Hatima ya mbunge wa Babati (CCM) leo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatima ya mbunge wa Babati (CCM) leo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Mar 28, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  Hatima ya Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini (CCM), Virajilal Jitu Son itajulikana leo wakati Mahakama Kuu Kanda ya Arusha itakapotoa hukumu ya kesi ya kupinga ubunge wake iliyofunguliwa na aliyegombea ubunge wa jimbo hilo, Laurence Surumbu Tara (NCCR Mageuzi).

  Kesi hiyo namba 12/2010 ipo mbele ya Jaji Fatuma Massengi na ilifunguliwa Novemba 2010 na kuanza kusikilizwa Februari 16, mwaka huu huku wadaiwa wakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Jituson.

  Novemba 2010, Tara ambaye ni Diwani wa Kata ya Bashnet alifungua kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa Februari 16, mwaka huu akiiomba Mahakama hiyo imtangaze kuwa mbunge halali wa jimbo hilo kwani ndiye mshindi halali wa jimbo hilo na kudai kuwa alishinda kwa tofauti ya kura 58 baada ya kupata kura 32,248 na Jituson kura 32,190.

  Tara katika madai yake, aliiomba Mahakama hiyo itangaze kuwa matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa sasa ni batili kwani yalikiuka taratibu za kisheria za uchaguzi na kanuni zake mwaka 2010.


  Chanzo: Gazeti la MWANANCHI
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  yetu masikio!
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  dah! Kazi kweli kweli, magamba haya! Mmmh
   
 4. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sometimes tunajikuta tunafanya kazi kwa shinikizo la Wanasiasa - "Rtd Judge, Ramadhani"
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sheria yetu ya uchaguzi hata ukishinda kwa kura 1 unatangazwa mshindi hivyo tofauti ya kura 58 ni kubwa
   
 6. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Tupashane matokeo yatakavyokuwa.
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kesi ya ngedere kapelekewa sokwe, nadhani dhahiri huyu wa ccm atashinda
   
 8. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Jitahidi mkuu utupatie habari zaidi hapo baadae
   
 9. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  It is very dangerous when political motives influence judiciary system!Mhimili wa kutoa haki unapoingiliwa na siasa that society is as good as a dead one!!majaji zingatieni weleni na taaluma zenu, acheni kupinda sheria kwa manufaa ya kisiasa,.machafukuo yakitoea hamtatoka salama!!
   
 10. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hawajaanza kusoma hiyo hukumu ya Jitu Soni?
   
 11. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,096
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  ccm kashinda mkuu waambie ukweli....
   
 12. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,096
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  nilikuwa naifwatilia pia kama jicho la ngombe lakini ndio hivyo ....huku akuna asilimia 50 ndio ushinde ukizidi moja kura mshindi kazi kweli kweli
   
 13. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Habari nilizopata sasa hivi ni kwamba mheshimiwa jitu soni kashinda!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  kumbe haya matokeo siyo halali! chama alichogombea nacho bana dah!
  [TABLE="class: arc90_altrows-Blue, width: 100%"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]MANYARA
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]WILAYA YA BABATI[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #B3D5E6, colspan: 4"]BABATI VIJIJINI[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%, bgcolor: #B3D5E6"]Candidate[/TD]
  [TD="width: 20%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
  Political Party
  [/TD]
  [TD="width: 20%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
  Number of Votes
  [/TD]
  [TD="width: 15%, bgcolor: #B3D5E6, align: center"]
  Percentage Votes
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"]JITU VRAJLAL SONI[/TD]
  [TD="width: 20%"]
  CCM
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]32,777[/TD]
  [TD="width: 15%"]44.32[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"]TARA LAWRENCE SUMBURU[/TD]
  [TD="width: 20%"]
  NCCR-MAGEUZI
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]31,635[/TD]
  [TD="width: 15%"]42.77[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"]FRANCIS PHILIP QAMARA[/TD]
  [TD="width: 20%"]
  CHADEMA
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]6,367[/TD]
  [TD="width: 15%"]8.61[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"]HICHEKA GODFREY NGOGOMBA[/TD]
  [TD="width: 20%"]
  APPT - MAENDELEO
  [/TD]
  [TD="width: 20%"]900[/TD]
  [TD="width: 15%"]1.22[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"] [/TD]
  [TD="width: 20%"] [/TD]
  [TD="width: 5%"] [/TD]
  [TD="width: 15%"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 10%"]SPOILT VOTES[/TD]
  [TD="width: 20%"] [/TD]
  [TD="width: 20%"]2,282[/TD]
  [TD="width: 15%"]3.09[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 10%"]TOTALS[/TD]
  [TD="width: 20%"] [/TD]
  [TD="width: 20%"]73,961[/TD]
  [TD="width: 15%"]100[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 30%"] [/TD]
  [TD="width: 20%"] [/TD]
  [TD="width: 5%"] [/TD]
  [TD="width: 15%"]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. D

