Lema awaliza NCCR Manyara, kigogo ahamia CHADEMA!

CHADEMA kiongozi ni zito namkubali sana mtu huyu but lema asome vitabu inaonekana hapitii nakala ni mropokaji tu
Ama kweli wewe ni mwabudu sanamu, umebadili jinalo tena kumtumikia nape! Ni kweli Zito anafaa sana je yeye mwenyewe atosha hahitji chama ? kwa nini asiwe mgombea wako binafsi mkawaacha wanaoamini katika timu ya watu. Au kwako Mesi atosha kucheza pekee yake dhidi ya timu yoyote? Bhuchilhu bhutahupaga ntwe! Nasikitika mtu mwenye digrii akajipa uhouseboy wa mjinga
 
hakuna cha ukamanda LEMA sio kiongozi ni mpiga debe tu kuweni makini nae atueleze zile milioni mia alizopewa marekani kazipeleka wapi?sio kujifanya kamanda wakati hata mgamboo hajapita
Sasa naona yale mataputapu uliyokunywa pale Lumumba umeanza kutapika humu.
Ukianza kuharisha tu, tunakuwaisha haraka hospitali.
 
CHADEMA kiongozi ni zito namkubali sana mtu huyu but lema asome vitabu inaonekana hapitii nakala ni mropokaji tu
Zito bado hajaoa na anatafuta mchumba kwa hali na mali.
Sasa unaonaje kama ikiwezekana mkutane?
 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Lawrence Tara, amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa CHADEMA na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga.

Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame NCCR-Mageuzi na kujiunga na CHADEMA; upendeleo na dhuluma kwa watumishi wa chama hicho.

Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.

Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya chama hicho kumtelekeza katika kudai haki yake ya ubunge aliyodai kwamba iliporwa na CCM.

"Tunahitaji chama cha siasa kilicho makini na ambacho Watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR-Mageuzi siyo chama cha aina hiyo," alisema Tara.

Akifafanua madai ya kudhulumiwa na CCM, Tara alidai kwamba alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini, lakini akadhulumiwa.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo mojawapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na hali hiyo na ambacho baadhi ya viongozi wake wanaendeleza upendeleo wa urafiki na undugu.

"Nikaona bora kujitenga na kuachana na chama chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama imara ambacho hakina simile na mambo kama hayo. Pia chenye kupigania haki, ukweli na ambacho kimepania utawala bora na ustawi wa Watanzania," alisema.
"Ninaamini Chadema ni chama makini kilichopania kutokomeza dhuluma, uovu na ufisadi wa kidola na kuleta ustawi wa Tanzania," alisema na kuwaomba wakazi wa Bashnet, Manyara na

Watanzania kumuunga mkono.
Akizungumza katika mkutano huo, Lema alimpongeza Tara na kusema chama hicho sasa kimeongezewa nguvu.

"Huyu ni sawa na Leonel Messi (mchezaji soka mahiri wa klabu ya Barcelona na Argentina). Sasa huwezi kumleta achezee AFC ya Arusha na Babati Stars halafu mpate mafanikio kutokana na mfumo uliopo, huyu anatakiwa awe Manchester United au timu nyingine kubwa," alisema Lema.

Alisema viongozi wa chama chake badala ya kumpa ushirikiano ili aweze kushinda ubunge, Mwenyekiti wake alikubali kupewa ubunge wa kuteuliwa na Rais na hivyo Tara kuachwa mwenyewe.

"Uso umeumbwa na haya kuna vitu ukishakula huwezi kupinga. Hivyo jambo bora ni kuondoka huko na kwa hili nampongeza Tara kwa kuacha vyeo vyote ikiwemo posho za vikao vya udiwani na posho ya kila mwezi," alisema Lema.

Alisema Tara anatarajiwa kupewa kadi ya chama hicho na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe au Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa kwa kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kutokana na nafasi kubwa aliyokuwa nayo mwanachama
huyo mpya.

Mbatia amtakia heri, Ruhuza aduwaa

Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia alisema anamtakia kila la heri Tara, kwani Katiba ya nchi inamruhusu mtu yeyote kujiunga na chama anachokitaka.
"Unajua kila neno linazaa neno. Hilo la kusema hatukumpa ushirikiano wakati wa kesi yake ni wazo lake. Namtakia kila la heri huko alipokwenda kwani yeye ana uhuru wa kujiunga na chama chochote. Kama anaona kile anachotaka anaweza kupata sehemu nyingine, aende hakuna tatizo," alisema Mbatia.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza alionyesha kushangazwa na hatua hiyo ya Tara alisema kuwa, alikuwa katika nafasi nzuri ya kushinda ubunge wa Babati Vijijini kwa njia ya Mahakama kupitia chama hicho.

