Wadau na wananchi hii ya Tanzania, leo shetani ameshndwa akiwa na majeshi yake yote, alijaribu kuwatesa watu wema kama watamkufuru Mungu akashindwa, akaanzisha zali la kuwafungulia mashitaka ya uongo km la Prof. Mahalu hapo akala mafumbi kama alivyoamuriwa tokea zamani, sasa wakati wake wa kwenda kuchomwa moto umewadia. Kilichotokea leo ni AIBU KUBWA kwa mamlaka inayoteua majaji na vigezo vinavyotumika. Tujiulize ni watanzani wangapi wamepelekwa lupango kwa hukumu za kupikwa kama hizi? Nimetafakari kwa kina nikagundua kuwa kuna shida kwenye mfumo mzima wa utoaji haki kuanzia mahakamu kuu hadi za mwanzo za mabaraza ya ARDHI, eee Mwenyezi Mungu shusha rungu lako kwa wale wanaofurahia dhuluma na manyanyaso kwa masikini wasio na pesa.