  Dr Gustav Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi ipo hatuna tume huru Tanzania kwa hiyo wachache wamekaa mahali walipo kihalali,watanzania tumuogope Mungu.
   
 16. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hizo kura 2,282 zilizoharibika zingetosha kumpa Tara ushindi. Na hilo Jitu linakaa bunge la Kenya au Rwanda. Maana sijawahi kulisikia likichangia mjadala hata mmoja.

   
 17. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Dullonet
  – January 17, 2012

  Posted in: Habari Mchanganyiko

  JAJI Kiongozi, Fakihi Jundu amesema Mahakama imelemewa na mzigo wa kesi za uchaguzi ambazo imeshindwa kuziendesha kutokana na kupewa bajeti finyu na kusema kwamba ikiwa hadi kufikia Mei mwaka huu haitakuwa imepewa fedha ilizoomba, itarejesha kesi hizo bungeni.Amesema hadi sasa Serikali imetoa Sh300 milioni kati ya Sh2.3 bilioni zilizoombwa na mhimili huo wa dola na kuonya kuwa kama fedha hizo hazitapatikana watazirudisha kesi hizo bungeni. Mahakama Kuu imeshapokea kesi 43 zilizofunguliwa kupinga matokeo baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana baada ya kumwapisha, Batista John Mhelela kuwa Kaimu Msajili wa Mahakama Kuu Sumbawanga, Jaji Jundu alisema kwa sasa Mahakama inakabiliwa na hali ngumu ya fedha.

  “Tayari muda wa kawaida umeshakwisha na tumeomba muda wa nyongeza wa miezi sita ambao nao unakwisha Mei mwaka huu. Kama fedha zitakuwa hazitapatikana baada ya muda huo, itabidi suala hilo tulirudishe bungeni,” alisema.
  Hata hivyo, alipotakiwa kuzungumzia madai hayo ya Jaji Jundu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alisema: “Mambo yanayohusu Mahakama ni vyema wakatuandikia moja kwa moja, lakini mimi ninachojua ni kuwa tumetoa fedha nyingi zaidi ya hizo.”

  Kesi za uchaguzi

  Akitoa taarifa Desemba 16, 2010, ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa, Jaji Jundu alisema jumla ya kesi 43 zilikuwa zimefunguliwa katika vituo 11 kati ya 13 vya Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga matokeo ya ubunge, katika majimbo mbalimbali.

  Alitoa angalizo kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiitaka ijiandae na kuwezeshwa ili kuruhusu mashauri hayo kuendelea na kumalizika kwa wakati bila kukwama.

  Alisema katika kuyashughulikia mashauri hayo kwa wakati na kwa haki, inakadiriwa kuwa kiasi cha Sh2.263 bilioni kitahitajika na kwamba kila kesi itagharimu kiasi cha Sh52,644,000, huku akisisitiza kuwa huo mzigo ni lazima ubebwe na Serikali.

  Source: Mwananchi la January 2012

  About Dullonet
  MY TAKE: Ni kwamba Serikali haina pesa za kuendeshea kesi za Uchaguzi na kurudia uchaguzi. hivyo tusitegemee kabisa kama kuna Jimbo au Kata yenye utata na kupinga matokeo ya uchaguzi kama Chaguzi zitarudiwa.

  Kinachofanyika ni kwamba Mahakama hata kama itasikiliza hiyo kesi Basi uamuzi utakuja kuelemea upande wa Kiongozi aliyetajwa kuwa ameshinda hapo awali. Tusitegemee matokeo kubadilishwa katika kipindi hiki kigumu cha Uchumi wa Tanzania.

  Hii ni kutokana na utabiri wangu  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...