"Sijawasiliana naye. Nimeona tu kwenye mtandao kwamba amehamia CHADEMA, lakini ni haki yake kwa vile ana haki ya kuhamia chama chochote," alisema Ruhuza.
Alisema kitendo cha kada huyo kusema amehama kwa kuwa chama kilimtelekeza, ni uongo kwa kuwa NCCR kilimlipia kila kitu katika kesi yake ya kuwania ubunge wa Babati Vijijini na hata kumpa gari ambalo analitumia hivi sasa.

"Aligombea ubunge na udiwani pale Babati Vijijini, lakini alishinda udiwani na kushindwa ubunge, kwa kuwa tafiti zetu tulizofanya alishinda, tulimlipia wakili asimamie kesi ya kupinga matokeo ambayo inaonyesha angeshinda," alisema Ruhuza.

Alisema ameshangazwa zaidi na kauli yake ya kutelekezwa na chama wakati akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama.

"Huyo amekosa kila kitu, ubunge ambao angeweza kuupata kwa njia ya Mahakama, Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu na nyinginezo. Ingekuwa ninaamini mambo ya uchawi ningesema labda huyo jamaa amerogwa," alisema Ruhuza na kuongeza:
"Hata gari la chama aina ya Double Cabin analotumia itabidi alirudishe baada ya kujiondoa kwenye chama.

*******M4C WITH NO APOLOGY******
PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS
 
.......Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.......

Angalia vizuri huo mwaka uliutaja.
 
Sam Ruhuza; you know the words but you miss their meaning!!

The issue is not about material gain rather it is the vision and the desire for change;

Law Tara wanted to be on board the right vehicle that could lead him to his desired destination. That vehicle happens to be CHADEMA through the M4C.
 
Pole sana Mh Mbatia lakini waruhusu CHADEMA wapate vichwa muhimu ili 2015 CCM waonje joto la kuzidiwa, mi naamin huyu Tara angegombea kwa tiketi ya CHADEMA 2010 tayari angekuwa mjengoni muda huu
 
Pole sana mh mbatia lakini waruhusu chadema wapate vichwa muhimu ili 2015 ccm waonje joto la kuzidiwa, mi naamin huyu tara angegombea kwa tiketi ya cdm 2010 tayari angekuwa mmojawapo wa wabunge
 
Wapinzani wa kweli huunganisha nguvu dhidi ya adui mmoja ambaye ni CCM. Kwa hali jinsi ilivyo mnazidi kutuchanganya wapenda mageuzi. Tatizo hasa ni nini? Acheni uroho wa madaraka na kutafuta umaarufu, kaeni chini mapema ili kujenga misingi imara. Kuja kuungana dakika za mwisho haijengi.
 
katiba ya sasa inakataa kunganisha vyama viwili vilivyo hai! Lazima kimoja kife ndo kiungane na kingine kinacho ishi!
 
lema.jpg

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbess Lema akipeana mkono na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu
wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara) Lawrence Surumbu Tara na Diwani wa kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara
ambaye jana alitangaza kujivua udiwani na vyeo vyote alivyokuwa navyo NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema mjini Babati jana.
​
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Lawrence Tara,
amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
​

Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga.

Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema; upendeleo na dhuluma kwa watumishi wa chama hicho.
Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.

Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya chama hicho kumtelekeza katika kudai haki yake ya ubunge aliyodai kwamba iliporwa na CCM.

“Tunahitaji chama cha siasa kilicho makini na ambacho Watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR-Mageuzi siyo chama cha aina hiyo,” alisema Tara.

Akifafanua madai ya kudhulumiwa na CCM, Tara alidai kwamba alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini, lakini akadhulumiwa.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo mojawapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na hali hiyo na ambacho baadhi ya viongozi wake wanaendeleza upendeleo wa urafiki na undugu.

“Nikaona bora kujitenga na kuachana na chama chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama imara ambacho hakina simile na mambo kama hayo. Pia chenye kupigania haki, ukweli na ambacho kimepania utawala bora na ustawi wa Watanzania,” alisema.
“Ninaamini Chadema ni chama makini kilichopania kutokomeza dhuluma, uovu na ufisadi wa kidola na kuleta ustawi wa Tanzania,” alisema na kuwaomba wakazi wa Bashnet, Manyara na

Watanzania kumuunga mkono.
Akizungumza katika mkutano huo, Lema alimpongeza Tara na kusema chama hicho sasa kimeongezewa nguvu.

“Huyu ni sawa na Leonel Messi (mchezaji soka mahiri wa klabu ya Barcelona na Argentina). Sasa huwezi kumleta achezee AFC ya Arusha na Babati Stars halafu mpate mafanikio kutokana na mfumo uliopo, huyu anatakiwa awe Manchester United au timu nyingine kubwa,” alisema Lema.

Alisema viongozi wa chama chake badala ya kumpa ushirikiano ili aweze kushinda ubunge, Mwenyekiti wake alikubali kupewa ubunge wa kuteuliwa na Rais na hivyo Tara kuachwa mwenyewe.

“Uso umeumbwa na haya kuna vitu ukishakula huwezi kupinga. Hivyo jambo bora ni kuondoka huko na kwa hili nampongeza Tara kwa kuacha vyeo vyote ikiwemo posho za vikao vya udiwani na posho ya kila mwezi,” alisema Lema.

Alisema Tara anatarajiwa kupewa kadi ya chama hicho na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe au Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa kwa kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kutokana na nafasi kubwa aliyokuwa nayo mwanachama huyo mpya.

​
 
KWA UELEWA NILIONAO MWANACHAMA wa chama kimoja anaweza kuhamia chama kingne kwa sababu nying, lakin miongoni mwa sababu kubwa ni pamoja:
1.chama alichopo kukosa muelekeo (kwa maana ya kuwa na uongozi usio madhubuti na hivyo kua mkusanyiko wa watu).
2.Kushindwa kufikia malengo yake kupitia chama hicho (kama kua kiongozi,kufanikisha maisha bora,kufahamika na nk).
3.Kuona chama alichopo hakina sera bora na nzuri katika kumkomboa mwananchi na hivyo kwenda chama ambacho yeye anaona kina sera bora.
BINAFSI WAKATI NAANZA KUZIONA SIASA ZA VYAMA VYINGI NA HASA NCCR NILIANZA KUMUONA TARA,AMEDUMU KWA MIONGO KADHAA AKIGOMBEA AKIWA NCCR INGAWA AMEKUA MARA ZOTE AKIKOSA BAHATI/FURSA YA KUA MBUNGE WA BABATI VIJIJINI!!

JE?,NI SABABU ZIPI ZILIZOMPELEKEA TARA KUHAMA NCCR INGAWA ALIKIPENDA NA KUKITUMIKIA CHAMA HICHO KWA MDA MREFU???....
 
Mkuu ishu ya Tara sidhani kama kuna yaliyomsibu,yule jamaa since 2005 aligombea na akatisha kiasi,2010 magamba yakamfanyia hujuma(uwizi wa kura),na kesi ipo mahakamani nadhani pia kuna uwezekano wa kushinda kesi dhidi ya Jitu Patel.

Ila jamaa atakuwa kasoma upepo maana ukifanya tathmini babati vijijini baada ya uchaguzi 2010 chadema imeanza kusikika sana na watu kuipuuzia nccr-mageuzi,nadhani jamaa atakuwa na idea ya kugombea kupitia chadema 2015.
 
SIASA

lema.jpg

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbess Lema akipeana mkono na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara) Lawrence Surumbu Tara na Diwani wa kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara ambaye jana alitangaza kujivua udiwani na vyeo vyote alivyokuwa navyo NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema mjini Babati jana. Picha na Joseph Lyimo​

Na Joseph Lyimo, Babati

Posted Jumanne,Decemba18 2012 saa 9:17 AM

KWA UFUPI

NI NAIBU KATIBU MKUU, LAWRENCE TARA, ATAJA SABABU LUKUKI, MBATIA AKUBALI YAISHE

​
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Lawrence Tara, amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga.

Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema; upendeleo na dhuluma kwa watumishi wa chama hicho.
Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.

Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya chama hicho kumtelekeza katika kudai haki yake ya ubunge aliyodai kwamba iliporwa na CCM.

"Tunahitaji chama cha siasa kilicho makini na ambacho Watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR-Mageuzi siyo chama cha aina hiyo," alisema Tara.

