watakua wakiangalia kama kuna chao kwa mbunge huyu pale Arusha au ndio kusema ubabe wa Magogoni sharti lipewe njia.
Hadi hapo hofu yetu ni kwamba, kwa matumizi zaidi ya dola mitaani tuwatisha wananchi, endapo uonevu utaendelea kupewa nafasi zaidi, chozi la Daudi Mwangosi huenda likadondoka upya mitaani kote nchini.
Pindi unapoona wanajeshi wakitolewa kwa mara ya kwanza kambini na kuanza kurandaranda ovyo mitaani katika makundi kote nchini, kwa watu makini ni ashirio kwamba kuna baya liko njiani.
Siku zote si kawaida kwa mnyama kakakuona kujitokeza hadharani mitaani hivyo hadi hapo juu ya madai haya ya JWTZ kutengeneza vijiwe mitaani basi mtu usisubiri kuambiwa kwamba tayari HUKUMU KINYUME NA HAKI tayari imeshatoka Magogoni juu ya Ubunge wa Mhe Lema, wiki kadhaa hata kabla ya kesi rufaa yenyewe kuanza kusikilizwa, hivyo wao ni kusubiri tu kuja kutusomea alivyotaka mkuu huyu kama kawaida yake.
Vijana wote nchini macho yetu ni kwenye kesi ya Kamanda Lema Arusha; tumechoka kabisa na maonevu ya Rais Kikwete kutoa maamuzi ya kesi mbaalimbali nchini akiwa Magogoni ... na kama vipi ... !!!