Lema awaliza NCCR Manyara, kigogo ahamia CHADEMA!

Lema awaliza NCCR Manyara, kigogo ahamia CHADEMA!

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,761
Naibu katibu mkuu Bara chama cha NCCR Bwana Laurent Sarumbu Tara ambaye pia ni diwani wa miaka yote kupitia NCCR toka mageuzi yalipoanza na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Babati Vijijini na kushindwa kwa kuibiwa kura, leo tarehe 17.12.2012 ameamua kuachia nafasi zake zote ikiwemo nafasi ya udiwani katika kata ya Bashnet na kupokelewa na mjumbe wa kamati kuu katika mkutano wa waandishi rasmi na makamanda wa CHADEMA na sasa Kamanda Lema yuko njiani kuelekea Kagera ambako atapokea magamba katika majimbo mbalimbali..


Mapambano yanaendelea…hakuna kulala mapaka mafisadi, majangili, wauwaji walale…

=========
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Lawrence Tara, amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa CHADEMA na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga.

Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame NCCR-Mageuzi na kujiunga na CHADEMA; upendeleo na dhuluma kwa watumishi wa chama hicho.

Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.


Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya chama hicho kumtelekeza katika kudai haki yake ya ubunge aliyodai kwamba iliporwa na CCM.

"Tunahitaji chama cha siasa kilicho makini na ambacho Watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR-Mageuzi siyo chama cha aina hiyo," alisema Tara.

Akifafanua madai ya kudhulumiwa na CCM, Tara alidai kwamba alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini, lakini akadhulumiwa.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo mojawapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na hali hiyo na ambacho baadhi ya viongozi wake wanaendeleza upendeleo wa urafiki na undugu.

"Nikaona bora kujitenga na kuachana na chama chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama imara ambacho hakina simile na mambo kama hayo. Pia chenye kupigania haki, ukweli na ambacho kimepania utawala bora na ustawi wa Watanzania," alisema.
"Ninaamini Chadema ni chama makini kilichopania kutokomeza dhuluma, uovu na ufisadi wa kidola na kuleta ustawi wa Tanzania," alisema na kuwaomba wakazi wa Bashnet, Manyara na



Watanzania kumuunga mkono.
Akizungumza katika mkutano huo, Lema alimpongeza Tara na kusema chama hicho sasa kimeongezewa nguvu.

"Huyu ni sawa na Leonel Messi (mchezaji soka mahiri wa klabu ya Barcelona na Argentina). Sasa huwezi kumleta achezee AFC ya Arusha na Babati Stars halafu mpate mafanikio kutokana na mfumo uliopo, huyu anatakiwa awe Manchester United au timu nyingine kubwa," alisema Lema.

Alisema viongozi wa chama chake badala ya kumpa ushirikiano ili aweze kushinda ubunge, Mwenyekiti wake alikubali kupewa ubunge wa kuteuliwa na Rais na hivyo Tara kuachwa mwenyewe.

"Uso umeumbwa na haya kuna vitu ukishakula huwezi kupinga. Hivyo jambo bora ni kuondoka huko na kwa hili nampongeza Tara kwa kuacha vyeo vyote ikiwemo posho za vikao vya udiwani na posho ya kila mwezi," alisema Lema.

Alisema Tara anatarajiwa kupewa kadi ya chama hicho na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe au Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa kwa kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kutokana na nafasi kubwa aliyokuwa nayo mwanachama
huyo mpya.


Mbatia amtakia heri, Ruhuza aduwaa

Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia alisema anamtakia kila la heri Tara, kwani Katiba ya nchi inamruhusu mtu yeyote kujiunga na chama anachokitaka.
"Unajua kila neno linazaa neno. Hilo la kusema hatukumpa ushirikiano wakati wa kesi yake ni wazo lake. Namtakia kila la heri huko alipokwenda kwani yeye ana uhuru wa kujiunga na chama chochote. Kama anaona kile anachotaka anaweza kupata sehemu nyingine, aende hakuna tatizo," alisema Mbatia.


Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza alionyesha kushangazwa na hatua hiyo ya Tara alisema kuwa, alikuwa katika nafasi nzuri ya kushinda ubunge wa Babati Vijijini kwa njia ya Mahakama kupitia chama hicho.

"Sijawasiliana naye. Nimeona tu kwenye mtandao kwamba amehamia CHADEMA, lakini ni haki yake kwa vile ana haki ya kuhamia chama chochote," alisema Ruhuza.
Alisema kitendo cha kada huyo kusema amehama kwa kuwa chama kilimtelekeza, ni uongo kwa kuwa NCCR kilimlipia kila kitu katika kesi yake ya kuwania ubunge wa Babati Vijijini na hata kumpa gari ambalo analitumia hivi sasa.

"Aligombea ubunge na udiwani pale Babati Vijijini, lakini alishinda udiwani na kushindwa ubunge, kwa kuwa tafiti zetu tulizofanya alishinda, tulimlipia wakili asimamie kesi ya kupinga matokeo ambayo inaonyesha angeshinda," alisema Ruhuza.

Alisema ameshangazwa zaidi na kauli yake ya kutelekezwa na chama wakati akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama.

"Huyo amekosa kila kitu, ubunge ambao angeweza kuupata kwa njia ya Mahakama, Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu na nyinginezo. Ingekuwa ninaamini mambo ya uchawi ningesema labda huyo jamaa amerogwa," alisema Ruhuza na kuongeza:
"Hata gari la chama aina ya Double Cabin analotumia itabidi alirudishe baada ya kujiondoa kwenye chama.


