Lema: Chagonja haamini kama Rais kaishateua IGP

Lema: Chagonja haamini kama Rais kaishateua IGP

yule bonge chagonja ni katili sana.

Huyu mzee ni katili sana, tena anajifanya anauchungu sana na nchi, anashindwa kuonyesha hayo machungu kwa mwanaye ambaye amemshindwa!! Amelazimsha shule hadi amechoka kwani yeye ni bangi tu!!! Hadi amenyoosha mikono.
 
Nikumbushe tukio moja tu wakati wa Mwema, asante.[/

17th March 2011 09:22 #1


Majambazi waua Polisi wawili kituoni
Majambazi waua Polisi wawili kituoni


Shija Felician, Kahama
MAJAMBAZI 10 waliokuwa wanashikiliwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Kagongwa, wilayani hapa, wamewaua polisi wawili wa kituo hicho kwa risasi na kisha kutoroka.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi wakati majambazi hao walipokuwa kwenye chumba cha mahabusu kituoni hapo.


Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 12:45 usiku baada ya majambazi hao waliokuwa wakituhumiwa kwa makosa
ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha, kumwita mmoja wa askari hao ndani ya mahabusu.


Kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, majambazi hao walimwita askari F5344, PC Salumu Mwanakatwe wakisema kuwa wana shida."Alipofungua mlango wa chumba cha mahabusu walimvuta ndani na kumfunika sweta kichwani kisha kumnyang'anya silaha aliyokuwa nayo aina ya SMG namba 14303612 na kuitumia kumuua," alisema.


Kamanda Kamugisha alisema, baada ya kusikia mlio wa bunduki, askari mwingine mwenye namba F 4964, PC Ngwegwe Dira alikwenda kutoa msaada."Kabla hajafika alipigwa risasi kifuani na kufariki dunia hapohapo na majambazi hao walichukua bastola aina ya Chinese yenye namba XR 7526 aliyokuwa nayo askari huyo na kutokomea nayo," alisema.


Baada ya mauaji hayo, majambazi hayo walitoroka na kati yao wawili ambao walikuwa wamefungwa pingu pamoja, waliikata kwa risasi na kukimbia na bastola lakini mmoja alishindwa kukimbia.


"Jambazi huyo (aliyeshindwa kukimbia) aliyekuwa anajulikana kwa jina la Audax Bubel akakamatwa na wananchi na kupigwa shoka kichwani lililomwua hapohapo," alisema na kuongeza: "Majambazi tisa waliobaki, walitoroka na bunduki mbili." Kamanda Kamugisha alisema majambazi hao walikuwa wamekamatwa wakihusishwa na matukio mbalimbali ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha katika Mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Tabora na walikuwa wamewekwa mahabusu kwa lengo la kufanyiwa utambuzi.


Kamugisha alitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ambalo linaendeleza msako wa majambazi hayo.
 
Yaani mnataka kusema kuwa Mheshimiwa wa Arusha ni Jambazi Mstaafu??
Hilo lipo wazi Mkuu. Kwa sasa amesitisha tu ujambazi na anashiriki kiaina ila baada ya kuukosa ubunge hapo Oktoba 2015 atakuwa active jambazi
 
Matukio ya kuvamiwa kwa vituo vya polisi hayajaanza sasa wakati wa Ernest Mangu. Nilichobaini kwenye maelezo ya Lema ni kutaka kuwagombanisha IGP Mangu na Mkuu wa Operesheni Chagonja kwa vile ameona kwa sasa Jeshi la Polisi ni moja. Lema ana uzoefu kutokana na kazi yake ya Ujambazi kwamba kunapokuwa na mpasuko ndani ya jeshi la polisi inakuwa ni wahalifu kujipenyeza

Mbona mnabadilisha mada kutoka kwenye issue na kuipeleka kumjadili mtu. Hii habari ni nzito sana, kama viongozi wote walikuwepo pale na imeongelewa bungeni, kwa nini wasingembana jamaa afute kauli zake hizo. Kweli serikali imeshakuwa legelege
 
Hilo lipo wazi Mkuu. Kwa sasa amesitisha tu ujambazi na anashiriki kiaina ila baada ya kuukosa ubunge hapo Oktoba 2015 atakuwa active jambazi

Ivi jambazi huwa anafanywaje? au hii ni propaganda tu, Hadi sasa dola yako imeshindwa kulithibitisha hilo
 
Mara nyingi wabunge huwa wanapewa habari toka sehemu husika ili wakaseme bungeni. Sasa hizi habari za Lema usizipuuze,inawezekana hao polisi wa vyeo vya chini ndiyo wanajua mchezo mzima wa Changoja ila sasa wanakosa pa kusemea na wakaamua njia pekee ni kumpa mbunge akailipue ishu bungeni. Kwahiyo lisemwalo lipo vuta subira huko mbele ukweli utakuja julikana.
Kwa hiyo Godbless Lema ametumwa na majambazi wenzake akaseme bungeni?
 
