Kama kuna makosa ya kisiasa ambayo CCM walifanya na watayajutia sana, ni siasa za Arusha.
Arusha ndio pameonesha wazi jinsi ambavyo watawala wanataka kupindisha sheria kwa maslahi yao ya kisiasa.
Hii imefanya hata waliokuwa wakereketwa wa CCM, lakini ni wapenda haki, wakichukie chama.
Hii pia imekuwa reference ya wazi hata sehemu nyingine za mbali na Arusha.
CCM itafakari vema maneno ya Injili:
Kwa maana, ni nani miongoni mwenu ambaye akitaka kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama zake ili ajue kama ana kiasi chakutosha cha kumalizia? La sivyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, watu watamcheka wakisema: `Mtu huyu alianza kujenga, lakini hakumalizia.`"Au, ni mfalme gani ambaye, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, hataketi kwanza chini na kufikiri kama ataweza, kwa askariwake elfu ishirini? Kama anaona hataweza, atawatuma wajumbe kutaka masharti ya amani wakati mfalme huyo mwingine angali mbali.
Lk. 14:28-32