*******M4C WITH NO APOLOGY******
PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
========


https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/240231-hatima-ya-mbunge-wa-babati-ccm-leo.html
 
Mjumbe wa kamati kuu chama cha NCCR Bwana Laurent Sarumbu Tara ambaye pia ni diwani wa miaka yote kupitia NCCR toka mageuzi yalipoanza na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Babati Vijijini na kushindwa kwa kuibiwa kura, leo tarehe 17.12.2012 ameamua kuachia nafasi zake zote ikiwemo nafasi ya udiwani katika kata ya Bashnet na kupokelewa na mjumbe wa kamati kuu katika mkutano wa waandishi rasmi na makamanda wa CHADEMA na sasa Kamanda Lema yuko njiani kuelekea Kagera ambakoatapokea magamba katika majimbo mbalimbali..

Mapambano yanaendelea…hakuna kulala mapaka mafisadi, majangili, wauwaji walale…

yap! hiyo ndo demokrasia bwana.unahama unavyotaka,nenda kamanda ,nenda.
 
Mjumbe wa kamati kuu chama cha NCCR Bwana Laurent Sarumbu Tara ambaye pia ni diwani wa miaka yote kupitia NCCR toka mageuzi yalipoanza na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Babati Vijijini na kushindwa kwa kuibiwa kura, leo tarehe 17.12.2012 ameamua kuachia nafasi zake zote ikiwemo nafasi ya udiwani katika kata ya Bashnet na kupokelewa na mjumbe wa kamati kuu katika mkutano wa waandishi rasmi na makamanda wa CHADEMA na sasa Kamanda Lema yuko njiani kuelekea Kagera ambakoatapokea magamba katika majimbo mbalimbali..

Mapambano yanaendelea…hakuna kulala mapaka mafisadi, majangili, wauwaji walale…
Merciless M4C.
Dhambi ya kufoji kadi Dr. Slaa wataijutia ccm hawa!
 
Nadhani wamekuwa na press comference pale kibo palace coz punde nimemuona kamanda lema pale..pamoja bw.Tara
 
Huyu jamaa (G.Lema) bora wangemuachiaga UBUNGE wake, maana amekuwa na impact kubwa zaidi katika kukijenga chama chake.
Mkuu umeona eeeh!!

Juzi hapa Lumumba walikuwa wanajadili nini cha kufanya kuhusu Lema, maana hasara ya kisiasa ambayo CCM imeipata kwa miezi sita toka wamemvua ubunge Lema ni kubwa sana.
 
Huyu jamaa (G.Lema) bora wangemuachiaga UBUNGE wake, maana amekuwa na impact kubwa zaidi katika kukijenga chama chake.
Ameapa kuanzia mwakani Do or die...na jumamosi tulichangia pesa ya kununua vifaa vya matangazo na canter itakayo mwezehsa kufanya mikutano kijiji kwa kiji na makamnda wengine bila kutegemea vifaa vya makao makuu au kukodisha mabavyo walikuwa wakiwekewa mashari makubwa na ni gharama kubwa pia sasa itabaki kuwa wezesha pesa ya chakula na mafuta na watakuwa wanajipikilisha wanapokuwa vijijini...
 
Lema awaliza Nccr Manyara , Mjumbe wa Kamati kuu na Naibu katibu mkuu bara chama cha Nccr mageuzi Bwana Laurent Sarumbu Tara ambaye pia ni diwani wa miaka yote kupitia Nccr toka Mageuzi yalipoanza na aliyekuwa Mgombea ubunge ktk jimbo la Babati Vijijini na kushindwa kwa kuibiwa kura , leo tarehe 17 ameamua kuachia nafasi zake zote ukiwemo nafasi ya udiwani ktk kata ya Bashnet nakupokelewa na Mjumbe wa kamati kuu katika mkutano wa waandishi habari mjini Babati na kujiunga rasmi na makamanda wa Cdm na sasa Kamada lema yuko njiani kuelekea Kagera ambako atapokea magamba ktk majimbo mbali mbali
 
Breaking News za Lema naona kila mpambe anakuja na yake.
 
Crashwise Asante sana kwa Taarifa hii.Mfikishie salam.Lema mwambie makamanda tuko nyuma yake

Kamanda Tara karibu nyumbani,njoo uungane na watanzania wazalendo kukomboa nchi.
 
Last edited by a moderator:
Hakika Mbunge Mtarajiwa.
Soma hili bandiko jamaa ni mbwanga mgombea wa CCM yakapinduliwa semamahakama zetu na sapoti kutoka kwenye chama chake inaelekea haikuwepo...
Novemba 2010, Tara ambaye ni Diwani wa Kata ya Bashnet alifungua kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa Februari 16, mwaka huu akiiomba Mahakama hiyo imtangaze kuwa mbunge halali wa jimbo hilo kwani ndiye mshindi halali wa jimbo hilo na kudai kuwa alishinda kwa tofauti ya kura 58 baada ya kupata kura 32,248 na Jituson kura 32,190.

Tara katika madai yake, aliiomba Mahakama hiyo itangaze kuwa matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa sasa ni batili kwani yalikiuka taratibu za kisheria za uchaguzi na kanuni zake mwaka 2010.


Chanzo: Gazeti la MWANANCHI
 
Back
Top Bottom