Wakuu salamaa?

Jana nimemsikikiza mh. Lema, akieleza juu ya sintofahamu ya kuvamiwa vituo vywa police, kupigwa na kupolwa bunduki n.k

Kwa mshangao mkubwa akasema, Kamanda Changoja haamini kama rais kaishafanya uteuzi wa IGP na sasa anafanya sabotage to a new IGP ili aonekane anamapungu kwa kuratibu matukio mbalimbali n.k

Ni kauli nzito sana, na matukio sasa ya aina hii ni mengi sana, tujadili pamoja kwa undani kama kuna kiukweli vile.

Mungu nibariki nifike December tu.

Lema ni alikuwa jambazi hatari wa magari enzi za akina Omar Mahita na kuna habari kuwa mtandao wake umo ndani ya jeshi la polisi hivyo anajua fika anachosema na kwa uzoefu wa kazi yake ya zamani atakuwa na habari za kutosha. Ningekuwa TISS ningemwendea taratibu kuongea naye huenda anasema ukweli.
 
Kuhusu chagonja na wizi wa silaha. Lema yuko sahihi ni kwamba chagonja amesaini na ccm bila mangu kujua mkakati wa kuhujumu uchaguzi wa mwaka huu. Kwa hivyo silaha zinazoibwa zinaandaliwa kukabidhiwa wahuni ili kuvuruga uchaguzi. Na Mangu alitakiwa kufanya yafuatayo:
1. Kumkataa makamo IGP kama lazima awepo basi yeye ndiye apendekeze msaidizi wake mwenye we. Rais akikataa basi naye asikubali uteuzi wa rais.
2. Yeye afanye mabadiliko makubwa kwa makamishina na kuwastaafisha akina chagonja kwa lazima.
3. Atekeleze ushauri wa CIA kuhusu watoto wa mitaani.
 
Mbona mnabadilisha mada kutoka kwenye issue na kuipeleka kumjadili mtu. Hii habari ni nzito sana, kama viongozi wote walikuwepo pale na imeongelewa bungeni, kwa nini wasingembana jamaa afute kauli zake hizo. Kweli serikali imeshakuwa legelege
Kwenye maelezo yangu hakuna sehemu nimemjadili Lema bali nimeeleza sababu za Lema kusema maneno yale bungeni
 
Ni mara chache sana wabunge wa upinzani hasa CHADEMA kutoa shutuma zisizo na ukweli. Kauli ya G Lema ni kubwa na isichukuliwe kimzaha.

Pia aliyetoa amri silaha za moto zitumike kwny maandamo ya CUF week iliyopita nae atsjwe hadharani maana walisema ni amri kutoka ngazi za juu.
 
Siyo kila alizungumzalo mwenda wazimu ni la kiendawazimu. Jaribu kusoma maandishi wanayoandika barabarani na kwenyekuta mijini, mara nyingi kuna reflection ya kitu fulani ndani yake. Kwa hiyo kuiita kauli ya Godbless Lema ni ya kiendawazimu sishangai sana ,Lakini ndani yake kuna mantiki kubwa sana Jeshi la Polisi na vyombo vinginevyo vya usalama vifanyie kazi jambo hilo.Kama wataendelea kulipuuza na kuona ni kauli za kisiasa matokeo yake yataonekana muda mfupi sana.Mheshimiwa Waziri mwenye dhamani hiyo ni wake Up call please take action soon.:flame:

Kweli kabisa
 
Kuna tatizo sana la kiuandishi kwa hawa vijana wa sasa, amini nafikiri alikua na maana ya haamini. Mtu anataka kuandika ''haoni'' yeye ataandika ''aoni''. Kuna omission za baadhi ya herufi hasa ''h'' bila sababu na wakati mwingine inaharibu kabisa maana ya neno husika. Kuna tatizo somewhere huko mashuleni kwa sababu ni wengi sana walio na uandikaji huo hata katika sms kwenye simu.


Tatizo ni kubwa mnoooo, kunasiku niliweka thread hapa muhimu BAKITA wakawa wanapita huku NA kusahihisha, wakanipopoa mawe. Lugha inaharibiwa tunakaa kuwachekea kama tunavyowachekea mafisadi...
 
Ndugu frema 120, unahoja nzuri sana lakini lifanyie kazi hili la kuiacha herufi H linabadili kabisa maana ya kile unachotaka kutueleza. Mfano hapo umeandika ataweza kumsahau lakini ulikua na maana hataweza kumsahau.

Mkuu ujumbe umeuelewa? Kama umeuelewa mambo mengine achana nayo. Hizi ni social media, asipotumia lugha rasmi (ilimradi ujumbe umeuelewa) athari sio nzito kama kwenye machapisho yanayohitaji "formal writing".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom