Siyo siri kwamba una haki ama hauna, bongo anayeamuwa hilo ni polisi na wanasiasa walioko madarakani.Haki yako haitokani na katiba na sheria za nchi,haki ya mtanzania inategemeana na utashi wa watawala!
Hili suala la kubambikiziwa kesi mbona tulishazoea kabisa?
Kuna watu wenye pesa ambao walishawahi kuhukumiwa miaka mingi kutokana na makosa yao,lakini amini usiamini.polisi huwa wanaenda mtaani kukamata mtu,anapewa hiyo kesi na anatumukia miaka ya huyo aliyehonga amabye anaachiwa.
Amabalo silijui ni hapo kwenye majina na document kutoka mahakamani kuwa kama ni kweli aliyeshitakiwa ndiye anatumukia kifungo hicho.
Pia kama kuna ujambazi ambao askari wameshiriki ama mkuu wao kahongwa,basi hiyo kesi ili iweze kufungwa,lazima apatikane mtu wa kubambikiziwa hiyo kesi na kuhukumiwa ili tu wafunge faili.
Nina uhakika kabisa kuwa wengi wasiokuwa na makosa wako ndani jela na wale wenye makosa wako nje.Wenye pesa hawakai ndani,na wenye connection na polisi ama wanasiasa pia hawakai ndani.
Na hata kama wakipata kesi,polisi wanaenda tu mtaani kuokoteza raia,na kuwapa hizo kesi ili kufunga mafaili na kuwafumba macho wananchi.
Na mara nyingi kwasababu polisi huwa wanaonekana wamefanya kazi nzuri mara baada ya kusolve kesi na kufunga jalada,basi huwa wanafanya hivyo kwa kwenda kuokoteza watuhumiwa na kuwapa kesi zilizoko kwenye makabrasha huko polisi na wanawapelekea watu mahakamani kwa kesi ambazo siyo zao.
Hili ni la kawaida kabisa bongo,nashangazwa kama kuna ambao hawajui!
Haya yote yanayotokea ni mambo amabyo ni ya kawaida sana bongo,na wengine yalishatuchosha kabisa na ni rahisi sana kujutia kuzaliwa Tanzania!
Sioni ni kwa njia gani tunaweza kumove forward bila mapinduzi,mfumo mzima ni hovyo bongo,na kupigia kelele Arusha peke yake siyo solution bali ni mwanzo tu,ni wananchi wachache sana wanojuwa haki zao na hata wale wenye kuzijua,ni wachache sana wanaamini kuwa zitakaa zipatikane bila rushwa nk....ni maoni tu.