TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,762
- 21,228
Wadau wa legacy leo tunalegacy yetu hapa Zanzibar inayotokana aliyekuwa rias wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa inayofanyika kwa mara ya pili na sasa inafanyika nchini Zanzibar kisiwani Unguja.
PHOTO: aliyekuwa Rais wa Msumbuji Joachim Chisano akiongea katika kongamano hilo.
Rais wa Tanzania Mama Samia Suruhi Hassan ndiye mgeni rasmi kwenye hili kongamano la pili juu ya kumbukumbu ya rais Benjamin Mkapa Zanzibar.
Wakati nchi yetu ikijinasibu kutumia kugha ya kiswahili na kukipa hamasa kutumika katika nyanja za kimataifa na OAU tayari inakitambua kuwa ya lugha kubwa inayokuwa kwa kasi, leo hii kuna jambo la kushangaza hapo ukumbuni.
Ndani ya kongamano hili kuna wageni mbalimbali wa kimataifa na wageni kutoka hapa nyumbani Tanzania, wageni waliotoka nje ni wachache kuliko wa hapa hapa ndani ya nchi.
Na hata wageni wa hapa hapa ndani wengi ni mabalozi ambao wanazungumza kiswahili, ila kwa hali iliyopo hapo ukumbuni kinasikika kilugha cha kizungu japo ndg MC balozi Mazura anajaribu kuchanganya Kiswahili na Kizungu.
Wakubwa waliopo hapo mmeshindwa wapi kukipa kiswahili power of kutumika ilihali hata balozi wa marekani anakiongea japo cha kuibia?.
Moderator naomba hii mada isiunganishwe na ile ya live hapa content ni kiswahili siyo tukio.