Akifafanua madai ya kudhulumiwa na CCM, Tara alidai kwamba alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini, lakini akadhulumiwa.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo mojawapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na hali hiyo na ambacho baadhi ya viongozi wake wanaendeleza upendeleo wa urafiki na undugu.

"Nikaona bora kujitenga na kuachana na chama chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama imara ambacho hakina simile na mambo kama hayo. Pia chenye kupigania haki, ukweli na ambacho kimepania utawala bora na ustawi wa Watanzania," alisema.

"Ninaamini Chadema ni chama makini kilichopania kutokomeza dhuluma, uovu na ufisadi wa kidola na kuleta ustawi wa Tanzania," alisema na kuwaomba wakazi wa Bashnet, Manyara na

Watanzania kumuunga mkono.
Akizungumza katika mkutano huo, Lema alimpongeza Tara na kusema chama hicho sasa kimeongezewa nguvu.

"Huyu ni sawa na Leonel Messi (mchezaji soka mahiri wa klabu ya Barcelona na Argentina). Sasa huwezi kumleta achezee AFC ya Arusha na Babati Stars halafu mpate mafanikio kutokana na mfumo uliopo, huyu anatakiwa awe Manchester United au timu nyingine kubwa," alisema Lema.

Alisema viongozi wa chama chake badala ya kumpa ushirikiano ili aweze kushinda ubunge, Mwenyekiti wake alikubali kupewa ubunge wa kuteuliwa na Rais na hivyo Tara kuachwa mwenyewe.

"Uso umeumbwa na haya kuna vitu ukishakula huwezi kupinga. Hivyo jambo bora ni kuondoka huko na kwa hili nampongeza Tara kwa kuacha vyeo vyote ikiwemo posho za vikao vya udiwani na posho ya kila mwezi," alisema Lema.

Alisema Tara anatarajiwa kupewa kadi ya chama hicho na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe au Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa kwa kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kutokana na nafasi kubwa aliyokuwa nayo mwanachama huyo mpya.

Mbatia amtakia heri, Ruhuza aduwaa
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia alisema anamtakia kila la heri Tara, kwani Katiba ya nchi inamruhusu mtu yeyote kujiunga na chama anachokitaka.

"Unajua kila neno linazaa neno. Hilo la kusema hatukumpa ushirikiano wakati wa kesi yake ni wazo lake. Namtakia kila la heri huko alipokwenda kwani yeye ana uhuru wa kujiunga na chama chochote. Kama anaona kile anachotaka anaweza kupata sehemu nyingine, aende hakuna tatizo," alisema Mbatia.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza alionyesha kushangazwa na hatua hiyo ya Tara alisema kuwa, alikuwa katika nafasi nzuri ya kushinda ubunge wa Babati Vijijini kwa njia ya Mahakama kupitia chama hicho.

"Sijawasiliana naye. Nimeona tu kwenye mtandao kwamba amehamia Chadema, lakini ni haki yake kwa vile ana haki ya kuhamia chama chochote," alisema Ruhuza.

Alisema kitendo cha kada huyo kusema amehama kwa kuwa chama kilimtelekeza, ni uongo kwa kuwa NCCR kilimlipia kila kitu katika kesi yake ya kuwania ubunge wa Babati Vijijini na hata kumpa gari ambalo analitumia hivi sasa.

"Aligombea ubunge na udiwani pale Babati Vijijini, lakini alishinda udiwani na kushindwa ubunge, kwa kuwa tafiti zetu tulizofanya alishinda, tulimlipia wakili asimamie kesi ya kupinga matokeo ambayo inaonyesha angeshinda," alisema Ruhuza.

Alisema ameshangazwa zaidi na kauli yake ya kutelekezwa na chama wakati akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama.

"Huyo amekosa kila kitu, ubunge ambao angeweza kuupata kwa njia ya Mahakama, Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu na nyinginezo. Ingekuwa ninaamini mambo ya uchawi ningesema labda huyo jamaa amerogwa," alisema Ruhuza na kuongeza:

"Hata gari la chama aina ya Double Cabin analotumia itabidi alirudishe baada ya kujiondoa kwenye chama."

NCCR Culturally Sio CHAMA Wabunge wake ni Wananchi Wanawapenda SIO CHAMA; Na Mwenyekiti wao KUPATA UBUNGE ni RAIS kumpenda kama MVURUGAJI DEMOKRASIA NCHINI...
 
Always Lema is very, very serious when it comes emancipation time! This man has done a lot for the last 8 months. Kudos!
 
Back
Top Bottom