Tinde nsalala
JF-Expert Member
- Feb 12, 2017
- 248
- 253
Jana umenukuliwa ukiongelea mambo mbalimbali yahusuyo gereza, wafungwa na mahabusu waliopo katika gereza kuku la Kisongo. Uliongea mengi. Lakini pamoja na yote, pia aligusia namna mahabusu wa ugaidi wanavyotendwa.
Kwa madai yake eti;
Mosi, wanaonewa!
Pili, kwa alivyofanya utafiti eti wale mahabusu hawana hatia.
Tatu na ndipo hasa hoja yangu ilipo ni kuhusu mahabusu hawa watasababisha machafuko ya kidini. Ndg Lema, tokea lini wewe ni mahakama? Je kama siye, kwanini unatoa hukumu ya eti watu hao wanaonewa?
Jamani, tuziache mahamaka zifanye kazi yake. Binafsi bado naamini mahakama ni chombo huru kabisa. Na ndiyo maana hata ninyi wapinzani na hata ukiwapo wewe Lema daima zimekuwa zikiwatendea haki na ninyi kuzipongeza.
Tusiwe watu wa kuiamini mahakama pale tu inapotenda haki kwa upande wenu tu na kuiona mahakama siyo mtenda haki wakati isipokuwa upande wenu.
Mchana mwema.